Naomba ushauri nimewakosea sana wanaoenda kuwa wakwe zangu kutokana na mkanganyiko wa familia yangu/Sikutokea siku ya Send off

roselina john

JF-Expert Member
Aug 17, 2017
758
942
Jamani mambo zenu, Niko katika wakati mgumu

Mimi ni binti wa miaka 29 kwa sasa, nimempata mwanaume ambaye tulipanga mengi sana hadi kupanga jinsi ya kufunga ndoa,

Mwaka fulani niliingia kwenye mahusiano na kijana mmoja toka Mbeya, ila kwa sasa anaishi Afrika ya Kusini kwa shughuli zake ,
Tulikubaliana kuanza kutambulishana kwao, na kwetu

Nakumbuka alinilipia nauli ya ndege nikaenda kwao kutambulishwa nikamshukuru Mungu kwamba nimepata mme sasa,

Tumeendelea na utaratibu na mshenga akatumwa kwetu kusema, baada ya kuondoka nikamweleza mama kuwa kijana sawa ananipenda ila hapendi jambo fulan ambalo kwa ukweli sitalisema hapa, mama akasema kama ndo hivo sitak habari zako za kuolewa,

Ikabidi mchakato uendelee kawaida, wakaleta kishika uchumba mama akawa hataki kushiriki hata kidogo, anasusa, sasa shangazi yangu akaniambia kwamba kwakuwa huna baba naomba ili suala tuwashirikishe baba wadogo na wajomba tuendelee na nchakato,

Baada ya muda tukapanga wataletaje mahari na siku ya send off tukaipanga,

Sasa kabla ya send off siku moja kabla tukapata habari kupitia kwa mjomba kwamba Mwanaume anayeenda kunioa kumbe ana mke mi naenda kuwa mke wa pili, taarifa hii ikawachanganya wote hata wajomba wakasema ngoja wajiweke pembeni, maandalizi ya send off yakavurugika wakati huo wakwe wakiwa njiani kuhudhuria sherehe hiyo , walikodi Costa na magari kadhaa kutoka mbeya hadi Ngara,

Wakanikimbia ndugu zangu wote nami nikachanganyikiwa kwa hasira sikutokea kwenye send off na maandalizi ikawa hasara, wakapiga simu nikazima nilikuwa na hasira sana,

Baadaye nikawasha simu nikakuta mama mkwe mtarajiwa amenitumia meseji kwamba "Sikutegemea kama ungetufanyia haya, sisi tunajiandaa kesho tunarudi lakini baki na amani"

Niliumia sana Akaendelea kunitumia meseji za machungu nikijua naye anajua kuwa Mwanae ana mke na mama huyu tumeongea kila siku niliumia,

Sasa yule mchumba wangu akawa ananitafta sipokei nikamwambia sina Muda mchafu wa kuolewa na wewe, hapo sikumwambia kwanini nimebadili mawazo,

Sasa nakumbuka siku kadhaa baadae naitwa nyumbani kwamba kuna kikao,

Kumbe kuna taarifa kwamba yule kijana hakuwa ameoa ila alichumbia sehemu akalipa mahari ila kumbe hakuoa,

Habari zilisononesha sana

Nikaenda kwa askofu mmoja akanishauri

1.Ama tuombe radhi kwao kuendelea na mchakato

2.Ama tuwape kishika uchumba chao maana mahari alikuwa bado angetoa siku ya send off asubuhi yake,

Naomba ushauri wenu plz

Nimeikosea Sana familia ile, pia hasira baada ya kupungua natamani niolewe naye japo nashindwa naanzaje

-----------------------------------

Nimeamua kuwaambia ukoo wangu, Kuanzia Mama sina Baba R.I.P
Mashangazi, Baba Mdogo na wajomba nia yangu ya dhati kuiomba msamaha familia ya ambaye alikuwa mchumba wangu,

Naenda kuomba msamaha nikitegemea maswali magumu,

Naenda Kuomba msamaha nikijua maumivu na uchungu hata hasara waliyopata kutoka Mbeya hadi Ngara,

Hatua ya Kwanza
Nimeamua niangalie upepo ndani ya familia yangu, idadi ya wanaonisapot,

