Mkwe mtarajiwa!!!

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,953
2,116
Jamani, mmoja wa mabinti / shangazi zangu kaja kumtambulisha mchumba wake kwangu uli nitoe baraka (unajua Shangazi ni mtu muhimu sana ktk suala la kuhalalisha uchumba) ili baadaye ukoo ujulishwe. Ile kumuona tu moyo wangu umemkataa, na nimewatimua, kama mume matarajiwa ndiye huyo, afadhali mwanangu asiolewe. Sababu: Mchumba ana muonekano wa kibabe, anaweza niulia binti yangu bure. Ebu nanyi mujionnee halafu minieleze kama hatua niliyochukua ni nzuri ili kunusuru future ya binti yangu.


Mbombo gafu.jpg
 

Kiranga

Platinum Member
Jan 29, 2009
60,871
75,237
Muonekano unadanganya.

Unaweza kumkataa Shwaziniga wetu hivi hivi. Mfikirie kama mtu mwenye discipline kubwa sana. Si kila mtu anaweza kufanya mazoezi na kuwa fit hivyo.

Kuna kaka yetu mmoja alikuwa anapiga chuma vibaya sana, halafu hata si mtu wa fujo wala ubabe. Kinadada walimuita "Gentle Giant".

Usimhukumu mtu kwa jinsi anavyoonekana. Mpe nafasi umjue.

Besides, ndo kashapendwa.Si ustaarabu kukataa mtu aliyependwa kwa sababu ziso msingi.

Unaweza kusababisha matatizo makubwa. Binti kakuheshimu kukupa intro, na wewe muheshimu kwamba anaweza kufanya uamuzi mzuri. Ma binti wa siku hizi ungeweza kusikia kaolewa kwenye redio mbao tu.

Zaidi ya misuli kitu gani kinakufanya ufikiri atakuulia binti? Pengine ndo mzuri kuweza kumtetea binti asichezewe shere na wahuni.
 

BHULULU

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
4,943
1,871
Binti ana bahati sana maana hapo ulinzi ni full,kwa kifupi naona yuko kwenye mikono salama
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
90,720
104,952
Umeongea naye na kuweza kumjua zaidi au umehitimisha tu kuwa hafai kwa kuangalia muonekano wake wa nje?
 

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,953
2,116
Binti ana bahati sana maana hapo ulinzi ni full,kwa kifupi naona yuko kwenye mikono salama

Asante kwa ushauri, lakini hiyo sura changanya na hiyo misuli na mavazi, moyo wangu umebutuka!!!
 

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,794
24,514
Unahukumu kitabu kwa cover yake? Kama amekuja ukweni akiwa amevaa hivyo basi ni ushamba wa bintiyo tu. Ungempokea na kumkaribisha upate kumfahamu. Na uongee na bintiyo, kuwa mwenza wake anam-define na yeye. Kama ambavyo yeye hawezi kwenda ukweni na leghings na spagheti top, basi amsaidie mwenzie ajue kuvaa accordingly. Watu wa hivi sio wakorofi kwa sababu wana nguvu nyingi ambazo hawataki kuzipoteza bure.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,916
287,621
Hahahahaaa lol! mama mdogo kumbe unaogopa misuli eeh! lol!...binti ataamua kutoroka na jamaa yake kwa raha zao na nyie akina shangazi mtabaki mnang'aa macho.
 

prianka

JF-Expert Member
Aug 29, 2012
684
168
usiangalie umbo na sura ya mtu angalia tabia je inakidhi kua na binti yako sasa kwa mara ya kwanza 2 kumuona umeisha mtoa baluuu shangazi wewe utakua una gubuu la uzeeni
 

Nyati

JF-Expert Member
Mar 6, 2009
2,427
1,699
Jamani, mmoja wa mabinti / shangazi zangu kaja kumtambulisha mchumba wake kwangu uli nitoe baraka (unajua Shangazi ni mtu muhimu sana ktk suala la kuhalalisha uchumba) ili baadaye ukoo ujulishwe. Ile kumuona tu moyo wangu umemkataa, na nimewatimua, kama mume matarajiwa ndiye huyo, afadhali mwanangu asiolewe. Sababu: Mchumba ana muonekano wa kibabe, anaweza niulia binti yangu bure. Ebu nanyi mujionnee halafu minieleze kama hatua niliyochukua ni nzuri ili kunusuru future ya binti yangu." First impression is the best impression" Umefanya vizuri kumtimua kwani kama yeye alijua kuwa anakuja kutambuliswa kwa nini alivaa hivyo?!!!!!!!!!!. Naungana nawe katika hili.

Mimi wakati naenda kutambulishwa kwa mara ya kwanza wife alipanga nivae nini na vitu vingine vingi in advance
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,142
9,466
" First impression is the best impression" Umefanya vizuri kumtimua kwani kama yeye alijua kuwa anakuja kutambuliswa kwa nini alivaa hivyo?!!!!!!!!!!. Naungana nawe katika hili.

Mimi wakati naenda kutambulishwa kwa mara ya kwanza wife alipanga nivae nini na vitu vingine vingi in advance[/QUOTE

Impression...........impression........hivi kuna harusi inafungwa bila nguo smart???? Mbona baada ya hapo ni matusi magumi na kashfa ndani ya baadhi ya ndoa.......impression ya mwanzo ilikuwaje kwa ndoa zenye dhahma na zilizovunjika?????

So kama mkeo asingekuchagulia wewe hukuwa na plan???? .......ukiitwa mbulullah for that hukuwa unajua hata jinsi ya kuvaa ukienda ukweni na yeye mkeo ndo kakutoa tunduni utakuwa mkali????

Je kama na yeye hayo mavazi alichaguliwa na mkewe mtarajiwa????

Shangazi alichemka kumtimua mara ya kwanza........angeweza kuwaambia that day hajisikii vizuri hivyo wakutane sehemu nyingine on other day then angeona zaidi


Vipi kama angekuja well dressed (subjectively) on that day halafu kumbe huko mitaani yeye hutembea hovyo na ni mtukanaji mzuri.......mshinda bar ....kulala club na mengineyo......???????
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom