Mmmhhh hii mbona inastua jamani, Jmosi nikiwa napita pale ubungo kituo kidogo cha daladala nikamwona mhubiri mmoja anadai ameokoka na ni mkenya, huyu bwana akaniteka fikra kidogo baada ya kumsikia akisema kwamba ajali ya wale wasanii wa 5 Stars Modern Taarabu ni kafara ya mtu wa Freemason, kiukweli nilistuka sana na akaita watu wakose sms aliyotumiwa kwenye simu yake, wakajitokeza watu kadhaa wakaisoma kila mtu then akamwambia mmoja wao aisome loudly kwa kutumia mic ili hata sie wapita njia tusikie, then sms ilisomeka hivi "MIMI NI MEMBER WA FREEMASON NA NDIE NILIESABABISHA AJALI YA 5 STARS KULE MOROGORO, NO YA KAFARA NI 13, 5 na 3, HIVYO 13 TAYARI IMEKAMILIKA BADO 5 na 3." na yule bwana akaelezea maana ya hizo namba za kafara kuwa ni idadi ya watu wanaotakiwa kutolewa kafara. Mie nasema kama haya ni ya kweli hawa wanaotoa wenzao kafara wajue kuwa maisha hayana gerentii na ni mafupi hivyo nao wana msala wa kwenda kujibu kwa Sir God!
:rip:wapendwa mliofikwa na ajali na Mungu awape afya njema majeruhi wote.