Ktk mkutano mkubwa wa
hadhara uliofanyika leo jijini Arusha,pamoja na mambo mengi
yaliyozungumzwa na watu mbali mbali,.Naibu Meya wa jiji la Arusha
amesema ktk kipindi cha siku kumi amefungua mikutano kadhaa ikiwepo wa
Banki ya Dunia ambapo wamekubali kuwapa jiji la Arusha kiasi tsh 20
bilioni kwaajili ya ujenzi wa barabara zake.Aidha wawekezaji hao
wameridhishwa na kiwango cha usimamizi wa miradi inayotekelezwa ktk jiji
hilo ikiwemo ile ya barabara kiasi cha kubakia pesa nyingi jambo ambalo
halijawahi kutokea ktk nchi za Africa mashariki.Aliwaeleza wawekezaji
hao kwamba kazi hiyo inafanywa na madiwani wa chama cha upinzani Chadema
ambapo yeye ni diwani wa chama hicho.Hivyo watoe fedha hizo bila
mashaka yoyote kwani zitafanya kazi hiyo iliyokusudiwa bila kupotea hata
senti moja,
source mimi mwenyewe kwenye mkutano wa Chadema viwanja vya Kilombero
stand ya samunge.