Mliyodhihaki mabehewa mapya TRC ombeni radhi!

Mliyodhihaki mabehewa mapya TRC ombeni radhi!

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,943
Ni ustaarabu kuomba radhi pale tunapokosea, lakini pia ni uungwana kuomba radhi pale tunapokosea wenzetu!

Tuliaminishwa humu kwamba mabehewa yanayopokelewa bandarini Dar es Salaam, ni ya zamani na pia siyo kutoka Korea kama tulivyokuwa tumeahidiwa na serikali ya JMT.

Tulikuwa tunataka kuonyeshwa ubovu mwingine wa JPM na wenye malengo yao!

Sasa tumeona "Uhalisia"ni tofauti na "Uzushi".

Screenshot_20221127-060429_Gallery.jpg
Screenshot_20221127-060436_Gallery.jpg
Screenshot_20221127-060444_Gallery.jpg
Screenshot_20221127-060453_Gallery.jpg
Screenshot_20221127-060503_Gallery.jpg
Screenshot_20221127-060515_Gallery.jpg
Screenshot_20221127-060532_Gallery.jpg
Screenshot_20221127-060542_Gallery.jpg
 
Mleta mada wewe ndio utuombe radhi. Bado huoni tu.

1. Ni kweli hayo ni mabehewa yaliyotumika (old&used), yamepigwa rangi na kuwekwa nakshi (accessories, decorations). Hiyo ni taarifa rasmi ya serikali na mkataba ndivyo ulivyonukuliwa ukitamka.

2. Muonekano wake ni mabewa ya kizamani sana, uliopitwa na wakati. Kuna nchi ukienda utayakuta makumbusho.

3. Muonekano wake ni tofauti kabisa na taswira tuliyohaidiwa hapo awali. Tumeletewa kitu ambacho hatukukiagiza tuletewe!
 
Sasa hayo mabehewa Yana tofauti gani na yale mabasi ya zamani ya UDA!?...au kwa sababu yamepigwa rangi kwa kutumia compressor na kupachikwa viti vya YUTONG ?!...nadiriki kusema hayo mabehewa hayajafikia ata ubora wa zile Steam Trains walizokua wanatumia wakoloni wetu wakati wanatutawala
 
Wajanja sana wameisha piga rangi na kufunga tumifuko tupya tujuwe mupya?

Si zile zile na rangi yake mbaya kama gari za kingi msukuma mwaza to bariadi?

Ila siasa bana, walituonyeshwa ualisia kitakachokuja ili aone reaction, walivyoona kelele, sasa hivi wamezifunga funga tumifuko tupya rangi wamepaka dah
Mbona huleti picha za nje? Tukaziona ni mtumba nyie leteni kwani tumesema hatutazipanda?

Mnapima kina cha maji na njiti ya kiberiti sio? Watanzania hatunaga tabia za kuzila leteni tu. Ila radhi hatuombi, sisi tunajuwa mlichotuhaidi na kilicholetwa.

Ila nyie kama mabasi ya kwa kwini msibani na rangi zile zile.
 
Ni ustaarabu Kuomba Radhi,pale tunapokosea!

Lakini pia ni Uungwana kuomba radhi pale tunapokosea wenzetu!

Tuliaminishwa humu kwamba mabehewa yanayopokelewa Bandarini Dar es Salaam, ni ya zamani na pia sio kutoka Korea kama tulivyokuwa tumahidiwa na serikali ya JMT.
Sasa tumeona "Uhalisia"ni tofauti uzushi
Mkuu Voice, kwanza naunga mkono hoja ni ustaarabu na uugwana mtu kuomba radhi pale unapokosea ama tunapowakosea wenzetu.

Uungwana huu na ustaarabu huu ni kwa wote, hakuna exceptional.

Hoja kuwa mabehewa haya ni mabehewa ya zamani sana, ni mitumba, used, iliyofanyiwa ukarabati kwa kuwekewa vifaa vipya na kufanyiwa nakshi nakshi haina ubishi,

Mzigo utolea Korea sio issue, mitumba hiyo imenunuliwa nchini Ujerumani ikapelekwa kukarabatiwa Korea!.

Tumeelezwa ni mapya na yametengemezwa Korea, na ndani tulionyeshwa yakiwa na dirisha za upande mmoja

ndio maana sio wote tumebeza, wengne tumepongeza ila kuna maswali ya msingi sana tumeuliza Hongera TRL kwa Mabehewa Mapya. SGR ni Reli Mpya ya Kisasa; Je, Mabehewa Haya ni Mapya ya Kisasa? Hakuna Ubaya Kutumia Mitumba, Ila Tuambiwe Ukweli!
Maswali yenyewe ni haya
Wanabodi, tunapaswa kuambiwa tuu ukweli
1. Taarifa ya TRC inasema vichwa vipya na mabehewa mapya, lakini ukweli ni kuwa ni vichwa mitumba na mabehewa mitumba kama ya mwaka '1947'!.

