Mkuu wa Wilaya ya Kahama anatishia usalama wa waandishi wa habari, zikiripotiwa stori za wanafunzi kusomea chini anakasirika

Kayugumis

Member
Jun 6, 2022
85
63
Waandishi wa habari Mkoani Shinyanga wameomba mamlaka zinazohusika kuingilia kati vitisho vinavyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga.

Malalamiko ya waandishi wa habari ni juu ya hali ya ulinzi na usalama wao katika shughuli zao pindi wanapoandika habari za changamoto zilizopo katika Wilaya ya Kahama kwa kutishiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama.

Siku za karibuni, waandishi wa habari wametoa malalamiko yao katika ofisi za waandishi wa habari juu ya kutishiwa usalama wao na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festi Kiswaga.

Waandishi hao walidai kutishiwa kutokana na kuandika habari iliyohusu wanafunzi zaidi ya 400 kusomea chini ya miti, ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo alidai kuwa wamekuwa wakiichafua wilaya yake.

Pia waandishi hao wamedai kuwa hii imekuwa ni mara ya pili kwa kiongozi huyo kutishia usalama wa waandishi wa habari hasa wanapoandika changamoto za wilaya hiyo.

Mara kwa mara amekuwa akiwatishia atawahamisha wilaya au kuwarudisha kwao.

Waandishi hao wamedai kuwa, Mwandishi wa mwingine wa Mkoa wa Shinyanga ameshawahi kutishiwa kwa kuandika juu ya wajasiriamali kunyanyaswa na wachimbaji wadogo wa katika Mgodi wa Nyamishiga.

Hii hapa chini ni moja kati ya habari ambazo kiongozi huyo hataki kuzisikia au kuona zinaripotiwa, hii iliripotiwa na ITV.


Wanafunzi zaidi ya 400, katika shule msingi Butibu iliyopo wilayani Kahama, mkoani Shinyanga wamelazimika kusomea chini ya miti baada ya madarasa manne ya shule hiyo kubomolewa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.
 
Waandishi wa habari Mkoani Shinyanga wameomba mamlaka zinazohusika kuingilia kati vitisho vinavyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga.
Amewatishia wapi na kwa kutumia nini?

Acheni kuwa mnatafuta Public Sympathy isiyowastahili.

Fanyeni kazi zenu kwa weledi na msiwe biased!

That's all you need to know!
 
Back
Top Bottom