Mkuu wa mkoa wa Geita Apata ajali

Afadhali mwenye akili za konokono hagongi kiumbe,na hata akigonga haui!!hebu waonee huruma maskini ngombe waliogongwa na kuuliwa/kuumizwa vibaya na RC!!!hapo mi naona afadhali konokono kuliko rc! Over.


Halafu utakuta aliyeandika hii ni graduate
 
Kwa hiyo kwa akili uliyozaliwa nayo mkuu unaamini ng'ombe kwa kuwa yuko barabarani na sheria inakulinda umgonge!? Kwa kweli kua uyaone! Mara ngapi tunakutana na wanyama wanavuka barabara tena Dar mjini,tunapunguza mwendo na kuacha wapite...sembuse Geita. Ila wewe na Mr RC sheria inawalinda!
Poleni Ng'ombe na wenye mifugo.
Nimeuliza sheria inasemaje na si akili ya kuzaliwa nayo. sisi wengine hatukuzaliwa na akili. Akili tuli-aquire tu mbele ya safari. Kwa hiyo ninachotaka kujua sheria inasemaje kuhusu mifugo kuingia barabarani na kusababisha ajali?
 
mwendo kasi ndio tatizo kubwa
ingekuwa mwendo wa kawaida driver angeshawaona hao ngombe
inabidi mwenye ngombe alipwe fidia.hayo maeneo yanajulikana kuwa na mifugo
spidi kubwa ya nini au kwa vile vx?
 
Dah!!!!!!!!!!1hata kama,iweni na moyo wa huruma huyu ni binadamu mwenzio,mbona kwa sharo pole zilikuwa nyiingi,au ka sababu yeye alipotea kabisa?!

Sharo huwezi kumfananisha na kada,Sharo alikuwa na faida kwa Taifa kama kutuburudisha tukiwa na stress...alikuwa mbunifu wa sanaa...alikuwa anabuni vitu ili aendelee kuishi.,mwisho alikuwa mlipa kodi....hawezi kuwa sawa na hao mburula wanaotegemea fadhila kutoka CCM..,ndio maana wanagonga ng'ombe wa maskini yote ni kulewa cheo,kulikuwa na ulazima gani wa kugonga ng'ombe?.....dah maskini ng'ombe
 
Ng'ombe amekufa au yu hai!!!! na mwenye ng'ombe hajaumia!!!! Pole sana ng'ombe get well soon.
 
Ha ha ha.. Shemeji yako hajambo Mkuu Whabhejasana.. Ila mkuu mara nyingi sheria inapindishwa kum-favour mwenye uwezo au madaraka..

Hahahahahahahahahaaaaaaa!Mkuu hongera sjemeji yuko sawa,lakini mkuu unamtesa sana kwa sababu inaonekana hapumi mkuu wangu Sosoliso?!!
 
Kwa akili yako utasema hana! . Kwataarifa yako damu ya hao ngombe ndio ya thamani kuliko hata kamati kuu CCM!

Mkuu hapa unakosea,CCM inaingiaje kwenye hili jamani,mbona hakuna uvumilivu nyie watz?!!,fukunyua humu ndani utazikuta mada zinazoizungumzia CCM ukamalie hasira zako huko,hii ni iktu ingine kabisa mkuu wangu!
 
Ni kweli mkuu kwa sababu kwa body lako na lake ni lazima iwe hivyo,lakini sasa ina maana hutaki hata kumuachia ama unaogopa vipanga wanaweza kumpitia??!!

Ha ha ha.. Wahuni wengi wanapenda wake za watu Mkuu Whabhejasana.. Pamoja na kucikia mtu kanasiwa na mke wa mtu na kwamba mke wa mtu ni gundi bado hawaogopi.. So ninalinda mwenyewe..
 
Wakuu wa JF:

Taarifa za uhakika nilizozipata usiku huu zinasemea Mkuu wa Mkoa wa Geita Said Magalula Said amepata ajali katika eneo la Kijiji cha Buhalahala nje kidogo ya mji wa Geita baada ya gari lake kuwaparamia[/SIZE] Ng'ombe aliokua akivuka Barabara kutoka malishoni.

Hata hivyo hakuna mtu aliyepoteza maisha kwenye ajali hiyo wala kujeruhiwa vibaya isipokuwa majeraha na maumivu ya kawaida tu,lakini gari lake limeharibika vibaya sana na sehemu ya mbele ya Gari,alikuwa akitokea jijini mwanza na amepata ajali majira ya aa moja na nusu usiku huu.



Pamoja na makosa mengi, Watanzania tufike mahali tuthibitishe kwa utashi na kwa vitendo kuwa sisi ndiyo wenye lugha adhimu ya Kiswahili! Neno kuparamia, hapa limetumika kwa makosa. neno sahihi lingekuwa "kupamia". Mfano, gari linapogonga ukuta, tunasema limepamia ukuta. Paka anapokwea mti, tunasema paka kaparamia ukuta! Gari haliwezi kuparamia ukuta, bali linapamia ukuta. Gari linapamia ng'ombe, na si kwamba linaparamia! Kiswahili jamani ni lugha yetu. Tukienzi kwa kukitumia kwa usahihi.
 
Back
Top Bottom