Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Musuguri afikisha miaka 100. Afanya Ibada maalum ya shukrani

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,226
5,947
IMG_20200104_161153_296.jpg

MKUU wa Majeshi mstaafu nchini Tanzania, Jenerali David Musuguri maarufu ‘Chakaza’ au Mtukula, ametimiza umri wa karne moja (miaka 100) tangu alipozaliwa Januari 4, 1920.

Hafla ya kuadhimisha miaka 100 ya Msuguri inafanyika leo Jumamosi Januari 4, 2020 nyumbani kwake kijiji cha Butiama mkoani Mara kwa ibada maalum inayoongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma, Michael Msonganzila.

Mmoja wa wana familia, Bahame Nyanduga, amesema pamoja na ibada, maadhimisho hayo pia yatahusisha shughuli na sherehe za kifamilia. Ibada ya shukrani inayofanyika nyumbani kwa mkuu huyo wa jeshi mstaafu imehudhuriwa na viongozi kadhaa wakiongozwa na Mbunge wa Musoma vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo.

Pamoja na ngazi mbalimbali za kijeshi, Msuguri alikuwa Mkuu wa Majeshi kati ya mwaka 1980 hadi 1988. Katika moja ya mahojiano yake, aliwahi kusema alichukizwa na unyama ambao Idd Amin alikuwa anaufanya na angetokea akamkamata angemchinja.

Wakati wa vita ya Kagera, aliongoza vikosi vya Tanzania kumpiga aliyekuwa Rais wa Uganda, Idd Amin Dada, mwaka 1979. Msingi wa vita hiyo ilitokana na Amin kuuvamia mkoa wa Kagera, Novemba 1978, hali ambayo rais wa wakati huo, Mwalimu Nyerere hakukubaliana nao na kutangaza kumpiga na kumwondoa.

Katika uvamizi huo, Amin alishusha bendera ya Tanzania na kupandisha bendera ya Uganda huku Watanzania ambao hawakuwa na hatia, wakubwa kwa wadogo, waliuawa na wengine kupata vilema vya kudumu, hali ambayo ilimuudhi Rais wa Tanzania wa wakati huo, hayati Julius Nyerere, na kutangaza vita ambayo Tanzania ilishinda chini ya Msuguri.

Msuguri alisema kwenye uwanja wa vita majeshi ya Amin yalipigwa na majeshi ya Tanzania na kusababisha Ikiongozi huyo kukimbilia Libya alikopewa hifadhi.

Akihubiri wakati wa misa hiyo, Msonganzila amefichua siri ya Msuguri kuishi miaka 100 akisema ni mazoezi ya kijeshi, nidhamu ya maisha na vyakula vya asili.

“Hofu ya Mungu ni siri nyingine iliyomfanya Mzee Msuguri kuishi miaka mingi. Maisha ya amani na heshima kuanzia ndani ya familia, serikalini na jamii kwa ujumla pia ni miongoni mwa sababu za Jenerali Msuguri kuishi miaka 100,” alisema Msoganzila.

Mahubiri hayo yalianza kwa kuongoza familia, ndugu, jamaa, marafiki na viongozi kadhaa wa serikali na jamii kumwimbia wimbo wa “happy birthday” ambapo Msonganzila amemwombea Msuguri kuishi miaka mingine 100 na kufikisha miaka 200.
 
Butiama. Mkuu wa Majeshi mstaafu nchini Tanzania, Jenerali David Musuguri maarufu ‘Chakaza’ ametimiza umri wa karne moja tangu alipozaliwa Januari 4, 1920.

Hafla ya kuadhimisha miaka 100 ya Jenerali Msuguli zinafanyika leo Jumamosi Januari 4, 2020 nyumbani kwake kijiji cha Butiama mkoani Mara kwa ibada maalum inayoongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma, Michael Msonganzila.

Mmoja wa wana familia, Bahame Nyanduga amesema pamoja na ibada, maadhimisho hayo pia yatahusisha shughuli na sherehe za kifamilia.

Pamoja na ngazi mbalimbali za kijeshi, Jenerali Msuguri alikuwa Mkuu wa Majeshi kati ya mwaka 1980 hadi 1988.

Ibada ya shukrani inayofanyika nyumbani kwa mkuu huyo wa jeshi mstaafu imehudhuriwa na viongozi kadhaa wakiongozwa na mbunge wa Musoma vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo.

Wakati wa vita ya Kagera, Jenerali Musuguri aliongoza vikosi vya Tanzania kumpiga aliyekuwa Rais wa Uganda, Idd Amin Dada mwaka 1979.

