Mkuu wa Wilaya Vs Kamanda wa Polisi

Mkuu wa Wilaya Vs Kamanda wa Polisi

Stori ni hivi?
Baada ya jeshi la polisi kukamata mbolea ya ruzuku iliyokuwa inatoroshwa na wafanya biashara kwenda Malawi..Mkuu wa Wilaya akaamua kuzigawa kwa wananchi..
Kumbuka hyo mbolea ni kielelezo au ushahidi mahakamani unaohitajika kwenye kesi..Kikosi cha polisi kikatumwa kuzikamata tena hizo mbolea..Mkuu wa wilaya amekasirika ameamua kumuita kamanda wa polisi ofisini ajieleze..
Wajuzi hapa nani anakosa?
Ni hawa wakuu wa wilaya waliopewa meno na baba yao ya kumweka mtu korokoroni hata masaa 48...??? Nafikiri alitaka kumweka OCD korokoroni alipokumbuka kwamba amegawa vielelezo vya kesi akaishia tu kupiga mkwara kwa kuwatetea WANYONGWE kwamba hii nchi ni nchi ya AMANI ni siyo nchi ya MABOMU OCD afike ofisini kwa mahojiano zaidi...
Ningekuwa mimi ni OCD ningepiga BOMU la machozi aliposimama/ningeamuru vijana wangu wampige na yeye TEAR GAS ili akili zikae vizuri...!!!
 
Mkuu wa wilaya ndiye amirijeshi wa majeshi yote hapo wilayani,
askari kaonyesha utomvu wa nidhamu,
inabidi ahamishwe tu
 
polisi sio jeshi,polisi ni idara
Wewe mshamba mkuu ila samahan kwa status niliyokupa! [emoji1] [emoji1]
Haya ndio majeshi ya TZ:
1.JESHI WANANCHI (JWTZ)

2.JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT)

3.JESHI LA POLISI TANZANIA (PT)
4.JESHI LA MAGEREZA TANZANIA (MT)

5.JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

ZIFUATAZO NDIO IDARA

1. IDARA YA UHAMIAJI (IMM)
Ruksa kutoa mawazo yako!!
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Hapo Polisi wana kosa la nidhamu na wanapaswa kuwajibishwa, Mkuu wa Wilaya ni sawa na raisi katika Wilaya, maamuzi yake OCD hapaswi kuyapinga hata kama kakosea. Huyo ni boss wake na anapaswa kutii pasipo kuhoji. OCD ni Mwakilishi wa IGP na DC ni Rais.
Kuwa Mwakilishi wa Rais hakumpi Absolutism kufikia kuharibu kesi! Pale yeyote anapovunja Sheria kwa Makusudi na HANA IMMUNITY AGAINST CRIMINAL CHARGES, lazima Dola imchukulie hatua!
 
Polisi siyo jeshi kama unavyoota ndoto,polisi ni raia kabisa kama raia wengne tofauti ni kwamba yeye anajua guu pande guu sawa ,

Polisi ni nanga tena wa demo ,mbona huyo mkuu wa wilaya hakumuita kamanda wa kikosi cha kambi ya jeshi hapo kwake atoe maelezo fooolish sana huyo mkuu wa wilaya na polisi wake
Duh mkuu wenzio foolish lakin
 
Naomba uelewe kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ipo kwenye Sheria ya Tamisemi ambayo Polisi wanaingia kama washauri kupitia Polisi Jamii na sio vinginevyo. Polisi hawatakiwi kupewa amri za moja kwa moja au maelekezo toka kwa viongozi wasio askari wa Polisi. JESHI LA POLISI LINAONGOZWA NA POLICE GENERAL ORDERS AMBAZO HAITOI MAMLAKA YEYOTE OVER POLISI KWA MWANASIASA YOYOTE ZAIDI YA AMIRI JESHI MKUU. Ukiona Polisi wanapokea maelekezo ya wanasiasa wanafanya hivyo kistaarabu tu.
Asant kwa elimu
 
