Mliooa mlipata wapi wake zenu?

Inawezekana tunakushauri tuu hapa ila kumbe huna mpango wala effort zozote za kumtafuta huyo mke.
Umefanya juhudi gani kutafuta mke
Umejiwekea lengo gani na kwa muda gani kumpata huyo mke
Na je vigezo gani umeweka kumpata huyo mke
Na je unatafuta mke wa kuoa mwaka huu au mwakani au baada ya miaka mingapi

vigezo vipo mkuu, ktk muda kiukweli ipo wazi, akipata afaae, maandaliz yanaanza
 
Kwanza jiulize ulishajitambua ni mwanamke wa aina gani unamtaka,
Coz kuna baadhi ya wavulana japo wanakuwa wanona ni wanaume ukimuliza aina ya mke anayetaka hizo sifa anazotaja mpaka aibu kwa uankuta kabase kwenye sifa za nje ambazo ni ngumu kwa mtu mmoja kuwa nazo zote labda mpaka kutoa oda kwa mungu amtengenezee,so kumpata inakuwa ishu,
Nakushauri tuliza akili,mke sio sura wala umbo,mshirikishe mungu ktk kumtafuta utampata tu coz kila mtu kaumbiwa mtu wake,
Jiweke km mwanaume alietayari kuwa baba wa familia sio ujiweke kivulana utaishia kupata visichana mcharuko,
Hata ukimpata anayefanania kuwa mke uwe na subira na mvumilivu kwan wengi huwa hawakurupuki kukukubali ni lzm auone userious wako,pia angalia namna unavowaaprochi,ulimi wako ndio silaha pekee hata km utakuwa na mwonekano wa aina gani!
Epuka kutumie pesa km ushawishi wakati wa kujieleza ni sumu kali kwa wadada walio makin,japo wengi hawaamin hili.

Dah! Sijui nikupe nini mtoto wee mweeeee umeongea point mpaka nimesisimka.
 
Ikifika siku Mungu atatuma malaika uitaona anakuonyesha huyu ndo mke wako.

Lakini wewe hutamuona malaika.


Songíto;3208307 said:
kaka shukuru unapata kugundua kuwa wenzio unaokuwa nao sio waaminifu!! kuna watu hawakugundua hayo mapema, au waligundua ila wakalazimisha kuingia kwenye ndoa, wakazaa na kuanza maisha kwenye ndoa zao, saizi wanaonja shubiri (chungu) kwa maisha magumu ya ndoa... naomba nikutie moyo mkuu kuwa "mke bora hutoka kwa bwana (muumba)". Ukiona hivyo ujue bado muumba hajakutengea wako!!!

ILA...ILA.... kama nawe umekuwa ukiwatendea wenziwako ndivyo sivyo, inawezekana muumba anafanya malipizi kwa mabaya hayo uliyotenda maana "Muosha Huoshwa", kama ndivyo, tubu mrudie muumba na omba misamaha kwa wabaya wako na halafu mpigie magoti muumba wako na omba mke bora, atakupa nakuambia...

Mshirikishe Mungu katika hatua hii ya kumtafuta mke wa kuoa maana mke sio nyanya ambazo unaweza kwenda soko lolote na kuchagua nyanya kwa muuzaji yyote unayekutana nae
Mke ni mtu ambaye ni muhimu sana kwako na mtu ambaye ije mvua liwepo jua usiku na mchana sometime mtakuwa wote na mtashare mengi so unatakiwa kuwa makini sana kwenye uchaguzi wako
Sio kweli kwamba wengi ni mcharuko ila may be wewe mwenyewe hujatulia na ndo maana kila unayempata anafanana na wewe
Jipe muda na tulia kwenye safari hii ya kumtafuta mwenza

Kilaza,

Ndugu yangu mke huwa hatafutwi, yani inatokea tu una date mtu hadi unaona mmh hapa sasa sina ujanja.

Mwenzako mimi nilikuwa nimemaliza chuo nipo kitaa sina kazi full kujirusha tuu na washikaji naanza starehe Alhamisi namaliza Jumapili na sitoki club had nisikie swalaaa swalaa lol...kipindi hiko sina hata mpango wa kuoa mtu akisema swala la ndoa namuona mshamba and thats when i met MRS Right.

