Mliowahi kuacha kazi mlifanyaje? Nataka kuacha

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,051
12,949
Mimi ni mtumishi wa umma,nina miaka 4 kazini ila nataka kuacha kazi.

Nataka kuacha ili niendeshe biashara zangu ndogo ndogo, lengo langu ni kua mfanya biashara na sio mfanyakazi. Najua mshahara haujawahi kumtajirisha mtu popote duniani ukiacha deals kama za kina masamaki.

Nimekua nafanya vibiashara vidogo vidogo ila naona havikui wala kuleta hela ya maana zaidi ya vipesa vya kubadili mboga na vocha.

Najua huwezi kufanya kazi huku unafanya biashara hiyo biashara ikakua, mabwana wawili kwa wakati mmoja haitawezekana.

Nataka kuacha kazi ila nakosa balls za kunisukuma kuacha ila natamani sana kuacha, nipeni mbinu mliachaje. Usilete ushauri hapa wa kutokuacha kazi.
 
Planning, courage and Passion

thamini unachokifanya usiite biashara yako 'vibiashara'
 
mimi niliacha mwaka jana June.. sababu ilikuwa ni lazima niache kwa target niliyojiwekea..

sema nilijipanga na wife alinisupport na kunikumbusha muda umefika.. ilikuwa lazima mmoja aondoke kazini akasimamie kikampuni chetu..

nina almost a year mtaani sina hata hamu ya kurudi na nashukuru mambo yanaenda
 
Mimi ni mtumishi wa umma,nina miaka 4 kazini ila nataka kuacha kazi.

Nataka kuacha ili niendeshe biashara zangu ndogo ndogo, lengo langu ni kua mfanya biashara na sio mfanyakazi. Najua mshahara haujawahi kumtajirisha mtu popote duniani ukiacha deals kama za kina masamaki.

Nimekua nafanya vibiashara vidogo vidogo ila naona havikui wala kuleta hela ya maana zaidi ya vipesa vya kubadili mboga na vocha.

Najua huwezi kufanya kazi huku unafanya biashara hiyo biashara ikakua, mabwana wawili kwa wakati mmoja haitawezekana.

Nataka kuacha kazi ila nakosa balls za kunisukuma kuacha ila natamani sana kuacha, nipeni mbinu mliachaje. Usilete ushauri hapa wa kutokuacha kazi.

Mkuu uko sahihi kamisa mimi mwenyewe niko mbion kuquit job nifanye yangu...sababu hakuna mtu aliyewahi kuwa tajiri kwa mshahari otherwise madili ya hapa na pale.

Ila mi ningekushauri before quit ,hivyo hivyo vibiashara vidogo make sure vinakulete faida ambayo itakutosheleza kuishi na ikiwezekena akiba kidogo bila kudisturb capital... hapo sasa ndo unaweza kuacha kabisa kabisa.

soma kitabu kinaitwa poor dad richdad, before quiting you job, cash flow quadrant vyote vya robert kiyosaki. Vitakusaidia sana kushape ideal mimi nimevisoma vimenisaidi sana.

hivyo vitabu vyote viko youtube unaweza kusikiliza pia, mimi kwangu naona vitabu muhimu sana kusoma vitakusaidia sana mkuuu hasa kubadili fikra na kujenga confidence.
 
Mimi ni mtumishi wa umma,nina miaka 4 kazini ila nataka kuacha kazi.

Nataka kuacha ili niendeshe biashara zangu ndogo ndogo, lengo langu ni kua mfanya biashara na sio mfanyakazi. Najua mshahara haujawahi kumtajirisha mtu popote duniani ukiacha deals kama za kina masamaki.

Nimekua nafanya vibiashara vidogo vidogo ila naona havikui wala kuleta hela ya maana zaidi ya vipesa vya kubadili mboga na vocha.

Najua huwezi kufanya kazi huku unafanya biashara hiyo biashara ikakua, mabwana wawili kwa wakati mmoja haitawezekana.

Nataka kuacha kazi ila nakosa balls za kunisukuma kuacha ila natamani sana kuacha, nipeni mbinu mliachaje. Usilete ushauri hapa wa kutokuacha kazi.
Taja umri wako, kazi unayoifanya, muda uliokuwa kazini na umejiandaa kufanya nini baada ya kucha kazi.
 
