Mlokole aliyeifedhehesha weekend yangu...

FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,792
5,374
Jamani kama mnavyojua haya ma long distance ..Ndio nimetoka kumpokea mzee baada kuwa mbali kwa takribani miezi kadhaa,

Mida ya saa mbili usiku naanda chakula mala simu inaita...naenda kupokea inakatika,

Ikaita tena ..Ile napokea napokelewa na salam ya bwana asifiwe

OOh nikaitikia kwa amani zote amina na wewe bwana asifiwe.

Mara simu ikakatika .

Mpendwa akaendelea sasa kubeep nikipiga hapokei ndipo nilipoamua kumtumia sms nikimwambia asinibeep.

Husband akasema piga.

Mlokole kapokea na sauti inatoka kila kona ya nyumba inasikika usiku

ooh nimefunga kwa muda wa week 3 nimeonyeshwa wewe ndo mke wangu mke mwema...najua hunijui sijui naitwa A.

Naomba upokee maombi yangu.

Nikauliza simu yangu umetoa wapi.

Mlokole kanambia kaipata kwa uwezo wa roho mtakatifu.

Nikamwambia lakini mpendwa mbona nimeolewa nina familia tayari huyo roho mtakatifu aliyekuongoza amekosea

Jaribu kufunga tena.

Mlokole akasema ooh ndoa huwa zinavunjika .

Na yeye yuko tayari kusubiri ndoa yangu ivunjike ili aje kuleta posa.

Ni mtu gani wa kusubiri ndoa ya mwenzie ivunjike eti kaokoka?

Mzee akabakia anaguna tu huku mie nikiendelea kushangaa.
Huyu mlokole mbona ananiletea balaa mwenzenu.:nono:
 
Huyo sio mlokolo anakujua fika.We ungempa kubwa tu.Hayo ndo majini yenyewe.Hata hivyo umeongea nae kistaarabu sana.Mpigie tena halafu mwambie asirudie.

Nilipata shock Mzinga ..
iweje mlokole ategee mzee amefika na mida ya usifu apige simu eti kaoteshwa???
Ila nilimwambia mzee kama atapiga tena naomba uongee nae
 
Ni Lugha tu katumia Huyo ni mtu anakufahamu nawala sio mlokoleUtaratibu wa kupata mke kwa makanisa ya kilokole hauko hivyo alivyofanyaNaomba utambue kwamba huyo sio mliokole kabisa, amevaa koti hilo ili akufikishie ujumbe wake
 
Ni Lugha tu katumia Huyo ni mtu anakufahamu nawala sio mlokoleUtaratibu wa kupata mke kwa makanisa ya kilokole hauko hivyo alivyofanyaNaomba utambue kwamba huyo sio mliokole kabisa, amevaa koti hilo ili akufikishie ujumbe wake
Mgeni kama ni hivi naona hana nia njema kwangu...

Maskini.....pole mwaya!! Kuna watu wanaboa acheni, hilo litakuwa linawafahamu kabisa.......ila basi tu mijitu inajitoaga ufahamu!

Asante Kipipi kweli kuna watu wanaboa ..na atakuwa amejitoa fahamu kupita kiasi..
 
umenikumbusha kisa kimoja.....
Kuna mzee mchungaji....
Mmoja wa waumini wake wa kiume alimfuata....
Akamwambia ameonyeshwa kuwa 'amuoe' binti yake....
I see
yule kaka alitolewa spidi 180.....

Huyo alokupigia simu hana cha ulokole wala nini... Biblia imeandikwa ndoa na iheshimiwe na watu wote......... Je yeye anatumia Bibilia gani?

Ibilisi tu huyo mpotezee...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom