Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,380
- 39,333
Mkutano mkuu wa CCM unaanza wiki moja toka sasa na yawezekana katika historia ya CCM huo ndio mkutano mkubwa zaidi na wenye kupima mwelekeo wa CCM kwa miaka mingi ijayo. Mkutano Mkuu wa CCM kwa mujibu wa Katiba ya CCM Ibara 105:2 ndiyo Kikao cha Juu kabisa cha CCM na majukumu yake yanaathari kubwa zaidi katika mwelekeo wa sera na siasa wa nchi yetu.
Majukumu ya Mkutano Mkuu ni haya yafuatayo:
Kazi za Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa zitakuwa zifuatazo:-
(1) Kupanga Siasa ya CCM na kusimamia utekelezaji wa shughuli zote za CCM
(2) Kupokea na kufikiria taarifa ya kazi za CCM iliyotolewa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa na kutoa maelekezo ya mipango na utekelezaji wa Siasa ya CCM kwa kipindi kijacho.
(3) Kuthibitisha, kubadili, kukataa au kuvunja uamuzi wowote uliotolewa na kikao chochote cha chini yake au na mkuu yeyote wa CCM.
(4) Kubadili sehemu yoyote ya Katiba ya CCM kwa uamuzi wa theluthi mbili za Wajumbe walio na haki ya kupiga kura kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili kutoka Tanzania Zanzibar.
(5) Unapofika wakati wa uchaguzi, Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa utashughulikia mambo yafuatayo:-
(a) Kuwachagua Mwenyekiti wa CCM na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM.
(b) Kuchagua jina moja la Mwanachama atakayesimama katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
(c) Kuchagua jumla ya Wajumbe themanini na tano kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wa kuingia katika Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kutoka orodha ya Taifa.
(6) Kuunda Kamati za Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa kwa kadri itakavyoonekana inafaa.
(7) Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa waweza kukasimu madaraka yake kwa Halmashauri Kuu ya Taifa kuhusu utekelezaji wa kazi zake kwa kadri itakavyoona inafaa.
Kwa maneno mengine, wakati Kamati Kuu ina uwezo wa kufanya maamuzi fulani (kama kuwasimamisha kazi watendaji, Mkutano Mkuu unaweza kubadili maamuzi hayo) Kuna baadhi ya watu wanaoamini (mimi mmojawapo) kuwa Mkutano Mkuu una nguvu kuliko Bunge na maamuzi yake kwa upande wa CCM yana uwezo wa kubadili kabisa mwelekeo wa kisiasa wa chama na Tanzania.
Ni matarajio yangu kuwa ingawa kikao hiki ni cha Uchaguzi, ninaamini kuwa viongozi wa CCM watatumia nafasi hii pia kufanya maamuzi fulani muhimu kwani alama za nyakati haziko upande wao.
Wakichelewa kuzisoma alama hizo watajikuta kabla ya 2010 wanalazimika kuitisha Mkutano Mkuu usio wa Kawaida. Sijui wenzangu mnamatumaini gani au wasiwasi gani kuhusu wale watakaochaguliwa katika mkutano huu na mada hii itatrack nani anaanguka na nani anaibuka kidedea huko Dodoma!!
Nawatakia wajumbe wote safari njema Dodoma, na kutarajia watafanya zaidi ya kile walichofanya wabunge wao miezi michache iliyopita huko huko Dodoma! Na binafsi naomba kutumia nafasi hii kutoa udhuru kuwa kuanzia kesho sitaonekana sana humu kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano huo Mkuu ambao natarajia kutuma ujumbe maalum.
M. M.