BRICS ina nafasi muhimu katika usimamizi wa dunia

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111450644579.jpg

Watu wengi wamekuwa wakiifananisha BRICS na NATO, kitu ambacho si sahihi kabisa. Tofauti na NATO, BRICS haina makao makuu, na pia haina uhusiano na makubaliano ya kijeshi, badala yake, kundi hilo linajihusisha zaidi na masuala ya kiuchumi. Kundi hili la BRICS linaunganisha juhudi za nchi zinazotaka kujikwamua na ubeberu wa Magharibi wa kuongoza nyingine kiuchumi, na kufuata njia ya kuimarisha maingiliano ya kiuchumi na shughuli za maendeleo kwa nchi zinazoendelea.

Awali, kundi la BRICS lilijumuisha nchi tano, ambazo ni Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini, ambayo ilijiunga na kundi hilo mwaka 2011. Mfumo wa kiuchumi wa nchi wanachama wa kundi hili umekuwa na athari kubwa katika masoko, na nchi zote, zikiwemo za kundi hili, zinaunganishwa na nadharia ya kimataifa, ambayo ni nchi zinazoendelea. Kundi la BRICS lina malengo kadhaa, ikiwemo kupunguza changamoto za mgogoro wa kiuchumi duniani, kuboresha ubora wa maisha ya watu, na kutetea mageuzi ya hatua kwa jatua kuelekea matumizi ya teknolojia ya juu katika sekta mbalimbali. Nchi washiriki zinadumisha usawa na kuheshimiana, na hivyo, kundi hili halina mmiliki, makao makuu, katibu mkuu, kanuni wala sheria.

Mwezi Agosti mwaka jana, kundi la BRICS lilikubaliana kuongeza wanachama, na kuridhia ombi la Saudi Arabia, Iran, Ethiopia, Misri, Argentina na Falme za Kiarabu, kuwa nchi wanachama, ambao uanachama wao umeanza rasmi Januari Mosi mwaka huu. Habari zinasema nchi zaidi ya 40 zilionesha nia ya kutaka kujiunga na BRICS, zikiwemo 22 ambazo ziliwasilisha rasmi ombi la kujiunga. Uamuzi wa kuongeza wanachama unaashiria utayari wa nchi wanachama waanzilishi wa BRICS. Kutokana na nchi mpya zilizojiunga nalo, kundi hili sasa linachukua asilimia 37.3 ya pato la dunia, na pia kuongezeka kwa nchi wanachama kunaimarisha uwakilishi wa BRICS katika maeneo kama Mashariki ya Kati na Afrika.

Kundi hili pia linapanga kuzindua mfumo wake wa malipo ambao unaweza kutumika katika nchi wanachama. Kutokana na maelekezo maalum kuhusu malengo, shughuli na uongozi, mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa BRICS unafanyika kila mwaka katika moja ya nchi wanachama, utamaduni ambao umeanza mwaka 2009, mkutano wa kwanza ulipofanyika. Kundi la BRICS halina rais wa kudumu, na kazi za kundi hilo zinaratibiwa na nchi mwenyekiti kwa kipindi cha mwaka mzima inapokuwa madarakani. Maamuzi muhimu yanafanyika katika majadiliano, hususan makubaliano ya ushirikiano muhimu katika maeneo ya nishati, afya, sayansi na teknolojia. Kazi za kundi hili hazihusishi tu mkutano wa mwaka wa wakuu wa nchi na serikali, kuna idara kadhaa katika nyanja mbalimbali zinazofanya kazi ndani ya kundi hilo, zikitekeleza kazi zilizopangwa katika mkutano mkuu.

Kundi la BRICS lina mipango mikubwa. Awali, ilitabiriwa kuwa India itashuhudia ukuaji mkubwa wa uchumi. Wataalamu wanaamini kuwa, China, na India pia, zitakuwa viongozi wa dunia katika usambazaji wa bidhaa za viwandani. Nchi hizi mbili zinatarajiwa kuchukua nafasi ya kwanza katika eneo la huduma ya ugavi. Katika makadirio hayo, Russia na Brazil zimepewa nafasi ya kuongoza duniani katika ugavi wa malighafi.

Utaratibu kama huu wa kiuchumi wa nchi hizo hautoi uhakikisho, bali unatoa uwezekano wa kuibuka kwa kundi lenye nguvu na lenye mamlaka halali. Kutokana na nchi wanachama kuongoza katika maeneo mbalimbali, Marekani inaweza kujikuta ikikosa fursa na nafasi yake kama kituo cha teknolojia, uzalishaji na manunuzi.

Kundi la BRICS pia limejikita katika kuboresha maisha ya kila mwananchi wake, ingawa hatua hii inatekelezwa polepole, lakini kundi hili linafanya kazi nzuri ya kipekee katika kuhakikisha hilo.

Kutokana na haya yote, ni wazi kwamba kundi la BRICS linajitahidi kushirikiana ili kuboresha maisha na maendeleo ya nchi wanachama wa kundi hilo, na hatimaye, kwa dunia nzima.
 
View attachment 2909595

Mkuu asante kwa maelezo mazuri na yanayoeleweka vizuri. Hizi ndio mada ambazo Great Thinkers tunatakiwa tujadili huku tukizingatia kuangazia maendeleo ya nchi yetu (Tanzania) kupitia majukwaa mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi.
 
Zamani nilikua naamini sababu iliyofanya nchi za ulaya magharibi na Marekani (Wanajiita Global North) ziendelee ni uongozi bora, siasa safi na uchapaji kazi
Ila nilivyokuja kusoma historia yao, hivyo vyote hapo juu ni uongo mtupu

Hizo nchi za Global North zilikua kiuchumi kwa kutumia ubeberu na ukoloni (imperialism & colonialism)

Ni nchi za kimafia tu.

Ndani ya miaka 40 tu, bila kurusha risasi wala kuvamia nchi yoyote ile duniani, China imetoka kuwa nchi masikini kuliko Haiti kuwa nchi tajiri zaidi duniani kuliko Marekani (kwa kipimo cha PPP)

BRICS ina future, kwasababu inaunganisha nchi zenye vitu viwili in common

Nchi zisizo za kibeberu na zenye real economy

Uchumi wa Marekani kwa sehemu kubwa ni "Financialized Economy", uchumi wa mazingaombwe
Dollars haina thamani yoyote, inalindwa kwa mtutu
 
Back
Top Bottom