Mkutano wa BRICS waonyesha nguvu mpya katika mabadiliko ya mfumo wa kimataifa

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111465972742.jpg


Mkutano wa kwanza tangu kuongezwa kwa nchi wanachama wa BRICS ulifanyika wiki iliyopita, ambapo rais wa China, Xi Jinping, alitoa hotuba na kusisitiza kuwa, ni muhimu kwa nchi wanachama kukutana kwa wakati huo na kupaza sauti kwa ajili ya haki na amani kuhusu suala la Israel na Palestina.

Katika hotuba yake, rais Xi alisisitiza kuwa, kusimamisha mapigano mara moja, kufungua njia salama za kupitisha misaada ya kibinadamu, na jamii ya kimataifa kuchukua hatua halisi za kivitendo kuzuia mapigano hayo kuenea ni masuala ambayo ni muhimu nay a dharura.

Ukanda wa Gaza una eneo lenye ukubwa kilomita za mraba 360, na idadi ya watu katika eneo hilo ni Zaidi ya milioni mbili. Eneo hilo limezingirwa na Israel kwa Zaidi ya muongo mmoja, na mapigano yanayoendelea yamelifanya eneo hilo kukabiliwa na uhaba mkubwa wa maji, umeme, na mafuta, na hivyo kuhatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo.

Kutokana na hilo, katika hotuba yake, rais Xi amesisitiza adhabu ya pamoja kwa watu wa Gaza ni lazima ikomeshwe, na kueleza kuwa, China inachukua hatua halisi kusaidia watu wa Gaza.

Kwa mujibu wa rais Xi, China imetoa msaada wa dharura wa kibinadamu wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 2 kupitia Mamlaka ya Palestina na mashirika ya Umoja wa Mataifa, na mahitaji ya kibinadamu yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 2.1 kwa msaada wa Misri ili kupunguza mgogoro wa kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.

Nafasi ya China katika kukabiliana na mgogoro wa Israel na Palestina imetambuliwa vizuri na jamii ya kimataifa. Ikiwa nchi mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa Novemba, China imechukua hatua za kivitendo kuondoa mvutano na kujenga maafikiano. Matokeo yake, ikiwa ni siku zaidi ya 40 tangu mapigano mapya kati ya Israel na Palestina yatokee, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kwanza linalolenga wasiwasi wa kibinadamu. Hatua hii imeonyesha kuwa jamii ya kimataifa imetambua nafasi ya China katika suala hilo.

Kama alivyosema rais Xi katika hotuba yake, chanzo cha hali ya Israel na Palestina ni ukweli kwamba, haki ya utaifa ya Wapalestina, haki yao ya kuishi, na haki yao ya kurejea zimepuuzwa kwa muda mrefu. Hivyo, suluhisho la nchi mbili ndio njia pekee ya kusuhisha mgogoro huo. China imekuwa ikiunga mkono wito wa Wapalestina wa hazi zao kisheria na kupendekeza majadiliano ya kisiasa katika kutimiza amani endelevu na usalama katika kanda hiyo.

Ingawa Umoja wa Mataifa umerejea tena ahadi yake ya kutimiza matakwa ya mataifa mawili jirani, ambayo Yerusalemu ya Mashariki ni mji wao mkuu, na kusuhisha vizuri suala la wahamiaji wa Palestina, mchakato wa amani kati ya Israel na Palestina umeshuhudia changamoto kubwa katika miaka ya karibuni.

Kwa upande mmoja, juhudi za Israel za kuongeza eneo la makazi ya Wayahudi Magharibi mwa Mto Jordan zimeongezeka. Kuongezeka kwa kasi kwa makazi ya Wayahudi na kuzingirwa kwa Ukanda wa Gaza kumeongeza mvutano kati ya Wapalestina na Waisrael, na hivyo kuondoa imani katika majadiliano ya amani kati ya Israel na Palestina.

Kwa upande mwingine, majadiliano kati ya pande hizo mbili yaliyoongozwa na Marekani yamesimama kwa muda mrefu. Israel inalielezea kundi la Hamas kama “kundi la kigaidi” katika mapigano yanayoendelea sasa, huku Hamas ikiiweka Israel katika nafasi ya taasisi isiyo rasmi ya kisiasa katika nyaraka zake za kisiasa. Matokeo yake ni kwamba, mawasiliano ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili yameshindikana kwa kuwa wanakosa mfumo sahihi wa majadiliano. Kwa mtazamo huu, mgogoro wa Palestina na Israel unahitaji upatanishi wa haraka kutoka jamii ya kimataifa.

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kuitisha mapema mkutano wa kimataifa wa Amani ambao utakuwa na mamlaka ya kujenga maafikiano ya kimataifa kwa Amani, na kufanya kazi ili kupata jibu la suala la Palestina ambalo ni la kina, la haki na endelevu.

Mkutano maalum wa BRICS kuhusu suala la Israel na Palestina una umuhimu mkubwa katika kuimarisha umoja na uratibu kati ya nchi za Kundi hilo, na kuondoa wasiwasi wan chi nyingine kuhusu kupanuka kwa kundi hilo. Baadhi ya nchi zinadai kuwa BRICS itakabiliwa na changamoto kubwa kwa umoja wake baada ya kuongeza nchi wanachama na haitakuwa na ufanisi wa kukabiliana na hatari na changamoto mpya.

Lakini kuitishwa kwa mkutano huo kumeonyesha nia halisi ya nchi za BRICS kuungana na kushirikiana, na kwamba zitatoa mchango mkubwa Zaidi katika kujenga utaratibu mpya wa kimataifa wa kisiasa na kiuchumi.

Kama nguvu mpya ya mabadiliko ya hali ya kimataifa, mfumo wa BRICS unaweza kuchukua nafasi kubwa Zaidi katika suala la Israel na Palestina na masuala mengine muhimu ya kimataifa. Kama alivyosema rais Xi, mfumo wa ushirikiano wa BRICS ni jukwaa muhimu kwa masoko yanayoibuka na nchi zinazoendelea kuimarisha mshikamani na ushirikiano ili kulinda maslahi yao ya pamoja.

China, pamoja na nchi nyingine za BRICS, itaendelea kutoa mchango wake katika amani na maendeleo ya dunia.
 
Hiyo Brics mbona haiangali haki ya waukraine waliovamiwa na urusi wakauawa kwa halaiki mfano huko Bucha, Lyman na maeneo ya Ukraine kuchukuliwa na urusi,kuchukuliwa kwa watoto wa Ukraine ila wanaiona Gaza pekee yake hii dunia imejaa unafiki na vitendo vya double standard.
 
Kumbe ndio maana waarabu walienda kumpigia kafiri china waape msaada,china ajichanganye atajuta,uzuri ni kwamba china,urudi na irani ni mbwa koko.
 
Back
Top Bottom