Lango la kuingia nchini linapokosa mtu makini lawama na kudumaa Kwa huduma lazima kuwepo; Kwa kipindi...
Nasema hivi, Sijiuzulu Ng'o.
Hivi wewe katika vitengo vyote vya mamlaka za Serikali umeona hichi changu tu? Binti mbona una nongwa sana wewe?
Niambie ni mamlaka gani iliyoko chini ya Serikali hii ambayo wewe unaona kila kitu kiko perfect mpaka uje uiseme hii ya kwangu? Yaan ushaenda Bandari, TRA, TBS, Ewura, Latra, Sumatra, Tanesco, Dawasco au ATCL, Mifuko ya Jamii, etc ukaona utendaji wao mpaka uje useme eti nijiuzulu?
Na nikijiuzulu nikakosa mshahara nitakula Nini? Utanisaidia kulisha na kusomesha Watoto wangu? Nijiuzulu ili nikose posho na marupurupu ya vikao na Safari mbalimbali ambazo zingine najitungia mimi Mwenyewe?
We unavyoniambia nijiuzulu utanipa wewe VX ya kutembelea? Unaona wivu sana navyoweka kishoka nikiwa naendeshwa kurudisha au kuchukuliwa nyumbani ee? Au utanipa wewe Allowance ya Nyumba ingawa naishi kwangu?
Wewe nani umemuona wa Level ya Mkurugenzi amejiuzulu kwa tumakosa tudogo tudogo kama hutu mpaka uje uniambie Mimi pia nifanye hivyo? Na nikijiuzulu nani ataniita Boss? Au unadhani sipendi sifa za kuitwa Boss? Unadhan sipendi kunyenyekewa?
Unajua hata nimehangaika vipi kupata hichi cheo mpaka uje useme kirahisi tu kua eti nijiuzulu? Usitake nitoe siri zingine za ndani mpaka leo unaniona niko hapa, lakin nakuapia kwa sababu ulizozitoa mimi kujiuzulu hiyo sahau.
Mambo ya hizi taasisi zetu hayaendi kiholela kama unavyodhani. Lazima ufanyike upembuzi yakinifu, iitishwe tenda, apatikane mzabuni, afanyiwe vetting kupitia vikao mbalimbali ambavyo vitahitaji gharama mbalimbali kama vile posho ya kikao, refreshments, ukumbi, etc, ipatikane bajeti ya huo ukarabati n.k. Hivi vyote vinahitaji muda na fedha ili tufanye kwa umakini zaidi.
Sio unakurupuka tu eti nijiuzulu.