Niangalie mtazamo wao juu ya kwanini nasukumwa kuomba msamaha,

Tatu naangalia dhamira yangu na msukumo wa moyo wa dhati,

Nne Nimeamua kuwashirikisha ndugu na kuwaambia sitaenda moja kwa moja kwa wakwe ila ntaenda kwa mshenga

Tutaenda timu ya watu 7 watu wazima sita na mimi nikiwa wa saba, katika timu hiyo mama aneendelea kugoma kutoshiriki, Nimepata shangazi mama mdogo na baba mkubwa,na wengine

Tutaelekea kwa mshenga kuomba radhi, na kueleza sababu za kutokuwapo kwenye send off alafu tumuombe atuombee msamaha,

Baada ya wao kujua tunaomba msamaha kup kwa mshenga

Nimeandaa kishika uchumba walicholipa na nimeandaa wazee 5 na wanisindikize Mbeya kutoka Ngara kwenda kuomba msamaha na pia kabla ya kufika kwenye familia ya wakwe, tutapitia kwenye parokia iliyokaribu kumuona kiongozi wa dini atupe mwongozo na kumuomba atupe ushirikiano kufika kule, pia tutaomba aambatane na wazee wa heshima wa Kanisa, hii nitaifanya tu hata wasipotoa jibu pitia kwa Mshenga

Nikifika nitakuwa na maombi mawili

1.Kuomba kusamehewa na kurudisha kishika uchumba chao

Ama

2.Kuomba kusamehewa na kuendelea na mchakato wa harusi kama watakua bado hawajapata mtu.

Naombenii mawazo yenu mengine pia

asante
 
Pole sana na ninajua huyo mjomba wako unamlaumu sana na baba zako walikuwa sawa maana walitaka kumuenzi baba yako ambaye kwa maelezo yako hayupo hivyo walitaka kumaliza majukumu ya kaka yao..
 
Kuelekea ndoa huwa kuna maneno mengi ya uchonganishi toka kwa wenye roho mbaya hivyo huwa ni vyema kuwa makini kuliko kukurupuka, kikubwa waeleze ukweli wa jambo kama wanayo nia hakitoharibika kitu.
 
kuelekea ndoa hua kuna maneno mengi ya uchonganishi toka kwa wenye roho mbaya hivo hua ni vyema kua makini kuliko kukurupuka, kikubwa waeleze ukweli wa jambo kama wanayo nia hakitoharibika kitu.
Alitakiwa awaambie kabla ya siku ya send-off ili maandalizi yasimame. Familia iliyostaarabika ingefanya hivyo na kusingekuwa na lawama. Hata kama atawaomba msamaha wakamsamehe bado hawatamsahau.
 
Yaelekea we si Mke Bora kabisa
1.Kwanini hukuwaeleza wasitishe safari?
2.Kuna jambo unasema mama yako hakuliafiki ni lipi?
3.Tatu unahisi hata ukisamehewa wazee wa ukoo ule watakuchukuliaje pindi wakipishana na wewe?
4.Una uhakika huyo bwana harusi hajapata mwingine wa kuendelea na mpango mwingine?

Tujibu
 
Kwanza pole sana kwa yaliyokukuta!!
Kabla sijasema lolote naomba kusema neno kwamba "kamwe usikurupuke kufanya uamuzi kabla hujafanya uchunguzi"

Lakini pili naomba kukuuliza, je nikweli unampenda huyo kijana..? Kama ni ndio basi omba msamaha kwake kadhalika kwa familia yake!! Mueleze jinsi ambavyo hukukamilika kama walivyo binadamu wengine!

Pia, kama humpenda kwa dhati kiasi kilichopelekea kufanya uamuzi wa kikatili namna ile hata kwa wakwe zako, still yakubidi uiombe hiyo familia msamaha wa dhati na uendelee na maisha yako mengine kwa amani!
 
Yaelekea we si Mke Bora kabisa
1.Kwanini hukuwaeleza waaitishe safari?
2.Kuna jambo unasema mama yako hakuliafiki ni lipi?
3.Tatu unahisi hata ukisamehewa wazee wa ukoo ule watakuchukuliaje pindi wakipishana na we we?
4.Una uhakika huyo bwana harusi hajapata mwingine wa kuendelea na mpango mwingine?

