Mbunge wa Arusha Mjini ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, Mh Godbless Lema ameeleza kushangazwa sana na kinacholazimishwa na watu na viongozi wa CCM akiwemo Mwigulu Nchemba, January Makamba, Ridhiwani Kikwete na wengineo, kuwataka Chadema wapatane na kumrudishia vyeo Bw Zitto Kabwe.
Akiwahutubia wananchi wa Arusha jana viwanja vya Kilombero, Lema aliwaachia kama swali wananchi hao watafakari wenyewe kwamba "Migogoro ndani ya Chadema ni faida kwa CCM, sasa inakuwaje wanatamani Chadema wapatane!? Wanamaslahi gani na Upatanishao huo!?"
Katika mambo mengine Lema alisema pia kwamba tofauti na maigizo mengi ya waliovuliwa vyeo kuwa kuna watu wanachoma kadi na kutoa matamko wakisaidiwa na wanapropaganda wa CCM, ukweli ni kwamba wananchi wengi wanaipongeza Chadema kwa maamuzi ambayo hakuna chama kingine nchini kimeweza kufanya.
Sentensi nyingine alizonukuliwa Mh Lema ziko hivi..
" Wanasema Chadema itaparaganyika. Chadema haitaparaganyika kwa sababu ya migogoro. Chadema itaimarika kwasababu ya changamoto na migogoro"
"Hakuna mtu maarufu zaidi kuliko Chadema. Chadema ni maarufu kuliko kiongozi yeyote. Kama mtu ni maarufu, umaarufu wake utusaidie kuimarisha chama na sio kuua chama"
Lema alihitimisha hotuba yake kwa kuzungumzia mzaha wa Serikali katika swala la gharama za umeme nchini na kuwatupia lawama wananchi kuwa ndio wanaruhusu kuonewa siku zote. Alisema tabia ya watanzania kuonekana wameshazoea umasikini na matatizo ndio mambo yanayowapa jeuri watawala kuendelea kuwanyonya. Alitolea mfano wa mashine za risiti za TRA kuwa ni mradi wa kinyonyaji kwasabu bei wanayouzia ni mara kumi ya bei halisi, kitu alichodai ni makakati wa kuwaibia wananchi kutafuta hela za kampeni 2015.
Lema pia alizungumzia utapeli unaotaka kufanywa na Lowassa jijini hapa kuteka kiwanja cha umma akidaiwa anataka kukodi kufungua Car Wash lakini mpaka sasa ameshajenga uzio wa thamani ya milioni 500. Uzio wa tofali 500mil kwa Car Wash ya kukusanya elfu 80 kwa siku??
NENO LA AMANI GOLUGWA (KATIBU WA KANDA YA KASKAZINI)
Akizungumza katika mkutano huo wa hadhara jana Nov 29, 2013 Ndg Amani Golugwa aliwataka wananchi na wapenzi wa Chadema kuwa wavulimivu, wawaamini viongozi na wawape ushirikiano kukijenga chama. Alisema mtaji mkubwa wa Kiongozi ndani ya Chadema ni UADILIFu na hivyo chama hakitasita kumuwajibisha yeyote yule bila kujali cheo chake endapo anakwenda kinyume na misingi ya chama.
Golugwa alisema kwa Chadema kipaumbele cha sasa ni ujenzi wa chama kuanzia ngazi yamsingi na hivyo kuomba ushirikiano na wala wananchi wasihuzunishe na maamuzi ya chama chao maana inalazimu kufanya hivyo ili chama kiimarike.
Aliwashangaa wale waliovuliwa vyeo kuhaha kutoa matamko na kushangazwa na utetezi wao aliouita wa kijinga kuwa eti waliandaa mkakati ili waje wamshirikishe Zitto. Golugwa akahoji ni kiherehere gani kimewakumba kumuhangaikia mwanaume mwenzao kama kweli hawajui anahitaji ama la!?
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Arusha kilifanya mkutano wa hadhara eneo la Kilombero uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi ambao muda wote walikuwa wakikatisha hotuba za viongozi kwa kushangilia na kupandishia maneno yao. Mkutano huo ulihudhuriwa na madiwani karibu wote wa Chadema Arusha pamoja na Naibu Meya Msofe, huku viongozi mbalimbali wa Wilaya na Mkoa wakiwa miongoni mwao bila kuwasahau makamanda wengine kama Ally Bananga n.k!
View attachment 124023
Amani Golugwa Jukwaani
View attachment 124024
Ally Bananga jukwaa kuu
View attachment 124026
Naibu Meya, Diwani wa Daraja Mbili Mh Msofe akiteta na wadau
View attachment 124030