Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 673
- 1,313
Habari wakuu, hii ni taarifa na dukuduku kwa wakati mmoja. Ipo hivi, abiria wa TRC waliokuwa wakisafiri na SGR ya leo jioni kuelekea Dodoma wamelazimika kukaa station (kituoni) hapo kwa saa zaidi ya 8 wakisubiri train baada ya treni hiyo iliyotakiwa kuondoka jijini majira ya 12:55 jioni kuchelewa na kupelekea safari hiyo kuanza saa 5 usiku, ikumbukwe abiri wengi wao walifika kituoni hapo majira ya saa 10 hadi 11 jioni kwa ajili ya kuwahi train hiyo kama ilivyoelekezwa katika tiket zao.
Changamoto hii inatoa mwanga juu ya umuhimu wa TRC kupitia upya sera na taratibu zao, hasa kuhusu haki za abiria na huduma bora za usafiri. Hivi sasa, TRC ina sera kali ya kutorudisha fedha au kuruhusu mabadiliko ya ratiba kwa abiria wanaochelewa kwa dakika chache. Ingawa suala hili linaweza kuwa na mantiki kwa upande mmoja, ni muhimu TRC izingatie hali maalum za abiria (circumstances iliyomfanya achelewe au kuhairisha safari)
Binafsi swali ninalojiuliza ni : TRC inafanya nini iwapo treni zao zitachelewa (kama ilivyotokea leo)? Na Je, kuna fidia yoyote inayotolewa kwa abiria wanaokumbana na hali hii ? Swali hilo nilijiuliza kwa kuzingatia kwamba haki ya abiria ni kipengele muhimu cha huduma bora za usafiri, na abiria wanastahili kufidiwa wanapokumbana na ucheleweshaji usio wa lazima.
Nina ushahidi wa jambo hili kwani nami ni moja ya watu niliokumbana na adha kadhaa za SGR. Nitaeleza, Ni hivi, nlinunua tiketi ya SGR kwa safari ya leo saa 12:00 asubuhi, lakini nilipofika kituoni saa 11:50 asubuhi, nilizuiwa kuingia kwenye treni. Sikulaumu TRC kwa sababu nilichelewa, ingawa kwa dakika chache na kwasababu zilizo njee ya uwezo wangu. Nilipoomba nirudishiwe angalau nusu ya gharama ya tiketi, walikataa kabisa. Nilijaribu pia kuomba kuongeza fedha ili kubadilishiwa ratiba na kupewa nafasi kwenye treni inayofuata (kama inavyofanyikaga kwenye ndege), lakini walikataa na kunitaka nikanunue tiketi mpya.
Nilinunua tiketi nyingine kwa safari ya saa 12:55 jioni, na kufika kituoni saa 10:00 jioni kuhakikisha round hii nazingatia ratiba. Hata hivyo, TRC walitoa taarifa ya kuomba radhi kwamba treni itachelewa na itaondoka saa 2:00 usiku. Ilipofika saa 2:00, walitangaza tena kuwa treni hiyo itaishia Morogoro badala ya Dodoma, na sisi tulioelekea Dodoma tulitakiwa kusubiri utaratibu mpya.
Hali hii ni ya kusikitisha na inahitaji TRC kujitathmini na kujipanga upya. Huduma za usafiri zinapaswa kuzingatia maslahi ya abiria wote, na sio kutoa adhabu zisizo na mantiki kwa wateja wanaochelewa kwa sababu mbalimbali. Kwa upande mwingine, TRC inapaswa kuwajibika pale inapochelewesha huduma zao, na kutoa fidia stahiki kwa abiria.
Kwa haya machache, ni wazi TRC wanatakiwa kuboresha taratibu zao ili kuhakikisha haki na huduma bora kwa wasafiri wote.

Ni hayo tu wakuu✍🏽