Mliooa mlipata wapi wake zenu?

Ila kweli mkuu wanawake wengi nimcharuko lakini siyo wote wewe jitaidi kutafuta kanisani kwako na pia umuombe mungu

kumuomba mungu ndio, ila wa kanisani nao siku hizi vimeo tu, haswa kwaya ya vijana ndo mastar wao kuwang'oa
 
kumuomba mungu ndio, ila wa kanisani nao siku hizi vimeo tu, haswa kwaya ya vijana ndo mastar wao kuwang'oa
Kwani nani kakuambia ukamtafute wa kanisani
Umeambiwa muombe Mungu akupe mke mwema na akupe mke unayemtaka wewe kwa vigezo vyako na sio kwenda kutafuta mwanakwaya wa kanisani
 
nyie ndo walee mnaotafuta wanawake wenye sijui wezere kubwa,ooo awe na sura nzuri,pua ndefu,mguu wa bia,macho ya kulegea,mrefu,awe na pozi.......badala ya kutafuta wenye sifa za kumcha mungu,,ndo mana matokeo yake mnaishia kupata micharuko

asa unadhani ntampenda vipi bila kumtamani kwanza? mwenyewe mbaya, mama watoto nae akiwa kapinda si adhabu kwa watoto
 
nielemishe mkuu

Inawezekana tunakushauri tuu hapa ila kumbe huna mpango wala effort zozote za kumtafuta huyo mke.
Umefanya juhudi gani kutafuta mke
Umejiwekea lengo gani na kwa muda gani kumpata huyo mke
Na je vigezo gani umeweka kumpata huyo mke
Na je unatafuta mke wa kuoa mwaka huu au mwakani au baada ya miaka mingapi
 
Huna nia ya kuowa. Wanawake wote waliopo duniani!!!!!! Mbona mimi wananifwata wenyewe niwaowe$$$
 
Sa unaguna kwanini sitoa point wapi kuna kosa, au kusikia malaika ndo imekuwa ajabu...wewe unaelewa nini mana ya malaika? malaika sio lazima umuone au mungu unadhnai utamuona? kama unadhani utamuona mungu ujuwe unaota.

Point yangu ni huwezi kuoa bila ya mungu kupenda....na FYI malaika kila binadamu anatembea nao lakini kwa kuwa wengine mko zero hamjui hayo.
 
kwanza jiulize ulishajitambua ni mwanamke wa aina gani unamtaka,coz kuna baadhi ya wavulana japo wanakuwa wanona ni wanaume ukimuliza aina ya mke anayetaka hizo sifa anazotaja mpaka aibu kwa uankuta kabase kwenye sifa za nje ambazo ni ngumu kwa mtu mmoja kuwa nazo zote labda mpaka kutoa oda kwa mungu amtengenezee,so kumpata inakuwa ishu,nakushauri tuliza akili,mke sio sura wala umbo,mshirikishe mungu ktk kumtafuta utampata tu coz kila mtu kaumbiwa mtu wake,jiweke km mwanaume alietayari kuwa baba wa familia sio ujiweke kivulana utaishia kupata visichana mcharuko,hata ukimpata anayefanania kuwa mke uwe na subira na mvumilivu kwan wengi huwa hawakurupuki kukukubali ni lzm auone userious wako,pia angalia namna unavowaaprochi,ulimi wako ndio silaha pekee hata km utakuwa na mwonekano wa aina gani!epuka kutumie pesa km ushawishi wakati wa kujieleza ni sumu kali kwa wadada walio makin,japo wengi hawaamin hili.
ahsante mdada!!
 
Mimi nilimpatia kwenye computer kozi alikuwa mwanafunzi wangu, kwanza nilimpenda kwa muonekano wake, tabia yake na nilipogundua kabila na dini yake vitaendana na matakwa yangu na kuwafahamu ndugu zake na tabia zao bila hata yeye kufahamu kwamba ninafanya uchunguzi niliamua kujaribu kuanzisha uhusiano, na kweli nilipomuomba kutoka nae hakukataa. Katika maongezi yetu swali la kwanza aliloniuliza ni kama mimi ni mume wa mtu au la, nilipomjibu kwamba mi sijaoa nilimuona ametabasamu na kuwa na amani sana. Tulianza urafiki wetu bila kujificha kabisa na ndugu zetu walijua toka miezi miwili ya mwanzo. Kusema ukweli kabla ya hapo nilikuwa kicheche nakwenda disko na marafiki zangu mpaka saa nane za usiku na huko kila mtu anachukua changudoa, tulikuwa na tabia ya kuchukua machangu tu, tulikuwa hatutaki kabisa kuwa na GF tuliona ni usumbufu usiokuwa na maana, unamchukua changu kesho hamjuani tena. Ila nilipompata mke wangu mpaka marafiki ilibidi nitengane nao kabisa kwenye mambo ya starehe, mpaka ilifikia wakawa wanasema nimelishwa limbwata. Ndugu yangu kitu cha muhimu ni kufanya uchunguzi na kujua tabia, elimu, dini, mila (kabila) kama vitaendana na matakwa yako na umuombe Mungu akusaidie umpate Mke mwema. Usiweke mbele tamaa za mwili na kufanya mapenzi ovyo, usimwambie kwamba unataka kumuoa kabla ya kufanya maamuzi. Tabia yako inaweza kukufanya kazi ya kumpata mke ikawa ngumu au rahisi sana jichunguze.

hapo kwenye kabila mi sijaweka kigezo.. inawezekana imekua too large eeh? embu nipe makabila mazuri basi nipunguze uwanja.. ila shukrani kwa ushauri, nmeupenda na story yako ni nzuri, ila tu usije rudia asili badae ukamletea magonjwa mwana wa watu
 
Wapo wengi sana tena wa kumwaga.....sema tu wewe ndo umeishiwa ujanja...Omba tu wataalamu wakusaidi ku-recharge!!

Uko tayari nikugawie mmoja wa wale nilionao??

Nataka kudispose mmoja ili nitafute mupya!!

Babu DC!!

kaazii kwelikweli
 
Back
Top Bottom