Mlioko kwenye ndoa na watoto wenu wa nje, Mnalitatuaje hili swala?? Msaada jamani naombeni....

Record Man

Member
May 25, 2023
77
343
Kuna Kaka yangu mmoja kutoka kwa Baba mkubwa alizaa na mwanamke mmoja miaka kama 12 hivi iliyopita. Ila hawakufanikiwa kuwa pamoja baada ya mtoto kufikisha miaka 4 mama yake alimleta kwa Baba yake na kumpa na kumwambia yeye anaolewa kapata Bwana mpya.

Basi kaka yangu huyu akamchukua mtoto wake. Na yeye akaoa baadae.

Sasa ishu ni hii sasa yafika miaka 8 dogo hajawahi kumuona mama yake tangu anamika 4. Kwa sasa anamika 12 yupo darasa la 6. Kuna kipindi dogo alikuwa anahitaji kuwa karibu na mama yake. Maana viashiria alikuwa anaonyesha anamuitaji mama yake.

Ila jamaa yangu akimpigia mama yake simu wanaishia kuongea tuu na mtoto. Wazazi wake wakamwambia ongea na mzazi mwenzio awe anamtembelea hata 1 wiki moja, ila mwezie wala hana time kabisa.

Sasa msaada jamani hii ishu kama ni wewe ilikukuta au ndugu au rafiki uliisolve vipi ishu kama hii. Msaada jamani.
 
Tunaisi labda mume wake kule anaweza kuwa ndo kikwazo.
Majibu mnayo sijui mnataka tushauri nini?
Hapo baba mtoto amuhoji kiujanja mama wa mtoto anuani ya makazi yake kisha mtoto akifikisha miaka 12 ampe nauli akamsalimie mama yake siku 5 tu arudi kwa baba yake.

Mama analinda ndoa yake, kwake ndoa muhimu kuliko mtoto wake damu yake. Analinda maokoto yake pia.
 
wamama wengine rohombaya tuu.
kunajirani aliachiwa kichanga Cha miezi minne.
bidada alimfuata mshkaji kazini akamwambia nishikie mtoto maramoja nakuja akaondoka hakurudi tena.jamaa aliteseka sana kumtunza yule kichanga aisee jinsi alivyokuwa analía.
 
Hapo baba mtoto amuhoji kiujanja mama wa mtoto anuani ya makazi yake kisha mtoto akifikisha miaka 12 ampe nauli akamsalimie mama yake siku 5 tu arudi kwa baba yake.
Sasa mkuu kama mume wake amuitaji mtoto hata kufika nyumbani kwake siku akifika si itakuwa shida.

Kuna mtu mmoja tupo nae office moja yeye wapo mapacha yeye na dada yake .
Mama yao alizaa kabla ya ndoa na baba yao ila mzee aliwachukua na kuishi nao na kulelewa na mama wa kufikia ila baada ya kufikisha miaka 17 mzee wao alifaliki.

Mtu aliyebaki ni mama yao ambae aliolewa na ME mwingine.
Jamaa alinisimulia yule mume wa mama yao hata kufika tuu home kwake alikuwa hataki , yani hata kuja na kuondoka tuu yani ni shida.

Baada ya wao kupata ndoa zao hata watoto kumtembelea bibi yao kwao alikuwa hatiki.

Sasa tunahofu anaweza jamaa nae akawa hivyo.
 
Kuna Kaka yangu mmoja kutoka kwa Baba mkubwa alizaa na mwanamke mmoja miaka kama 12 hivi iliyopita. Ila hawakufanikiwa kuwa pamoja baada ya mtoto kufikisha miaka 4 mama yake alimleta kwa Baba yake na kumpa na kumwambia yeye anaolewa kapata Bwana mpya.

Basi kaka yangu huyu akamchukua mtoto wake. Na yeye akaoa baadae.

Sasa ishu ni hii sasa yafika miaka 8 dogo hajawahi kumuona mama yake tangu anamika 4. Kwa sasa anamika 12 yupo darasa la 6. Kuna kipindi dogo alikuwa anahitaji kuwa karibu na mama yake. Maana viashiria alikuwa anaonyesha anamuitaji mama yake.

Ila jamaa yangu akimpigia mama yake simu wanaishia kuongea tuu na mtoto. Wazazi wake wakamwambia ongea na mzazi mwenzio awe anamtembelea hata 1 wiki moja, ila mwezie wala hana time kabisa.

Sasa msaada jamani hii ishu kama ni wewe ilikukuta au ndugu au rafiki uliisolve vipi ishu kama hii. Msaada jamani.
Bora uzima....kuonana ni majaaliwa
 
Back
Top Bottom