Mambo yafuatayo hayatakiwi kuomba ushauri kwa mtu amua wewe wenyewe binafsi:-
1. Kujinyonga
2. Kuacha kazi
3. Kuacha mke au mme
4. Kumuuwa mtoto au kumloga apate kichaa ili upate utajiri.
5. Kulala kwenye leli
6. Kunywa dawa aina ya dayazon chupa nzima
 
Ulishawahi kupewa barua yyte ya onyo? Ukiandika barua ya kuacha kazi ni sawa ila utamlipa mwajili wako mshahara wa mwezi mmoja , angalia mkataba wako wa ajira unasemaje, na jibu utalipata humo,
 
Kwanza ww ni mwalimu bila shaka, ukijiamini tu mbona rahisi ,sema ukiomba ushauri sana kuna baadhi ya watu watakutisha tisha, na asikudanganye mtu ukiwa makini utafanya maendeleo makubwa tu na kupoga hatua, else usubirie mafao yako wakati wa kustaafu pengine yakaja kukuua kwa ugonjwa wa moyo kama ilivomtokea hayati mzee Mangunga R.I.P
Sifanyi kazi serikali kuu.
 
Mimi ni mtumishi wa umma,nina miaka 4 kazini ila nataka kuacha kazi.

Nataka kuacha ili niendeshe biashara zangu ndogo ndogo, lengo langu ni kua mfanya biashara na sio mfanyakazi. Najua mshahara haujawahi kumtajirisha mtu popote duniani ukiacha deals kama za kina masamaki.

Nimekua nafanya vibiashara vidogo vidogo ila naona havikui wala kuleta hela ya maana zaidi ya vipesa vya kubadili mboga na vocha.

Najua huwezi kufanya kazi huku unafanya biashara hiyo biashara ikakua, mabwana wawili kwa wakati mmoja haitawezekana.

Nataka kuacha kazi ila nakosa balls za kunisukuma kuacha ila natamani sana kuacha, nipeni mbinu mliachaje. Usilete ushauri hapa wa kutokuacha kazi.
ni vyema sana kuacha kazi bcoz utakuwa tajiri kama bill gate.Pia acha na dini kabisa
 
Mimi ni mtumishi wa umma,nina miaka 4 kazini ila nataka kuacha kazi.

Nataka kuacha ili niendeshe biashara zangu ndogo ndogo, lengo langu ni kua mfanya biashara na sio mfanyakazi. Najua mshahara haujawahi kumtajirisha mtu popote duniani ukiacha deals kama za kina masamaki.

Nimekua nafanya vibiashara vidogo vidogo ila naona havikui wala kuleta hela ya maana zaidi ya vipesa vya kubadili mboga na vocha.

Najua huwezi kufanya kazi huku unafanya biashara hiyo biashara ikakua, mabwana wawili kwa wakati mmoja haitawezekana.

Nataka kuacha kazi ila nakosa balls za kunisukuma kuacha ila natamani sana kuacha, nipeni mbinu mliachaje. Usilete ushauri hapa wa kutokuacha kazi.

Omba likizo bila malipo japo hii haikupi presha ya kupambana kisawasawa mtaani maana inatakiwa uwe katika position ambayo Failure is not an option.
 
Hakuna ugumu ktk hilo. Mambo mawili unatakiwa uyafahamu:

(A) Mkataba wowote wa ajira ambao unazingatia taratibu za kisheria, ni lazima uwe na kipengele kinachoelezea namna ya kuvunja huo mkataba kwa pande zote mbili. "Termination of contract". So angalia kwanza mkataba wako wa ajira unasemaje kuhusu kuvunja mkataba. Hapo ndo pa kuanzia.

(B) Kwa mujibu wa Sheria ya mkataba, upande wowote (mwajiri au mwajiriwa) ukitaka kufanya termination of contract by short notice (summary termination), unatakiwa utoe (uulipe ule upande mwngne) mshahara wako wa mwezi mmoja. Kwamba: unamuandikia mwajiri wako notice ya kuacha kazi kwa ghafula (short notice), kisha unampa mshahara wako wa mwezi mmoja. Mchezo kwisha.

Hivyo ndo navyofahamu mimi kwa uelewa wangu mdogo. Hopefully magwiji wa Sheria humu watakupa muongozo zaidi.

-Kaveli-
 
Hivyo havihitajiki hapa na havina matumizi hapa,kazi umri na wapi nafanya hayahusiki.
MKUU si kweli kama havihitajiki,
- Umri- kuna umri ukifikia huna aja ya kuacha kazi kwamaana soon utastaafu.
- muda aliofanya kazi: kuna muda ukifikisha kazini, ukaamua kuacha kazi unalipwa kila mwezi na mashirika ya mafao, kama amebakiza muda mchache kuufikia muda huo anaweza subiri.
- Kazi anayofanya ( Sijauliza anapofanya). kuna kazi nyingine unaweza kufanya mambo yako mengine huku bado ukiwa kazini bila kuharibu kazi kabisa.
- Umejiandaa kufanya nini baada ya kucha kazi: utakuwa ni mwendawazimu kama unataka kuacha kazi kama hujajipanga
 
Sio rahisi kuacha kazi kivile na kuanza biashara bila kuyumba... Jiandae na Changamoto utakazokutana nazo
 
Pole sana Mkuu kwa tatizo lako, jaribu kufuata ushauri ulio mzuri na usioathiri maisha yako.
 
Back
Top Bottom