Je, ana watoto/mtoto ? maana umri wa kupata watoto ni miaka 35, vinginevyo, ataongeza idadi ya watoto Yatima. Kama yuko 40 hana mtoto, ina maana atapata mtoto akiwa ni miaka 45, huyo mtoto akikisha 23 wakati anaingia chuo, tayari umri wa mama umeenda. Jaribuni kuwa mnawashauri hao marafiki zenu, poda zinawadanya sana.
Huyo atakuwa sio mke bali chombo cha starehe, kumbuka sheria za dini zinatofautiana kulingana na imani ya mhusika/wahusika, baadhi ya imani zinaelekeza kuwa mke ni msaidizi wa mwanaume. Sasa kama kama imani inasema kuwa mke ni msaidizi, iweje tena umfanyie kila kitu badala ya kusaidiana kufanya hizo kazi. Kama Baba anatafuta mahitaji ya familia, basi Mama awe anasimamia matumizi yake. Halafu mwanaume unaanzaje kwenda kuchambua na kunua bamia sokoni ukiwa umemwacha mkeo nyumbani, mimi huwa tunaenda wote maana huwa tunafanya manunuzi ya mwezi, na yeye ndo anatangulia mimi nyuma wakati mwingine nabaki kwenye usafiri, akirudi ananikuta sio kumbana mwanamke kila sehemu hata asikonyezwe.