2. Ukiyaangalia kwa ndani, haya mabehewa ni kama yana madirisha only one sided!, hiki ni kuashiria originally haya ni mabehewa ya underground trains na sio ya terestrial train!. Sisi SGR yetu ni terestrial, moja ya faida kubwa kusafiri na treni ni pamoja na kuenjoy kitu kinachoitwa scenery enjoymement, madirisha makubwa both sides abiria kuona nje, hizi behewa za madirisha ya upande mmoja, hebu mfikirie abiria wa Kigoma, seat ya upande usio na dirisha!, kuna tofauti gani na chumba cha jela?.

3. Mkataba ni wa ukarabati na kutiwa nakshi nakshi kwa vichwa na mabehewa mitumba!, na sio kuundwa kwa vichwa na mabehewa mapya!, kwanini Watanzania hatuelezwi ukweli?.
Hakuna ubaya nchi kununua vichwa mitumba na mabehewa mitumba, kitu muhimu ni Watanzania tuelezwe ukweli!.

4. Je, hivyo vichwa viliundwa lini, wapi?, jee originally vimetumika wapi na kwa muda gani kabla sisi hatujauziwa?

5. Mitumba hiyo imenunuliwa kwa bei gani, ikakarabatiwa kwa bei gani, na kusafirishwa kwa gharama gani?

6. Tufanyiwe comparative analysis, kama tungenunua vichwa vipya na mabehewa mapya, tungetumia gharama kiasi gani, compared na kununua vichwa mitumba na mabehewa mitumba, ili tujue tumeokoa fedha kiasi gani kwa kununua mitumba hiyo?

7. Japo gharama za kununua vitu vipya ni juu ila maintance cost ni ndogo, unaweza kununua mitumba kwa bei poa kumbe ni mitumba choka mbaya, hivyo maintenance cost ikawa juu.

8. Sii wengi wanajua kazi ya CAG sio kutoa tuu zile ripoti za hesabu za serikali, CAG ni Mdhibiti na Mkaguzi, ufhibiti unafanywa kabla ya manunuzi, je, kulifanyika tathmini yoyote rail worthness report ya vichwa na mabehewa hayo mitumba kabla hayajanunuliwa?. Then CAG atufanyie value for money audit, msikute mitumba hiyo tumepewa bure, huku watu wakipiga kubwa tunauziwa kwa bei ya mapya!.

9

. Ukiingia mkataba wa manunuzi, kwa matengenezo, mzigo ukanunuliwa, delivery ndio ikachelewa, huwezi kuvunja mkataba huo ukabaki salama, hivyo kesi ikifunguliwa, Tanzania tunashindwa hata kabla kesi haijaanza!.

10. Tulivunja mkataba wa Dowans, tulishitakiwa, tukashindwa, tukadaiwa tukasema hatulipi!, watu wakajiapisha "over my dead body", hatulipi!.
ukweli ni kuwa tumelipa kwa siri, Watanzania hatukuambiwa!.

11. Tulipo vunja mkataba wa Dowans, Zitto akashauri tuitaifishe mitambo ile, Wabunge wetu wakagoma kuwa Tanzania hatununui mitambo chakavu, mitambo mitumba!

12 Mitambo ile ikanunuliwa na Simbion, tukaingia nao mkataba ule ule wa Dowans, watu wale wale walio ikataa dowams, ndio hao hao danced to the tune na Hilary Clinton kuzindua Simbion kwa mkataba ule ule tuliovunja!, kwa gharama zile zile!, na capacity charge ile ile!, na tukawalipa!.

13. JPM alipoingia tukavunja mkataba wa Simbion, tukashitakiwa, tukashindwa, JPM akagoma kulipa!, ila baada tuu ya JPM kuitwa kule alipoitwa huku nyuma, sisi sio tuu tumelipa!, bali pia tumeinunua ile mitambo ya Simbion kwa bei ya ajabu!, sasa mitambo ile tuliosema ni chakavu, mtumba, na serikali yetu hatununui, mivitu chakavu, sasa ndio tumeinunua!, sasa mitambo ile ya Simbion ni mitambo yetu, ni mali yetu! na malipo yote yaliisha fanyika chap chap fasta fasta!, bila bajeti yake kuombwa popote!, bila Bunge letu kuijadili, bila CAG kuidhinisha malipo hayo!, na haya yote yamefanyika bila iWatanzania kuambiwa!.

