Kutokana na mahitaji kuzidi uwezo wa ugavi, umeme utakuwa ukikatwa muda wowote kuanzia saa tisa alasiri mpaka tatu usiku kwa kupokezana baina ya viunga tofauti tofauti vya mkoa wa California, kwa mujibu wa Mheshimiwa Davin Newsom, Mkuu wa Mkoa.
Bwana Newsom ameziomba kampuni zenye mivyombo mizito ya umeme kama vile meli zilizoegeshwa bandarini kutumia nishati ya generator katika kipindi hiki kigumu kwa Wamarekani wa California.
Nchi mbalimbali duniani zikiwemo Ethiopia na Tanzania zimekuwa mstari wa mbele kufikiria mikakati mipya ya kuzindua vyanzo mbadala vya umeme wa ziada ili kukidhi mahitaji ya uchumi na idadi za watu zinazokua kwa kasi.