MKURUGENZI WA SHERIA CHADEMA: Mrejesho wa shauri la marejeleo Na. 8323/2026 na Kesi ya Msingi ya mgawanyo wa mali na maombi madogo Na. 8960/2025

MKURUGENZI WA SHERIA CHADEMA: Mrejesho wa shauri la marejeleo Na. 8323/2026 na Kesi ya Msingi ya mgawanyo wa mali na maombi madogo Na. 8960/2025

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
3,611
Reaction score
9,269
Mahakama ya Rufaa, iliyoketi jijini Dodoma jana ilipata maelezo kutoka kwa mawakili wa wadawa kuhusiana na marejeo ya shauri la madai Na. 8323/2026 shauri la msingi, pamoja na Maombi madogo namba 8960/2025 maombi ya zuio kwa Chama kufanya shughuli za kisiasa na kutumia mali za chama.

Kuhusiana na kesi ya msingi, Mahakama ya Rufaa ilitaka mawakili kutoa mawasilisho yao kuhusiana na uhalali na usahihi wa mwenendo wa shauri hilo na amri zilizotokana na shauri hilo kuhusiana na mambo yafuatayo:

MOSI: Mahakama ilitaka kusikia kutoka kwa mawakili kuhusiana na hoja ya mamlaka ya mahakama kuu kusikiliza shauri hilo.

PILI
: Mahakama ilitaka kusikia kuhusiana na hoja ya ukomo wa muda,

TATU
: Mahakama ilitaka kusikia kutoka kwa mawakili kuhusiana na lini hasa mgogoro ulianza,

NNE
: Mahakama ya Rufaa pia ilitaka kusikia kutoka kwa mawakili kuhusiana na hoja kama shauri hilo lilikuwa na madai yanayohusiana na uvunjwaji wa haki msingi zilizoko kwenye Katiba ya Tanzania na hivyo kutakiwa kusikilizwa na mahakama ya kikatiba.

Aidha katika shauri namba 8960/2025, ambayo ilikuwa ni Maombi ya zuio, Mahakama ya Rufaa ilitaka kusikia kutoka kwa mawakili kuhusiana na hoja zifuatazo:

MOSI: Utaratibu uliotumika kusikiliza Maombi ya zuio hasa kwenye kipengele cha haki ya kusikilizwa.

PILI
: Mawanda ya amri ya zuio iliyotolewa, kwa kuzingatia;

a) kama amri zilizotokana ziliendana na Amri ya XXXVII Kanuni ya 3 ya sheria ya mwenendo wa madai, sura ya 33, Marejeo ya mwaka 2023.

b) kama amri ya zuio kwa CHADEMA kufanya shughuli za kisiasa iliathiri haki za wanachama kufanya siasa.

Mahakama ya Rufaa ilichukua mwelekeo huo, kutokana na hoja kwamba, marejeo hayo yameitwa na mahakama yenyewe.

Bodi ya wadhamini wa Chama na Katibu Mkuu wa Chama waliwakilishwa na Jopo la mawakili wa Chama, kwa Mapenzi yake Allah, mawakili wametekeleza wajibu wao vizuri sana, nami kama Mkurugenzi wa sheria wa Chama, Nawashukuru na kuwapongeza mawakili wote ambao tumeshirikiana katika hatua zote za maandalizi hadi hatua ya mwisho ya mawasilisho.

Haikuwa kazi rahisi, uthubutu wa mawakili, kujitoa kwao kwa Chama kumefanikisha jambo hili.Pamoja nami, kama mratibu Mkuu wa shughuli za kila siku za kisheria kwenye Chama, Mawakili mwandamizi, Mpale Kaba Mpoki aliongoza jopo letu, pamoja nami Dr Rugemeleza Nshala, Hekima Mwasipu, Dickson Matata na Nashon Nkungu.

Nawashukuru pia mawakili wengine ambao nao walifika mahakama ya Rufaa wakipasha jalamba tusipungukiwe na chochote, hawa ni wakili Alex Massaba, Deogratius Mahinyira, Ruguna na Ikoti Lissu.

Asanteni pia wanachama mkiongozwa na @HecheJohn , Makamu mwenyekiti Bara, Mhe Said Issa Mohamed, Makamu mwenyekiti Zanzibar, Katibu Mkuu wa Chama @jjmnyika , Naibu Katibu Mkuu Bara @amanigolugwa , Mwenyekiti Bawacha Taifa, Sharifa Suleiman, viongozi wa ngazi za chama kutoka mikoa mbalimbali na marafiki wa Demokrasia ambao walifika mahakamani na kutuweka katika Maombi.

Kwa sasa, tunasubiri mahakama ya Rufaa ikamilishe kuandika uamuzi wake, Mungu akipenda tutarejea Dodoma kusikiliza maamuzi ya wazee wa Mahakama ya Rufaa, kama tutakavyo fahamishwa na Msajili wa Mahakama.
 
Mwamba huyu hapa!
Screenshot_20260224-131356~2.png
 
Hapa hakukua na kesi ni mbinu za kupoteza muda na kutaka kuizuia CHADEMA isifanye shughuli zake ila bado watashindwa vibaya hao CCM na vidampa wao.
 
Jaji Hamidu Mwanga ametumika kipumbavu sana kuihujumu Chadema ili kuinusuru CCM, kusema kweli ameidhalilisha Mahakama kiasi kikubwa huyu alitakiwa arudishwe akawe hakimu wa Mahakama ya Mwanzo .
 
Jaji Hamidu Mwanga ametumika kipumbavu sana kuihujumu Chadema ili kuinusuru CCM, kusema kweli ameidhalilisha Mahakama kiasi kikubwa huyu alitakiwa arudishwe akawe hakimu wa Mahakama ya Mwanzo .
Kwa taarifa yako Mahakimu Mahakama za Mwanzo ni very bright Kwa sasa kuliko wakati wowote do isiwachukulie poa.
 
Na nilichojifunza kingine ni hiki:

Kumbe wale mawakili wa Said Issa Mohammed ni weupe hawana lolote, wanabebwa na mfumo tu ambao umekita mizizi mpaka huko mahakamani ukiwatumia mahakimu na majaji kama Hamidu Mwanga kujitoa ufahamu na kufanya maamuzi ya kijinga
 
Back
Top Bottom