Kuwa Mwakilishi wa Rais hakumpi Absolutism kufikia kuharibu kesi! Pale yeyote anapovunja Sheria kwa Makusudi na HANA IMMUNITY AGAINST CRIMINAL CHARGES, lazima Dola imchukulie hatua!
Hebu tupe mfano mmoja na unalosema...undoa lesions binafsi / madai
 
polisi sio jeshi,polisi ni idara
hapana,
Polisi sio idara kwa muktadha huu,

Idara~Department

TPDF ~Tanzania People's Defence Force
PT ~ Police Force Tanzania

Sasa apo unaanzaje kusema Polisi ni idara?? polisi sio idara labda uje unambie kitu kingine, aseee unadharau kinoma kwa jeshi letu linalotulinda aseee!!
Acha walinde mali zetu kwa amani!!
 
Hapo Polisi wana kosa la nidhamu na wanapaswa kuwajibishwa, Mkuu wa Wilaya ni sawa na raisi katika Wilaya, maamuzi yake OCD hapaswi kuyapinga hata kama kakosea. Huyo ni boss wake na anapaswa kutii pasipo kuhoji. OCD ni Mwakilishi wa IGP na DC ni Rais.
hata mimi nakuunga mkono ingawa sihami chama haa ahaaaaaa....
ila, kwa weledi wa kazi kwa sababu wote wanajenga nyumba moja, mi nilidhani kua wote watashirikiana ili hata wananchi wawe na confidence na serikali yao, waswahili wanasema umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu!!
Kutaka kujiona ndio mkubwa wengine hawana lolote hakuna ulazima wowote zaidi a kujenga chuki juu kwa juu!!!
 
hapana,
Polisi sio idara kwa muktadha huu,

Idara~Department

TPDF ~Tanzania People Defence Force
PT ~ Police Force Tanzania

Sasa apo unaanzaje kusema Polisi ni idara?? polisi sio idara labda uje unambie kitu kingine, aseee unadharau kinoma kwa jeshi letu linalotulinda aseee!!
Acha walinde mali zetu kwa amani!!
Fuatilia sana elimu za hao wanaodharau. Utapata shida hata kumlaumu. Cha msingi ni kumsamehe na kumuonea huruma!!!!
 
Vita vya kungunguru furaha kwa nyenyele watuhumiwa washashinda kesi
 
Hebu tupe mfano mmoja na unalosema...undoa lesions binafsi / madai
Ni kosa la jinai kuzuia utendaji wa maofisa wa Polisi, na pia ni kosa la jinai kuficha au kuharibu kielelezo cha kesi iliyopo mikononi mwa Polisi. Labda kuna jambo watu hawalioni hapo linaitwa contamination of evidence.
 
Fuatilia sana elimu za hao wanaodharau. Utapata shida hata kumlaumu. Cha msingi ni kumsamehe na kumuonea huruma!!!!
Mkuu unajua ni nini,
kumradhi ''sijui dini yako'' ila hata maandiko yanasema ajikwezaye atashushwa na ajishushaye atakwezwa!!
Binafsi nawapenda sana hawa viumbe wasiolala wananilindia duka langu apo ingawa halina mali nyingi, wananiongozea foleni pale ambapo huwa tunakosa ustaarabu na mengine mengi ingawa nawao kama binadamu wanamapungu yao.
 
Polisi siyo jeshi kama unavyoota ndoto,polisi ni raia kabisa kama raia wengne tofauti ni kwamba yeye anajua guu pande guu sawa ,

Polisi ni nanga tena wa demo ,mbona huyo mkuu wa wilaya hakumuita kamanda wa kikosi cha kambi ya jeshi hapo kwake atoe maelezo fooolish sana huyo mkuu wa wilaya na polisi wake
We ni mvivu sana kusoma ,,
 
Back
Top Bottom