Mliooa mlipata wapi wake zenu?

nyie ndo walee mnaotafuta wanawake wenye sijui wezere kubwa,ooo awe na sura nzuri,pua ndefu,mguu wa bia,macho ya kulegea,mrefu,awe na pozi.......badala ya kutafuta wenye sifa za kumcha mungu,,ndo mana matokeo yake mnaishia kupata micharuko
 
Hongereni wana jf kwenye thread hii mmenishangaza maana wengi wenu mmeongea point....haleluuuuuuyaaaaa
 
Wewe utakua ndio wale wakaka ambao hutoka na ladies, akidhania kua siku akitaka kuoa ataselect toka kwenye shelve..... Ukisahau kabisa kua wadada wa kulala nao ni wengi wa kila sampuli na kila kona; ila wale ambao ni worth it kujenga nao mahusiano ni adimu. Ukisahau kabisa kujiandaa kua walau two years before hujaoa jiandae kuanza kutafta a partner ambae utaona atafaa kua mke. Saizi unataka kuoa ndio unakuta kumbe sio lelemama wala sio mchezo, wadada wa kuoa hawapo.... wapo almost absent.... na bahati mbaya saana upo pressured by the fact kua sasa it is time. Nikwambie kweli kabisa kazi unayo, hivo brace your self.....

USHAURI.

Unataka mke wa kuoa yatakiwa umakini sababu ndoa bana is for life.... inatakiwa utulize akili na huyo mdogo wako pia umtulize na kikubwa I am genuienly telling you usimsahau kumshirikisha mwenyezi Mungu. Punguza kidogo vigezo, vya the type of woman you want,... Naamini kabisa una vigezo na kama wachukua list ya vigezo vyako kama njia ya kumpata unae ona ana qualify utakesha. Enways nakutakia kila la kheri katika kumpata....

asante sana.. na nimeipenda
 
Mimi nilimpatia kwenye computer kozi alikuwa mwanafunzi wangu, kwanza nilimpenda kwa muonekano wake, tabia yake na nilipogundua kabila na dini yake vitaendana na matakwa yangu na kuwafahamu ndugu zake na tabia zao bila hata yeye kufahamu kwamba ninafanya uchunguzi niliamua kujaribu kuanzisha uhusiano, na kweli nilipomuomba kutoka nae hakukataa. Katika maongezi yetu swali la kwanza aliloniuliza ni kama mimi ni mume wa mtu au la, nilipomjibu kwamba mi sijaoa nilimuona ametabasamu na kuwa na amani sana. Tulianza urafiki wetu bila kujificha kabisa na ndugu zetu walijua toka miezi miwili ya mwanzo. Kusema ukweli kabla ya hapo nilikuwa kicheche nakwenda disko na marafiki zangu mpaka saa nane za usiku na huko kila mtu anachukua changudoa, tulikuwa na tabia ya kuchukua machangu tu, tulikuwa hatutaki kabisa kuwa na GF tuliona ni usumbufu usiokuwa na maana, unamchukua changu kesho hamjuani tena. Ila nilipompata mke wangu mpaka marafiki ilibidi nitengane nao kabisa kwenye mambo ya starehe, mpaka ilifikia wakawa wanasema nimelishwa limbwata. Ndugu yangu kitu cha muhimu ni kufanya uchunguzi na kujua tabia, elimu, dini, mila (kabila) kama vitaendana na matakwa yako na umuombe Mungu akusaidie umpate Mke mwema. Usiweke mbele tamaa za mwili na kufanya mapenzi ovyo, usimwambie kwamba unataka kumuoa kabla ya kufanya maamuzi. Tabia yako inaweza kukufanya kazi ya kumpata mke ikawa ngumu au rahisi sana jichunguze.
 
kaka shukuru unapata kugundua kuwa wenzio unaokuwa nao sio waaminifu!! kuna watu hawakugundua hayo mapema, au waligundua ila wakalazimisha kuingia kwenye ndoa, wakazaa na kuanza maisha kwenye ndoa zao, saizi wanaonja shubiri (chungu) kwa maisha magumu ya ndoa... naomba nikutie moyo mkuu kuwa "mke bora hutoka kwa bwana (muumba)". Ukiona hivyo ujue bado muumba hajakutengea wako!!!

ILA...ILA.... kama nawe umekuwa ukiwatendea wenziwako ndivyo sivyo, inawezekana muumba anafanya malipizi kwa mabaya hayo uliyotenda maana "Muosha Huoshwa", kama ndivyo, tubu mrudie muumba na omba misamaha kwa wabaya wako na halafu mpigie magoti muumba wako na omba mke bora, atakupa nakuambia...

nikishafikiria shubiri ya ndoa ndo nakatika hamu ya ndoa kabisa....
mi sinaga tabia mbaya..
 
micharuko kila sehemu, ata hakuna pa kutokea!! sijui mi ndo nna gundu.. au ndo hali ilivyo ila lile neno ambalo lipo kwenye kiapo na linasisitizwa sana 'uvumilivu' linachukua nafasi yake!!
aise wake walishaisha

Wapo wengi sana tena wa kumwaga.....sema tu wewe ndo umeishiwa ujanja...Omba tu wataalamu wakusaidi ku-recharge!!

Uko tayari nikugawie mmoja wa wale nilionao??

Nataka kudispose mmoja ili nitafute mupya!!

Babu DC!!
 
Leo hii ukiniuliza nilimpataje mama Ngina hata sikumbuki...................... haya mambo huwa yanatokea Automatikale.

ngoja nisubiri zamu yangu nami ata kama inachelewa, teh teh teh
 
Pole sana, wanawake kwa kiasi kikubwa wanachagua nani waolewe nao. Bado hujachaguliwa. Pili, ndoa ni zao la mahusiano halinunuliwa sokoni. Ukitafuta kama bidhaa sio rahisi kupata. Jipende utapedwa tu. Kila la kheri
 
micharuko kila sehemu, ata hakuna pa kutokea!! sijui mi ndo nna gundu.. au ndo hali ilivyo ila lile neno ambalo lipo kwenye kiapo na linasisitizwa sana 'uvumilivu' linachukua nafasi yake!!
aise wake walishaisha

fumba macho na masikio ziba

 
Kama una kwama waambie wazazi waku-postie. Ukizingatia ndoa za zamani za kupangiwa zilidumu zaidi

zamani wake walikua wengi ndo maana, siku iz wameisha!! wazazi ndo kwanza wanakwambia usituletee wa suruali za kubana, wao hata hawatii mguu kukutafutia wa sketi ya marinda
 
Back
Top Bottom