Mkuu wa Wilaya Vs Kamanda wa Polisi

Mkuu wa Wilaya Vs Kamanda wa Polisi

Mkuu hicho kitu ulikisoma wapi? Don't talk amateurish
Ukitaka uelewe vizuri siku moja wewe uwe DC nami niwe OCD alafu fanya alivyofanya huyo jamaa uone mamlaka yako yanapoishia. DC hawezi kuwa OCD lakini OCD anaweza kuwa DC, huo ndio ukweli
 
Ukuu wa wilaya ni mzigo kwa Taifa.
Wanashinda maofisini kuchati, hawana kazi
 
Jaribu ku google maana ya soldier
Ukigoogle maana ya soldier utaambiwa kwa tafsiri ya Kichina, kimarekani, kikorea n.k. kwa tafsiri ya kitanzania Katiba ipo wazi. Zipo nchi ambazo zina Police Services ambazo kwao Polisi ni huduma na sio Jeshi lakini kwetu tuna Police Force. Jitahidi kuuzoeza ubongo wako kukubali hata usichokipenda.
 
Mbna umewahi kuwekwa ndanj kwa order ya DC....je hiyo sio direct order? Mkuu sometimes kitu kama hukijui jaribu kunyamaza.
Usipende hisia zikuendeshe.
Order ya DC sio direct order. Kwa bahati mbaya hujui maana ya amri na maelekezo. Mkuu wa Wilaya hawezi kuliamuru Jeshi la Polisi kwa kuwa hana rank ya kufanya hilo bali anachoweza kufanya ni kuelekeza ili wenye amri wakikubaliana nae waitoe. Hapo ndio mtajua kwa nini upolisi nao ni taaluma ambayo asiyokuwa nayo hawezi kuielewa
 
Ukigoogle maana ya soldier utaambiwa kwa tafsiri ya Kichina, kimarekani, kikorea n.k. kwa tafsiri ya kitanzania Katiba ipo wazi. Zipo nchi ambazo zina Police Services ambazo kwao Polisi ni huduma na sio Jeshi lakini kwetu tuna Police Force. Jitahidi kuuzoeza ubongo wako kukubali hata usichokipenda.
Soldier ni neno la kingereza kaka lakini pia maana yake polisi hawamo
 
Soldier ni neno la kingereza kaka lakini pia maana yake polisi hawamo
Unajichanganya labda uje siku moja kituoni uone watu wanapofanya kazi ya kubaini uhalifu, wakakamata na kuanza upelelezi alafu aje mtu aanze kugawa vielelezo atakachofanywa. Nashukuru ustaarabu wa OCD kuzinyang'anya mbolea hizo kwa wananchi maana mwingine Mheshimiwa Rais angesikia DC yupo mahabusu
Order ya DC sio direct order. Kwa bahati mbaya hujui maana ya amri na maelekezo. Mkuu wa Wilaya hawezi kuliamuru Jeshi la Polisi kwa kuwa hana rank ya kufanya hilo bali anachoweza kufanya ni kuelekeza ili wenye amri wakikubaliana nae waitoe. Hapo ndio mtajua kwa nini upolisi nao ni taaluma ambayo asiyokuwa nayo hawezi kuielewa
 
Binafsi naona wote wapo sawa; police wako sahihi kwa muktadha wa mahakamani wakati mkuu wa wilaya ana haraka na muda. Nitafafanua:-
1. Police wanataka hao walio husika na wizi huo kuwapeleka mahakamani ili wapewe stahiki zao/yao hao wezi na wahujumu uchumi, kitendo cha kuikamata hiyo mbolea ni kutaka kua na ushahidi but again wapate pia mahali pa kuanzia kwa maana ya upelelezi with NO time limit.
2. Mkuu wa wilaya yeye ana kwenda na kasi ya muda, say upelelezi wa police uchukue miezi 2 then hiyo mbolea itakua haina maana kwa wakulima kwasababu ya msimu wa kilimo kua umeisha and may be hata expired date ya hiyo mbolea itakua tayari.

Changamoto yangu iko hapa; police na mahakama hawaangalii muda au msimu, upelelezi unaweza chukua hadi mwaka mzima and hence hata wanacho kiokoa kikawa hakina maana though kwa mkwara huo wa kukamata hiyo mbolea kutasababisha wengine wenye mawazo kama hayo kuogopa kufanya kama walio fanya wenzao. Mkuu wa wilaya in the other way round anaweza someka kua anataka kupoteza ushahidi and hence anaweza fikiriwa kua anahusika na tukio ingawa pia anaweza kua ni mtu anaye jail muda, kwake yeye Time is money, loosing opportunity is loosing money. Kwangu mimi wote wapo sahihi.
 
