Mkuu wa Wilaya ya Liwale afia Guest House!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,555
113,739
Wanabodi,

Mkuu wa wilaya ya Liwale, Paul Chiwile amefariki usiku wa kuamkia leo katika nyumba ya kulala wageni ya Vission aliyofikia mjini Lindi.
Mkuu huyo wa wilaya alikuwa Lindi kuhudhuria mkutano uliokuwa unatarajiwa kuanza leo wa utekelezaji wa mpango wa kitaifa wa magonjwa yasiyokuwa na kipaumbele.

Kwa mujibu wa Radio One mwili wa marehemu upo katika hospitali ya mkoa ya Sokoine ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.
Imefahamika kwamba atazikwa kwao Kibaha.

RIP DC Paul Chiwile!.
 
Sasa kwani kufia Guest House ni ishu? Kama alikuwa ugenini angelala wapi? Ninyi ndio mnachafua chama chetu
 
Wanabodi,

Hii nimetumiwa kwa SMS kutoa mkoa, fulani, kuwa kuna mkuu wa wilaya fulani, kafia Gest House fulani Vision iliyopo mkoa fulani. Hivi ninavyo post sasa, RC wa mkoa huo, akiandamama na RPC, RCO, OCD, na DCO NA kikundi cha askari na makachero, wameizunguka hoteli hiyo ili kuvunja mlango kuthibitisha tukio hilo!.

Jina la Mkoa, na Mkuu wa wilaya hiyo nimelihifadhi ili kusubiri uthibitisho.

Lengo la kuposti mapema ni kuhakikisha wewe kama mwana jf, "be the first to know".

Pasco.


tunashukuru
weka japo jina la mkoa ili tufuatilie
 
Mkuu wa wilaya ya Liwale, Mkoani Lindi amefariki usiku wa kuamkia leo, ktk hoteli aliyofikia
akijiandaa kuhudhuria mkutano wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele.

Source radio One na ITV
 
"mkoa, fulani, kuwa kuna mkuu wa wilaya fulani, kafia Gest House fulani Vision iliyopo mkoa fulani."

Nakuheshimu sana kama mwana taaluma, mkuu. Maana ya sentensi hii na lengo lake ni nini? Unanikumbusha enzi za vitendawili...chemsha bongo. hii taarifa inatakiwa kuwa informative, na maadam umeweka hapa, haiwezi kuwa siri wewe taja kila kitu bwana ili mradi ni kweli.
 
Habari zilizothibitshwa na Radio one break news Mkuu wa wilaya ya Newala Paul amefariki dunia baada ya kukutwa amekufa kwenye nyumba ya wageni ya mission iliopo lindi alipokwenda kwenye semina.
 
Back
Top Bottom