Maria Roza
JF-Expert Member
- Apr 1, 2009
- 6,802
- 1,606
Poleni sana majeruhi jamni wana jf tuwe tunafuata sheria za barabarani
Poleni waliopata ajali, we must be careful when entering the main road jamani, uwe kwa mguu,pikipiki, gari hata ukiwa ndani ya basi.
Katika vigezo vya kupata leseni ya udereva kuwepo na kipimo cha SAIKOLOJIA. yaani uwezo wa mtu kuicontrol akili yake na kufanya maamuzi sahihi.
Kutoka lango la Mlimani City mpaka round about ni hatua chache, mwendo wa madereva wengi pale ni wa kifo. Inasikitisha kwamba pamoja na barabara kuwa nzuri (one side) lakini haisaidii kupunguza ajali. Matuta ndo suluhisho la pekee kwani hata ile alama ya Zebra huwa hatuiheshimu sisi madereva...
Sooo sad
Tushasema tayari.....Poleni sana, sasa utasikia solutions za kibongo bongo, "Weka matuta hapo"
Pole kwa wahanga wote wa ajali hii, kuna kitu ambacho watu wengi hukipuuzia sana 'seat belts', watu wengine eti wanadhani mikanda ni kwa ajili ya dereva tu, hao kina dada wangevaa mikanda (mshipi) uwezekano wa kusrushwa nje ya gari ungekuwa mdogo sana, na twaweza sema wana bahati maana wakati mwingine unaweza kutupwa barabarani halafu ukapitiwa na gari nyingine.
Usiku wa leo mara tu baada ya kuisha kwa mechi ya mpira kati ya manchester na chelsea imetokea ajali mbaya katika lango la kutokea mlimani city kuingia main road upande unaotazamana na Sinza (siyo upande wa survey)..
Gari aina ya corona premio lilikuwa linatoka Mlimani City na kuingia main road bila kuangalia ambapo gari aina ya altezza likiwa kasi sana limeigonga premio na kuzunguka karibu mara 2.
Watu (wanawake/wasichana) hali zao ni mbaya sana kwani karibu wote walirushwa nje na kutua barabarani..watu waliosogea karibu zaidi yangu wanasema mmoja amekufa palepale na wengine wawili wana hali mbaya wamekimbizwa hospitali. Aliyekuwa kwenye toyota altezza amesalimika kabisa..
Naomba kuwasilisha...