Tujibu
Send off ilikuwa tarehe 10 taarifa zinatoka tarehe 8 wakati wameanza safari tarehe 7 Kutoka mbeya, nilimtext mvulana kuwa wasitishe wakati huo wameshafika Kahama,

Suala ambalo mama na mimi tulitofautiana ni baada ya kumweleza mchumba wangu kwamba nina mtoto akasema mi ndo naoa kwakuwa nimekukubali ukiwa na mtoto hakuna shida ila akaomba mtoto atamlea na kumsomesha na ameshamlipia ada ya primary one ya mwaka mzima niwe mkweli, ila akanisihi nisiwajulishe kwao kama mi nina mtoto, hapo ndio mama akakazania kwamba lazima wajue, nikamsihi mama kwamba anayenioa kashamkubali mtoto na anamhudumia ila kwao wataleta mapingamizi nikiwaambia muda huu, hivyo kasema tutawaambia mbeleni, mziki ukaanzia hapo mama akajitoa
 
Kwanza pole sana kwa yaliyokukuta!!
Kabla sijasema lolote naomba kusema neno kwamba "kamwe usikurupuke kufanya uamuzi kabla hujafanya uchunguzi"

Lakini pili naomba kukuuliza, je nikweli unampenda huyo kijana..? Kama ni ndio basi omba msamaha kwake kadhalika kwa familia yake!! Mueleze jinsi ambavyo hukukamilika kama walivyo binadamu wengine!

Pia, kama humpenda kwa dhati kiasi kilichopelekea kufanya uamuzi wa kikatili namna ile hata kwa wakwe zako, still yakubidi uiombe hiyo familia msamaha wa dhati na uendelee na maisha yako mengine kwa amani!
Kijana yule namjua kiundani ni mpole mno ana Busara sana, najua ataweza kunisamehe ila sijajua namuanzaje na naianzaje familia yake
 
Send off ilikuwa tarehe 10 taarifa zinatoka tarehe 8 wakati wameanza safari tarehe 7 kutoka mbeya , nilimtext mvulana kuwa wasitishe wakati huo wameshafika kahama,

Suala ambalo mama na mimi tulitofautiana ni baada ya kumweleza mchumba wangu kwamba Nina mtoto akasema mi ndo naoa kwakua nimekukubali ukiwa na mtoto hakuna shida ila akaomba mtoto atamlea na kumsomesha na ameshamlipia ada ya primary one ya mwaka mzima niwe mkweli, ila akanisihi nisiwajulishe kwao kama mi nina mtoto, hapo ndo mama akakazania kwamba lazima wajue, nikansihi mama kwamba anayenioa kashamkubali mtoto na anamhudumia ila kwao wataleta mapingamizi nikiwaambia muda huu, hivyo kasema tutawaambia mbeleni, mziki ukaanzia hapo mama akajitoa
Wewe unaonekana una makando kando mengi sana.Shika taimu yako muache kijana atafute mwingine sababu hata hukutaka kumuliza mwemzio juu ya hiyo ya yeye kuwa tayari ana mke na kupata ukweli wa wa hizo tuhuma,ona sasa unataka uuwashe moto mwingine kwa ndugu zake pindi wakijua wewe uliolewa ukiwa single mother.Hawajambo hapo Murugwanza lakini?
 
Mimi ningekuwa huyo mchumba wako, ningekusamehe. Ila nisingekuoa tena huna sifa za kuwa mke Bora. Huna adabu, huna busara, huna hekima, unapenda umbea na majungu, huna uvumilivu.

Hata ukiolewa kwa tabia uliyoweza kuionesha mbele ya ndugu zake, hasa wazazi, hata ndoani mkiwa wenyewe unaweza kuirudia kwa kupenda na kuyaamini maneno ya uzushi na umbea.
 
Pole sana kwa yaliyokukuta ila;
  • Familia yenu ipo so disorganized kiasi kwamba mmepokea rumours tu, rumours tu zikawafanya wote as a family kuahirisha jambo kubwa la namna hiyo.
  • Wewe hufai kuwa mke wa mshkaji kwa sababu baada ya mjomba kusema hivyo, kwa nini usimtafute mchumba na kuuliza mwenyewe hayo uliyosikia na ukweli wake.

Mwisho, ingekuwa mimi ningekusamehe kiroho safi lakini nisingekuoa, you're unfit to be a wife.
 
Back
Top Bottom