Mkutano Mkuu Wa CCM - Matarajio Ya Kujiokoa?

hao wote uliowataja ni marehemu kasoro Mugabe, halafu second sio watanzania so i they dont stand a greater chance in me kuanza kuwachambua ilihali viongozi wetu (wa vyama vyote) wanahitaji uchambuzi kamilifu !

Shukrani !

Nilikuwa nakukumbusha MAPUNGUFU ya takwimu (after saying JK alishinda kwa 80%).Dead or Alive,hoja ni kwamba USHINDI WA KISHINDO doesnt necessarily mean mchaguliwa anapendwa hususan katika siasa zetu ambazo zimetawaliwa na nini ulichonacho na sio wewe ni nani (and by "nini" simaanishi sera bali fedha na mbinu chafu),that's WHAT YOU HAVE AND NOT WHO YOU ARE.Hakuna dhambi kutolea mifano,kujadili au kuiga wasio Watanzania,if kwa kufanya hivyo tutafika tunapotaka kwenda.Sidhani kama mtu anayeipenda nchi yake hatopenda kutolea mifano ya mataifa kama Rwanda au Msumbiji ambayo yamefika hapo yalipo from the dust kwa vile tu viongozi wa nchi hizo walikuwa madarakani kwa AJILI ya wananchi na SIO WASHKAJI ZAO.By the way,mbona chama chenu kinapenda sana kutumia mifano ya conflicts za majirani zetu ku-underline hoja yao ya "amani na utulivu" (wa nyumba ndogo zao,mahekalu yao na mashangingi yao,I suppose!)
 
...nada nada dadd manada dad dad da d dad dad ,hivi CCM mafisadi wakubwa na makada wa rushwa na umaskini wa nini humu wezi wakubwa wale
 
...nada nada dadd manada dad dad da d dad dad ,hivi CCM mafisadi wakubwa na makada wa rushwa na umaskini wa nini humu wezi wakubwa wale

lakini hili ni swali *maana limeanza na hivi, statement au nini ?? maana haina kituo, kiulizo, yaani nada kama ulivyosema !!
 
Dodoma: Fitna tupu!

2007-11-01 17:56:49
Na Emmanuel Lengwa, Dodoma


Wakati joto la uchaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi linazidi kupanda, mjini hapa ni fitna tupu!

Wakiongea na gazeti hili baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali zikiwemo za ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, wamedai kuwa wapinzani wao na wapambe wao wamekuwa wakitembeza fitna dhidi yao, lengo likiwa kuwachafua na kujisafishia njia.

Licha ya fitna kutembea kimya kimya na baadhi ya vimemo kutua hadi mikononi mwa mapaparazi, inadaiwa kuwa baadhi ya wanasiasa wanaowania nafasi za uongozi, wengi inadaiwa wako `Bungeni` kimwili lakini kimawazo wako kwenye kampeni.

Baadhi ya wanaowania uongozi wameonekana wakitembeza `vimemo` vyenye kujinadi kila pembe ya mji wa Dodoma ikiwemo ndani ukumbi wa Bunge.

Alasiri imeshuhudia vipeperushi kibao vya kuwania nafasi mbalimbali vikisambazwa ndani ya chombo hicho kikubwa cha kutoa maamuzi.

Kwa siku nzima ya jana, wahudumu wa Bunge walionekana wakiwa `busy` wakisambaza vipeperushi vyenye nembo na rangi za chama tawala kwa wabunge huku kikao kikiendelea.

Spika wa Bunge, Mhe. Samwel Sitta, alipoulizwa na mwandishi juu ya kuzagaa kwa vipeperushi hivyo vyenye nembo ya chama ndani ya ukumbi wa Bunge, alisema ni suala la kawaida kwa wabunge kupelekeana ujumbe lakini si sawa kufanya kampeni ndani ya Bunge.

Akafafanua kuwa ni marufuku kwa mujibu wa kanuni ya Bunge kwa mbunge ama mtu yeyote kuiingia Bungeni akiwa amevalia mavazi yanayoonyesha itikadi ya chama chochote.

Aidha, akasema kutumiana `vimemo` miongoni mwa wabunge ni suala la kawaida, hata kama vimemo hivyo vitakuwa vikihusu vyama vyao.

