Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke aache kutisha na kufedhehesha Waandishi wa Habari

Hiki ni kiburi wanachokipata kutoka kwa bwana yule. Like father like son!

Hakuna wa kumuwajibisha kwasababu maji hufuata mkondo!
 
Backup gani bhana, kama hawezi kufanya kazi za wananchi na wananchi arudi nyumbani kwake akakurugenzi familia yake. Wanaotafuta kazi na wenye sifa za kuwa wakurugenzi wako wengi
 

Hapa sasa ndio umeongea ukweli uliposema jamaa ni mropokaji, hapaswi kuropoka hovyo
 
hapa sasa ndio umeongea ukweli uliposema jamaa ni mropokaji, hapaswi kuropoka hovyo
Yaap Ni hulka yake hiyo kuibadil Ni ngumu sana sema aangalie na mazingira .

Ila huyo mwamba Ni muongeaj sana
 
Yaani kwamba mtu akijenga jumba zuri mkoani ndio anakuwa hana njaa? Au mimi sijaelewa
 
Boss wao aliwahi kuombwa lami enzi hizo huko jimboni kwake akawaambia wananchi kunyeni mavi yakishakauka yatageuka kua lami.

Kwahio sishangai sana majibu ya hawa manyokaa wake.
 
Wenye pesa zao labda
 
MKURUGENZI WA MANISPAA YA TEMEKE AACHE KUTISHA NA KUFEDHEHESHA WAANDISHI WA HABARI!

Tarehe 2 Desemba 2020, ITV ilikuwa na taarifa kuhusu kero ya wananchi katika Manispaa ya Temeke. Mkurugenzi wa Manispaa ambaye ni Mteule wa Rais anapigiwa simu na mwandishi wa habari wa ITV kutaka ufafanuzi kuhusu jambo muhimu la kijamii lenye masilahi kwa taifa.

Badala ya kujibu au kutoa ushirikiano kwa mwandishi wa habari, yeye anaamua kumfokea mwandishi wa habari kwa kumwambia kuwa, yeye (Mkurugenzi) siyo saizi yake (mwandishi wa Habari), hivyo aliyetakiwa kumpigia simu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke ni Mkurugenzi [wa ITV?] na wala siyo mwandishi yule wa habari.

Your browser is not able to display this video.

Vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari katika nchi hii wasipozinduka watakuwa wanakaripiwa na kila Mtendaji wa Serikali. Uhuru wa Vyombo vya Habari katika nchi hii umewekwa mfukoni mwa Serikali na hili la Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kumfokea mwandishi wa Habari wa ITV ni kielelezo kimojawapo!

Tunamuonya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, ndugu Lusubilo Mwakabibi, kuacha tabia ya kuwafokea, kuwadharau na kuwatisha waandishi wa habari. Anahitaji kuwa mnyenyekevu kwa kuwa anakalia ofisi ya umma inayoendeshwa kwa kodi za Watanzania! Kama tuliwahi kuwakemea na kuwaonya wengine, ni wajibu wetu kumkemea na kumuonya na yeye pia! Tunaomba rehema kwake ili atambue kuwa alilofanya halikuwa jema machoni pa Watanzania.

Tunaishauri Serikali isianze kumfuatilia Mwandishi wa ITV aliyeripoti tukio lile na wala ITV isifuatiliwe kwa kurusha hewani tukio lile. Badala yake Serikali ijikite katika kuwaonya na kuwaelekeza watendaji wake kujirekebisha. Tunamshauri pia Mwakabibi asianze kumfuatilia mwandishi, bali ikiwezekana amuombe msamaha mwandishi yule na ITV yenyewe kwa kumnyanyasa mwandishi wake!

Tunatimiza wajibu wetu wa kikuhani kwa Serikali na jamii kwa ujumla (Ezekieli 33:1-20)!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
 
Mwakabibi kuwa DED na kwa vile alishiriki kuiba kura Kakonko basi anajiona mungu mtu , nimemdharau sana ! Hivyo vijimadaraka alivyonavyo ni dhamana ya muda mfupi sana .
 
Amefanya kama wakubwa zake, hakuna jipya.
 
wewe DED cha ulimbukeni, leo upo kesho utaacha hiyo ofisi
 
Mzee unamsifia mwanaume mwenzako hata chawa hafikii huko, usizoee sana wanaume tunaweza waza mengine. Labda kama una jinsia ya kike. Mwambie jamaa usilete utani kazini wamedondoshwa hadi mawaziri wakuu. Kitengo ni nani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…