Nilikuwa na mshikaji tunatoka usiku one akapigiwa simu na cousin yake binti aliyekuwa anasoma chuo Dsm akiomba twende tuka wa pick hostel coz nae alikuwa na shosti wake wangependa kwenda out. Mshikaji alichomoa,lakini nikamsihi tukawachukue after all itakuwa poa kuwa na company. That night nili dance sana na cousin yake mshikaji huku jicho langu lipo kwa shosti wake na cousin. Maana alikuwa anang'aa hadi balaa.Offcoz mshikaji alikuwa ana dance na shosti mtu ambaye ndio my waifu wangu kwa sasa. After hapo tuka date kwa takriban miaka 4 alikuwa akitaja swala la ndoa ananitibua lakini finally nikaoa huyo huyo.

inawezekana anakupa wa kufanana na wewe, badilika uone.

Leo hii ukiniuliza nilimpataje mama Ngina hata sikumbuki...................... haya mambo huwa yanatokea Automatikale.

Ila kweli mkuu wanawake wengi nimcharuko lakini siyo wote wewe jitaidi kutafuta kanisani kwako na pia umuombe mungu
Nimesoma hizi comments hakika nimeona busara zenu, i hope kwa wale wote wanaosaka ndoa watanufaika na mashauri haya. Kila la kheri waJF
 
Nimefarijika sana na ushauri wenu.Thanks guys ngoja nami nijipange upya,possibly nilikuwa nakosea.
 
Dah! Sijui nikupe nini mtoto wee mweeeee umeongea point mpaka nimesisimka.

Sidhani kama unanyanyuka from nowhere unamtaka tuu mwanamke awe mkeo bila kuhakikisha kuwa anafikia kiwango kile unachotaka
Inawezekana umeweka elimu, kazi, sura, ucha Mungu wake na ni mwanamke wa aina gani unataka
Sana sana huwa hayo hayazingatiwi sana ila sidhani utanyanyuka tuu na kumvamia mwanamke yeyote utakayomuona na akakuvutia na ukamfanya mke
Mkuu nenda taratibu na kama nilivyokuambia Mke sio nyanya sokoni wala sio nguo dukani ila mke ni mtu wa muhimu sana kwako na ambaye utautumia muda mrefu sana wa maisha yako kuwa nae
Usiende papara wala usivamie kila mwanamke utakayemuona na ukadhania ni mke
Wanawake wako wengi lila mke ni mmoja tuu sasa issue inakuwa hapo kumpata huyo mmoja
Muombe Mungu na utulie katika kufanya chaguo lako
Achana na papara maana utaishia kupata mcharuko
 
Tatizo wanaume micharuko pia mnataka waliotulia. Tuliotulia wenyewe tupo wachache. Hebu oeni micharuko yenu hyo hyo.
 
Tatizo wanaume micharuko pia mnataka waliotulia. Tuliotulia wenyewe tupo wachache. Hebu oeni micharuko yenu hyo hyo.

Husninyo kweli hututakii mema kuoa mcharuko aise noma
Mwanaume mcharuko anaweza kutulia bana
 
Wewe una gundu.

Jichunguze :tabia/fikra/hobbies/muelekeo wa maisha/unavyojionyesha au onekana, chunguza vigezo unavyotumia kutafuta/chagua mpenzi, chunguza matarajio yako kama yanaendana na eneo unalowinda n.k

Ningekua mwanaume na nimeoa ningekwambia pa kwenda

Dear!
Kwa nyongeza katika ulochangia ni kwamba mtoa mada inabidi aache tabia zake mbaya.

Ukimu-aproach mwanamke kimzaa mtaishia kwenye mzaa. Ukiwa serious katika kumweleza nia yako naye atakuwa serious tu! Wanawake wana akili sana kuliko sisi wanaume; wanatusoma, wanatujadili - sisi wanaume hatuna mda wa kuwajadili - ndo maana wanatu-handle.

Najibu swali la mtoa mada....
Mlioooa mlipata wapi wake zenu?

Wa kwangu nilimpata siku alipokuja dukani kwa kaka yangu kufanya shoping; nikamjengea ukaribu - hadi akawa rafiki wa familia yetu na mwisho nikamtamkia kuwa nataka kuwa naye maishani - hakusita. Inataka muda kumteka mawazo mtoto wa kike. Vijana wa siku hizi wanakurupuka kuomba tendo la ndoa, wanachokana mapema na kutimuana. Pengine ni malezi mabaya; kwetu sisi tuliolelewa katika mazingira kiroho tunakuwa na woga sana - si kwamba tunawaogopa wanawake; la hasha - tunamwogopa Mungu.
 
Hivi kuna aina ngapi za wanawake?Halafu kumbe kuna vipezo vya kumpata mwanamke!Inawezekana ndo maana wanawake wanashindwa kuolewa!Watu wanatoa vigezo kama vile anaweka oda ya gari kwenye kiwanda!Wanawake kazi mnayo!
 
Back
Top Bottom