Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,468
- 23,744
Hivi karibuni nmekuwa nikifuatilia kwa makini sana hali ya Mkuu wa Mkoa wetu. Nikiangalia videos na picha mbalimbali akiwa misikitini,makanisani na sehemu nyingine za nyumba za ibada akiombewa kwa kila imani aijuayo.
Hii ni ishara ambayo kitaalam inaitwa desperate condition au stressful. Ana msongo wa mawazo mkubwa sana. Anajaribu kushika kila sehemu ni kama mtu ambaye anazama baharini halafu akaona jani la mwembe anaweza shika akidhani linaweza msaidia asizame.
Watanzania ni wakati wa kumsamehe ndugu huyu kwa kuwa inawezekana kabisa amekuwa akikosa mwongozo mwema katika shughuli zake na siku zote kujikuta akitumika vibaya. Na wanaomtumia katika shughuli zao za kisiasa hufikia hatua wakajikuta inabidi wabaki nyuma ya pazia.
Kama binadamu anakosea. La muhimu kwake ni kujifunza. Hali aliyo nayo si rahisi kama tunavyomuona. Hana amani hata kidogo. Jamii inapokutenga pesa si suluhisho au nguvu. Ni kuirudia jamii husika na kutengeneza nayo. Na unapokumbuka kuwa hata waliokuzunguka sasa ni kwa vile wanajua una nguvu ya dola ila si kwa mapenz ya dhat hili ni tatizo kubwa sana kisaikolojia.
Ni wakati wa kumsaheme na kuelewa kuwa naye ni binadamu kama binadamu wengine. Hivyo anakosea kama binadam mwingine yeyote.