``Mavazi dhahiri ya vyama vya siasa hayaruhusiwi ndani ya ukumbi, kupitishiana karatasi miongoni mwa wabunge ni jambo la kawaida hata kama inahusu vyama vyao,`` akasema Spika Sitta.

Uchaguzi huo wa CCM ndio umekuwa gumzo mjini hapa kiasi cha kusababisha baadhi ya wabunge waliozoeleka kuwa machachari, kushindwa kuonyesha cheche zao, pengine kutokana na ubize wa shughuli hiyo.

Katika kikao cha juzi, wabunge wawili pekee walichangia muswada wa mabadiliko mbalimbali ya sheria ya mwaka 2007 uliowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Johnson Mwanyika.

Wabunge waliochangia walikuwa ni Mbunge wa Karatu, CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa na Mbunge wa Kyela, CCM, Dk. Harrison Mwakyembe.

SOURCE: Alasiri

Nakuomba sana utume maoni yako ya dhati.
 
Hivi ni CCM imepanga ratiba yake kwa kufuata ile ya Bunge, au Bunge limepanga ratiba yake kwa kufuata ile ya CCM? Au imetokea kwa bahati mbaya tu?
 
coincident ! hizo ratiba ni fixed, kama kwa mfano kuna fixed date ya siku ya mwisho ya rais kutumikia taifa, ndivyo hivyo hivyo kwa viongozi wa chama !(wana mwisho wa kutumikia chama chao)

so CCM haina uhusiano wowote na bunge wala bunge halina uhusiano wowote na ccm ! vyote ni vyombo viwili tofauti !
 
Kuna mtu alihoji kuhusu kutofautisha matumizi ya mali za umma na mali za chama kipindi hiki! Obviously ni strategy ya ku-mixmax mavituz hapo..! Kikao cha bunge ni opportunity tosha kwa chama tawala kupata mteremko katika gharama za kuendesha mkutano.

kwa Taifa ni hasara kubwa sana kugharamia bunge katika kipindi ambacho wabunge wapo kimwili na si kiakili!
 
sio kweli kabisa hapo ^^, mbona marehemu mama Mbatia alipokumbwa na ajali alikuwa kwenye shughuli zake za kichama, na hakuwa na gari ya serikali !
 
sio kweli kabisa hapo ^^, mbona marehemu mama Mbatia alipokumbwa na ajali alikuwa kwenye shughuli zake za kichama, na hakuwa na gari ya serikali ! so count that out !
 
niliuliza suala na naliuliza tena,
hivi vikao vya kichama vikiwekwa siku za kazi, hawa mawaziri, na marais na wafanyakazi wengine wa serikali huwa wanachukuwa siku zao za likizo kwenda kwenye hiyo mkutano?

na jee ikiwa kuna ulazima wa waziri huyo kubakia ofisini kwake, anaweza kupiga na chini kikao cha chama?

naomba majibu
 
sio kweli kabisa hapo ^^, mbona marehemu mama Mbatia alipokumbwa na ajali alikuwa kwenye shughuli zake za kichama, na hakuwa na gari ya serikali !
Alikuwa na gari ya serikali akataka kuondoka mida mibovu, dereva wake akasita mama akawa mkali. Akomba gari kwa mkuu wa mkoa na dereva mwingine awahi kampeni zake. Aliyopewa akaondoka na ndiyo iliyomuua kwa ajali!!

Dereva wake karudisha gari majuzi kwenye pool.Hizi ni nyeti zilizofichwa na sasa zinaleak.
 
sio kweli kabisa hapo ^^, mbona marehemu mama Mbatia alipokumbwa na ajali alikuwa kwenye shughuli zake za kichama, na hakuwa na gari ya serikali !
Alikuwa na gari ya serikali akataka kuondoka mida mibovu, dereva wake akasita mama akawa mkali. Akomba gari kwa mkuu wa mkoa na dereva mwingine awahi kampeni zake. Aliyopewa akaondoka na ndiyo iliyomuua kwa ajali!!

Dereva wake karudisha gari majuzi kwenye pool.Hizi ni nyeti zilizofichwa na sasa zinaleak.
 
Back
Top Bottom