Mimi kwa mtazamo wangu naona kama mnalihukumu hilo vodacom kwa yasiyowahusu...utasusia kila kampuni ambapo watanzaniaa wengi amabao wana connection na hao mafisadi wana hisa humo...taja makampuni makubwa yenye wana hisa wa tz uone nini kitafuata...je ukikuta pesa alizowekeza huko alikopa au kuna wana hisa wadogo wadogo weengi sana humo na wamekopa si kulihukumu kampuni na wengineoo ???ni mtazamo wangu piaa...nina haki ya kujadili na kuwa upande mmoja lunyungu
Hili linawezekana huko Pemba... Sijui Bara kama wana ubavu huo...😀 😀Mnaonaje kama tutasusia kutumia noti zenye signature ya Ballali kwa kuwa ni fisadi... how does that sound..
Mnaonaje kama tutasusia kutumia noti zenye signature ya Ballali kwa kuwa ni fisadi... how does that sound..
Lunyungu has a point. Sisi wananchi tunachoweza kufanya ni kuanza kumark mali za mafisadi na kuwakimbia. Honestly kama RA et al... wapo Voda tuanzishe campaign za kugomea bidhaa zao..sasa what else can we do? Mkuu Lunyungu tuko na wewe. Hata kama waajiriwa ni ndugu zetu..ni katika mapenzi mema na nchi yetu, watatusamehe. Jamaa analipwa millions every day---kodi zetu....na bado tunampelekea nyingine..why?
Hata Gandhi alisema...hiyo ni silent protest! Hakuna la soko huria wala nini..mali yoyote ya fisadi, ni kuigomea..infact wenzetu huko majuu hii trick ya kugomea vitu imefanikiwa sana! Lets try it..na isiishie kwenye Vodacom tuu..ni kote mafisadi wanakohusika...
Vodacom situmii line yao tena....
Lunyungu,
Hii ni move ya kijasiri sana na natumaini ya kwamba kama Watanzania tutafikia kiwango hicho cha Uzalendo basi hawa Mafisadi watachomoka tu. Kwa vyovyote vile.
Lakini nina mawili matatu ambayo nataka fumbuliwa zaidi maana naamini kila ambalo tunafanya tunatakiwa kujua matunda yake:
1. Je katika Wamiliki Hisa wa hapo Vodacom wote ni Mafisadi ama ni huyu Rostam peke yake?
2. Huyu Fisadi ni Mfanyabiashara, sasa je tunatakiwa susia Bidhaa zake zote ama ni hii ya Mawasiliano tu?
3. Kutokana na sisi kutumia huduma za VODACOM kuna Watanzania wengi wamefanikiwa kupata ajira na kupunguza makali ya Maisha. Wao wamewekwa katika Kundi la Mafisadi kwa kuwa Wanamtumikia Fisadi ama? Na je Huoni kwamba tutakapoamua kufanya Hivyo tutakuwa tumewahukumu na wao kwa kiwango kikubwa?
Naomba tufikiri kwa upana zaidi!
Nasema kampuni ama bidhaa yeote yenye mkono wa Fisadi kama tunaweza kuiepuka tufanye hivyo kwa nguvu zetu zote .
Vp kuhusu ushabiki wa mpira ligi kuu inadhaminiwa na VODACOM, mashindano ya MA-MISS wa kibongo nayo wanadhaminiwa na VODACOM sasa sie tunaweza kujitoa wote na je tulio wapenzi wa mpira tutawashawishi vp kina Simba,Yanga,Prison,Mtibwa na wengineo wakatae udhamini wa VODACOM kwa sababu ya huyu RA wakati ndio wanawaweka hapa mjini.
Inabidi tuanzie kwenye mzizi mkubwa kuukata ndipo tufuate matawi, ukikata matawi baada ya muda mengine yatachanuwa cha msingi ni kuanza kukata huu mzizi mkubwa unaofanya mti unakuwa na kushamiri kila kukicha na unatoa kivuli kizuri.
Kenya waligomea hata vyakula kwenye supermarket when they felt kwamba pesa zao zilienda kwa Kibaki na zikatumika kuwanyima haki yao .Tanzania Rostam Aziz kila kukicha ana wezi mpya lakini iko kimya na support anapewa .Sisis tuna lalamika lakini bado tunatumia huduma za simu za Vodacoma ambazo yeye ni mmoja wa share holders .Kama tuna uchungu kweli na huyu ambaye analindwa na CCM na serikali yake , tuhamie sote kwenye tigo ama zantel ama Celtel .Hii itakuwa njia nyingine ya sisi kuonyesha kwamba tumechoka kuibiwa na kuzidi kukamuliwa kila mara .Mimi nimesha hama na huhu unakaribia mwaka tangia nimejua kwamba Rostam anatumaliza bado na vodacom yumo .Mie natumia Zantel sasa na Celtel .Je wewe unangoja nini ?Tuambiane tuachana nao hawa .Wanatuona wajinga katika maamuzi yao je waendelee kutuona wajinga hata katika pesa zetu wenyewe za kutumia katika simu ?
Mnaonaje kama tutasusia kutumia noti zenye signature ya Ballali kwa kuwa ni fisadi... how does that sound..
Mkuu Masatu naona hapo umeteleza kidogo!
Tukisusia noti zenye saini ya Balali maana yake hatutauza wala kununua na hivyo hatutakula! Sasa tukiwasusia Vodacom hatutawasiliana?
Rudi ndani ya mada, tafadhali
Wewe Lunyungu sasa unaishiwa, yaani watu wasitumie vodacom au bidhaa za Rostam Azizi kisha watatumia nini? Rostam amekukosea nini mpaka ukatae kutumia bidhaa zake?
Kenya waligomea hata vyakula kwenye supermarket when they felt kwamba pesa zao zilienda kwa Kibaki na zikatumika kuwanyima haki yao .Tanzania Rostam Aziz kila kukicha ana wezi mpya lakini iko kimya na support anapewa .Sisis tuna lalamika lakini bado tunatumia huduma za simu za Vodacoma ambazo yeye ni mmoja wa share holders .Kama tuna uchungu kweli na huyu ambaye analindwa na CCM na serikali yake , tuhamie sote kwenye tigo ama zantel ama Celtel .Hii itakuwa njia nyingine ya sisi kuonyesha kwamba tumechoka kuibiwa na kuzidi kukamuliwa kila mara .Mimi nimesha hama na huhu unakaribia mwaka tangia nimejua kwamba Rostam anatumaliza bado na vodacom yumo .Mie natumia Zantel sasa na Celtel .Je wewe unangoja nini ?Tuambiane tuachana nao hawa .Wanatuona wajinga katika maamuzi yao je waendelee kutuona wajinga hata katika pesa zetu wenyewe za kutumia katika simu ?
No no no hapo bado hauja tushawishi tuache kutumia mtandao wa Voda kisa ni wa RA tena kwa hiyo mada yako isiyokuwa na ushahidi wowote. Please kama una ushahidi wa uhakika uweke hapa kila mtu aone. La sivyo hadi house girl wangu naenda kumnunulia line ya VODA. siwezi kushawishika kwa hayo maneno yako tu.