benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
TANZANIA inatarajiwa kujitangaza kimataifa kupitia Mkutano wa 28 (COP 28) wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, utakaofanyika Dubai Umoja wa Falme za Kiarabu kuanzia Novemba 28 hadi 12 Disemba 2023.
-
Hayo yamesemwa leo Novemba 11, 2023 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dk. Selemani Saidi Jafo wakati akitoa tamko kuhusu ushiriki na msimamo wa Tanzania kwenye majadiliano ya mkutano huo.
-
Amewakaribisha wadau mbalimbali waliopo nchini kutumia fursa ya Mkutano wa COP28 kwa kuhakikisha nchi inaendelea kujitangaza na kuleta manufaa ya kijamii na kiuchumi kwa maendeleo ya wananchi.
-
Dk. Jafo amesema Tanzania imepanga kuendesha mkutano mkubwa wa pembezoni utakaowaleta pamoja Wakuu wa nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na mabara mengine pamoja na wadau mbalimbali kwa lengo la kuvutia wawekezaji katika fursa za mabadiliko ya tabianchi zilizopo nchini.