Katika moja ya mahojiano yake, Jenerali Msuguri aliwahi kusema alichukizwa na unyama ambao Idd Amin alikuwa anaufanya na angetokea akamkamata angemchinja.

Msingi wa viti hiyo ilitokana na Idd Amin kuuvamia mkoa wa Kagera Novemba 1978 hali ambayo rais wa wakati huo, Mwalimu Nyerere hakukubaliana nao na kutangaza kumpiga na kumwondoa.


Katika uvamizi huo uliofanywa na Idd Amin alishusha bendera ya Tanzania kuamua kupandisha bendera ya Uganda huku Watanzania ambao hawakuwa na hatia wakubwa kwa wadogo waliuawa na wengine kupata vilema vya kudumu.

Katika moja ya mahojiano aliyowahi kuwafanya Jenerali Msuguri alisema kwenye uwanja wa vita majeshi ya Idd Amin yalipigwa na majeshi ya Tanzania na kusababisha Idd Amin kukimbilia Libya kuomba hifadhi baada ya kuzidiwa

Chanzo: Mwananchi
 
So huyu mwamba wa vita leo hii anaadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa. Alizaliwa tar 4 Jan 1920. Nilikua naangalia video hii toka katika "sherehe" hizo zilizofanyika huko kwake Butiama.

Vitu kadhaa nilivyojifunza ni tofauti kubwa ya kizazi hicho na kizazi cha sasa, ni kwamba kizazi hicho waliweza kufanya mambo makubwa sana kwa umri mdogo.

-Kwamba alianza Jeshi akiwa na umri almost miaka 13??

-Kizazi hicho ndo ilikua kijana ukibalehe tu(around 13/14 yrs) unakabidhiwa mke na familia unaanzisha

- Kizazi hicho ndio kilitoa watu kama Salim Ahmed Salim(Alikua balozi akiwa kijana mdogo kabisa, umri wa vijana walio Chuo kikuu kwa sasa)

-Kizazi cha sasa watu wengi mpaka wanastaafu wana utumish wa Miaka 30 mostly au mpaka 35 kwa waliobahatika.

- Vijana wa sasa kuna mambo mengi tunapaswa kujifunza/kuendelea kujifunza.

Nadhani kuna mjadala mkubwa inabidi ufanyike ili kutambua ni namna gani Nguvu kazi ya taifa inatumika. Kuliko kufuata njia moja tu "formal" ya kusoma mpaka kuanza Utumishi watu wakiwa na miaka 25-30(karibu miaka 16 ya masomo)

Happy 100th Birthday Kamanda Mutukula
Happy 100th Biryhday Gen(Rtd) David Bugozi Musuguri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah! kumbe jamaa alikwenda msituni kuongoza vita akiwa na miaka sitini? Jamaa yuko fit kweli kweli. Hongera sana Generali Msuguli kwa kuingia katika ligi nyingine; ni asimia nne tu ya watu duniani hufikia umri huo wa 100.
 
Leo mtoto wa miaka 13 hata kufua nguo zake hawezi anafuliwa na dada wa kazi shule anapelekwa na dada au baba akichelewa kurudi tu sm zinaanza kupigwa kwa walimu unategemea nini

Mtoto wa miaka 13 anayejitegemea ni wa uswahilini tu hawa dady I hate that channel I want cartoon hamna kitu mzee
 
Happy birthday commander.

Kumbe Msuguli alikuwa mkubwa kuliko Nyerere?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo. Mwalimu alizaliwa mwaka 1922 hivyo Msuguli ni mkubwa kwa umri. Ila kwa hadhi ya Uongozi au madaraka, Mwalimu alikuwa Mkubwa kwa Msuguli. Wakati Msuguli alikuwa Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Mwalimu alikuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Tanzania.
 
Ndiyo. Mwalimu alizaliwa mwaka 1922 hivyo Msuguli ni mkubwa kwa umri. Ila kwa hadhi ya Uongozi au madaraka, Mwalimu alikuwa Mkubwa kwa Msuguli. Wakati Msuguli alikuwa Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Mwalimu alikuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Tanzania.

Kwahiyo aliongoza vita akiwa na miaka 60?!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Leo mtoto wa miaka 13 hata kufua nguo zake hawezi anafuliwa na dada wa kazi shule anapelekwa na dada au baba akichelewa kurudi tu sm zinaanza kupigwa kwa walimu unategemea nini

Mtoto wa miaka 13 anayejitegemea ni wa uswahilini tu hawa dady I hate that channel I want cartoon hamna kitu mzee

Hahaaa kweli kina junia ni shida sana
 
Back
Top Bottom