kila wakati tukio kama hili linatokea na hapa naomba tusiilaumu serikali kwa hivi vifo tujilaumu wenyeweBaada ya gari la mafuta kupata ajali wilayani Manyoni eneo la round about ya kwenda Singida na Tabora kupitia Itigi, watu kadhaa ( Idadi kamili haijapatikana bado) wamefariki dunia na wengi kujeruhiwa kufuatia tank la mafuta kulipuka. Vifo na majeruhi vimetokana na wananchi wengi kwenda eneo la tukio kwa ajili ya kusomba mafuta hayo. Chanzo cha mlipuko bado hakijafahamika.
Tunaendelea kufuatulia chanzo cha mlipo na idadi ya majeruhi na waliopoteza maisha.
Ushauri: Watanzania ni lazima tufike mahali tuepuke njia za mkato katika maisha.
bana watu wakome na hii tabia ya kijinga kukimbilia kuchotamafuta magariyanapopata ajali ....mi siwatakii rest in peace wala nini
kila wakati tukio kama hili linatokea na hapa naomba tusiilaumu serikali kwa hivi vifo tujilaumu wenyewe
umasikini na shida tulizo nazo havi-justify matumizi ya vichwa vitupu visivyo na ubongo wenye akili ndani yake.
Kwanini kila wakati watu wawe wanaambiwa jambo lile lile, ni mara ngapi tumeona na kusikia ajali za namna hiyo, kwanini tulazimishane kuachiana majonzi na mizigo ya kijamii kwa kuyakatisha maisha yetu kikatili na kipumbavu namna hiyo???
Hiki tabia inaudhi sana, sisi tumekuwa watu wa aina gani ambao hatujifunzi kitu kutokana na historia na majanga yanayotukumbuka?
Mungu amua mwenyewe pa kuwalaza mimi sina ombi maalum kasoro kwa wale ambao ajali hii haikutokana na kwenda kuchota mafuta...
wananchi hawajui kuwa mafuta yanalipuka??jamani jamani mambo mengine sio laziam hadi serilakli iwepo karibu. kitendo chenyewe ni cha mda ambao hauzidi hata masaa mawili,Mungu katupa uwezo wa kufikiri kwa kial mwanadamuSerikali haiwezi kukwepa lawama katika hili kwani eneo ajali ilipotokea ni eneo ambalo trafic hakaa na kuweka kuzuizi wakati wa duria usiku na kwa taarifa za awali polisi waliokuwepo eneo la tukio wamefariki dunia kutokana na kushindwa kuwazuia wananchi na inasemeka miongoni mwao walikuwa wanauza hayo mafuta.
bana watu wakome na hii tabia ya kijinga kukimbilia kuchotamafuta magariyanapopata ajali ....mi siwatakii rest in peace wala nini