Hapo Polisi wana kosa la nidhamu na wanapaswa kuwajibishwa, Mkuu wa Wilaya ni sawa na raisi katika Wilaya, maamuzi yake OCD hapaswi kuyapinga hata kama kakosea. Huyo ni boss wake na anapaswa kutii pasipo kuhoji. OCD ni Mwakilishi wa IGP na DC ni Rais.
Acha kuongelea ushabiki DC hana mamlaka ya kugawa Mali ikiyokamatwa na wakati watu waliokamatwa wanashikiliwa na polisi anatakiwa asilikilize ushauri kutoka kamati yake ya ulinzi na usalama na ushauri kutoka mamlaka ya juu je aliyafanya hayo?
 
Unajichanganya labda uje siku moja kituoni uone watu wanapofanya kazi ya kubaini uhalifu, wakakamata na kuanza upelelezi alafu aje mtu aanze kugawa vielelezo atakachofanywa. Nashukuru ustaarabu wa OCD kuzinyang'anya mbolea hizo kwa wananchi maana mwingine Mheshimiwa Rais angesikia DC yupo mahabusu
Kaka usiongee kwa jazba kiswahili hakipo sawa soldier haima maana ya polisi soldier ni sehemu ya armed forces ambapo polosi sio armed forces
 
Uanajeshi na uaskari kiingereza tafadhali
Polisi kwa kingereza anaitwa policeman mwanajeshi ni soldier katika kingereza military ambayo ndio jeshi ni tofauti kabisa na Police angalia ata katika dictionary police sio sehemu ya military ila soldier anatoka katika military
 
Bahati mbaya uaskari sio uniform, uanajeshi either wa JW au Police ndio unaoonekana. Kiingereza Jeshi linaitwa Force, soldier kwa kiswahili ni askari. Sasa kwako wewe unaamini Polisi sio askari?
 
Nanikakudanganya polisi ni jenshi??? Rufi shule wewe ungekuwa unawaonawakati wakumuapisha Rais
Kama sio Jeshi ni nini na unapata wapi authority ya kusema sio Jeshi? Katiba kipengele gani kinasema polisi sio Jeshi?
 
Kuna kesi miaka ya nyuma ilitokea kuhusu wizi wa mbolea,watu walibomoa ghara la mbolea na kuiba,wakaenda kuweka hiyo mbolea kwenye mashamba yao,baadae upelelezi ukafanyika na wakagundulika na kukamatwa woote na kutiwa ndani, baadae mwl nyerere akawa ziarani hilo eneo,akaisikia hiyo hbr,alichokifanya ni kuamuru watolewa ndani hao wezi mala moja,na mabwana shamba waliokuwa wakihusika na kugawa hiyo mbolea woote akaamuru watiwe ndani kw kuchelewesha kuigawa hiyo mbolea wkt wakulima wanaihitaji,
 
Busara na sheria vitu viwili tofauti. Nimeangalia video nimesikitishwa na uelewa mdogo wa DC uliopelekea OCD ampige mabomu yeye na watu wake. Hivi hujiongezi tu kuona Polisi wanalinda vielelezo kwa nguvu hizo? Kazi ya Polisi haiwezi kukwamishwa na umaarufu wa kisiasa mwisho wa siku OCD angeharibu kesi angewajibika peke yake. Kuna tofauti gani ya wezi waliokamatwa na mali na Mkuu wa Wilaya aliyeiba kielelezo???? Eti twende ofisini, akaambiwa tunakwenda lakini hakuna mbolea kutoka hapa!!! Hajiongezi tu bado anataka sifa tu????
 
Kuna kesi miaka ya nyuma ilitokea kuhusu wizi wa mbolea,watu walibomoa ghara la mbolea na kuiba,wakaenda kuweka hiyo mbolea kwenye mashamba yao,baadae upelelezi ukafanyika na wakagundulika na kukamatwa woote na kutiwa ndani, baadae mwl nyerere akawa ziarani hilo eneo,akaisikia hiyo hbr,alichokifanya ni kuamuru watolewa ndani hao wezi mala moja,na mabwana shamba waliokuwa wakihusika na kugawa hiyo mbolea woote akaamuru watiwe ndani kw kuchelewesha kuigawa hiyo mbolea wkt wakulima wanaihitaji,
Nyerere hakuwa DC, alikuwa Rais!!! Mwenye nguvu za kusamehe hata wafungwa
 
Back
Top Bottom