14. NB. Unapohoji vitu kama hivi, huchelewi kunyooshewa vidole vya kukosa uzalendo au kutokuwa na nia njema!, no!, wala sijasema kilichofanyika ni wrong!, no!, ninachosema hapa ni sisi
Watanzania wa sasa ni waelewa, tuwe tuu tunaambiwa ukweli,

15. Kwa vile mambo kama haya kwenye manunuzi makubwa yaliwahi kutokea kule nyuma kwenye ununuzi wa Rada mtumba toka BAE, watu wakaweka cha juu kikubwa tuu, tukalipa fasta!, Mama Mzalendo wa kizungu, Linda Chalkel akabaini, akatupigania tukarudishiwa chenji ya Rada!.

16. Ununuzi wa ndege ya rais Gulf Steeam bei ikapaishwa zaidibya mara tatu!, John Cheyo akaonyesha bei ya kiwandaji watu wakatia pamba masikioni tukalipa fasta!.

17. Kuna vifaa vya kijeshi chakavu tumeuziwa hapa!, tangu vimenunuliwa havijawahi kutumika mpaka leo!. Hivi naomba nisivizungumzie wala msiniulizie!, maana hata sisi waandishi wa habari haturuhusiwi kuzungumzia mambo ya jeshi na usalama wa taifa, ila fedha zilizotumika sio fedha za jeshi au za usalama wa taifa, ni fedha za Watanzania, kuzungumzia vifaa vya jeshi, tuliuziwa nini mitumba ni vifaa vya nini na viko wapi, hii ni no!, hatuzungumzi, lakini tulilipia fedha kiasi gani, ni haki ya Watanzania kujua!.

18. Tukanunua Boti mtumba ya MV Bagamoyo, ikafanya safari moja tuu mahali pa 30 min, ilitumia masaa 3!, Hii pia sasa ni kufaa cha kijeshi!, isizungumzwe!, ila fedha zake ni fedha za Watanzania!.

19. Hivyo kweli hivi vichwa na mabehewa haya, ni bora tukaelezana ukweli tangia mwanzo!.

20. Namalizia kwa msisitizo, hakuna ubaya kutumia vitu used!, tena vingine ni vizuri, imara, bora, madhubuti kuliko hata vipya!, na Watanzania walio wengi, kutokana na low purchasing power due to umasikini uliotopea, wengi wetu affordability yetu ni mitumba kuanzia magari, nguo hadi mitambo, hivyo tumezoea, tunachohitaji ni kuambiwa ukweli tuu!,
tutaelewa tuu kuliko...

Wasalaam.
Paskali.
Tuambiwe tuu ukweli, Watanzania hatuna tatizo kabisa na kutumia mitumba, tumezoea!. Watu Bongo wanavaa nguo za mitumba na wengine hata naniliu za mitumba!, itakuwa mabehewa!. Sisi wengine hatulalamiki bali tunataka transparency tuu!.

P
 
Ni ustaarabu Kuomba Radhi,pale tunapokosea!

Lakini pia ni Uungwana kuomba radhi pale tunapokosea wenzetu!

Tuliaminishwa humu kwamba mabehewa yanayopokelewa Bandarini Dar es Salaam, ni ya zamani na pia sio kutoka Korea kama tulivyokuwa tumahidiwa na serikali ya JMT.

Tulikuwa tunataka kuonyeshwa ubovu mwingine wa JPM na wenye malengo yao!

Sasa tumeona "Uhalisia"ni tofauti na "Uzushi"View attachment 2428630View attachment 2428631View attachment 2428632View attachment 2428633View attachment 2428634View attachment 2428635View attachment 2428636View attachment 2428637
CC. Kigwabgwala,Pasco na wengineo
 
Wenzetu haya nimesikia 2023 wanataka wabadilishe walete mengine na washaanza baadhi ya mabehewa kuyapeleka chuma chakavu sisi ndio tunaagiza na hayapo kwenye kiwango hiki...
 

Attachments

  • Screenshot_20221127-071623_Google.jpg
    Screenshot_20221127-071623_Google.jpg
    200.5 KB · Views: 7
  • Screenshot_20221127-071723_Google.jpg
    Screenshot_20221127-071723_Google.jpg
    214.9 KB · Views: 8
  • Screenshot_20221127-071735_Google.jpg
    Screenshot_20221127-071735_Google.jpg
    220 KB · Views: 6
  • Screenshot_20221127-071631_Google.jpg
    Screenshot_20221127-071631_Google.jpg
    190.5 KB · Views: 7
  • Screenshot_20221127-071638_Google.jpg
    Screenshot_20221127-071638_Google.jpg
    238.9 KB · Views: 9
Back
Top Bottom