Bandari ya Mtwara kwa sasa ina uwezo wa kuhudumia Zaidi ya Tani 1,000,000 kwa Mwaka

DodomaTZ

Member
May 20, 2022
71
107
Screenshot 2024-02-13 164937.png
Bandari ya Mtwara ni miongoni mwa bandari kuu tatu zinazosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) iliyopo Kusini mwa Tanzania karibu na mpaka na Msumbiji.

Kijiografia inapatikana kilomita 578 Kusini mwa Jiji la Dar es Salaam. Bandari ya Mtwara ambayo ina kina kirefu ilijengwa kati ya mwaka 1948 na 1954. Ujenzi wa awali na uendelezaji wa bandari hiyo uliendana na ujenzi wa reli kuanzia Mtwara hadi Nachingwea.

Ofisi ya Meneja wa Bandari – Mtwara Tanzania imeeleza kuwa mazingira ya Bandari ya Mtwara yana nafasi ya kuwa bora zaidi upande wa huduma kutokana n maboresho ambayo yanafanyika hapo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Gati ya Zamani (Old Barth) ambayo ilijengwa wakati wa Ukoloni, ina urefu wa Mita 385 kutoka mwanzo hadi mwisho, ilipojenga wahusika wa wakati huo walisema itachukua Meli tatu zisizozidi Mita 185 kila moja lakini kutokana na ukuaji wa Teknolojia, bandari hiyo inao uwezo wa kuingiza mpaka Meli zenye urefu zaidi ya Mita 220.

Kutokana na maboresho yaliyofanyika katika Bandari ya Mtwara ya ujenzi wa gati moja la nyongeza lenye kina cha mita 13 (chart datum) na urefu wa mita 300, Bandari ya Mtwara kwa sasa ina uwezo wa kuhudumia Zaidi ya tani 1,000,000 kwa mwaka.

Taarifa inaeleza kuwa Watu wa Mtwara tunajivunia kuwa na miongoni mwa Bandari zenye kina kirefu Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

1.png

Meli zilizohudumiwa katika Bandari ya Mtwara kwa Kipindi cha 2018/2019 hadi 2023/2024 (Julai 2023 hadi Januari, 2024).

Gati ya Zamani
Kina cha mita 9.5 (CD) , urefu wa mita 385 na uwezo wa kuhudumia hadi tani 45,000DWT.

Gati Jipya
Kina cha mita 13.0 (CD) , urefu wa mita 300 na uwezo wa kuhudumia hadi tani 65,000DWT. Ujenzi wake uligharimu Shilingi Bilioni 157.8

Yadi katika Gati la Zamani
Yadi 3 zenye ukubwa wa mita za mraba 38,000 na uwezo wa kuhifadhi makasha 4,350 (TEUs) kwa wakati mmoja.
Screenshot 2024-02-13 165206.png
Yadi katika Gati Jipya
Yadi yenye ukubwa wa mita za mraba 75,807, uwezo wa kuhifadhi makasha 8,600 TEUs kwa wakati mmoja.
2.png

3.png

SCANNER
Scanner moja ambayo inaweza ‘scan’’ hadi makasha 30 kwa saa.

SSG
TPA imepokea “crane” ya kisasa iitwayo “Ship to Shore Gantry Crane (SSG)”, mtambo huu umeshasimikwa katika bandari ya Mtwara na wenye uwezo wa kuhudumia makasha 25 (TEUs) kwa saa.

Maghala
Bandari ina maghala mawili ya kuhifadhia mizigo (Zambia Shed na Shed No. 3) yenye ukubwa wa mita za mraba 12,500 na uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tani 18,000 za mizigo kwa wakati mmoja.

Fursa zilizopo
Kilimo cha mazao mbalimbali yanayozalishwa katika Mkoa wa Mtwara na Mikoa ya jirani ya Lindi na Ruvuma.

Shughuli za utafutaji wa Mafuta/Gesi, uzalishaji wa Gesi Asilia na bidhaa zitokanazo na Gesi.

Ujenzi wa miradi ya miundombinu na viwanda inayotarajiwa katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Uwepo wa bidhaa za madini na viwanda mbalimbali katika Ukanda wa Maendeleo wa Mtwara (Mtwara Development Corridor) na nchi jirani za Msumbiji, Malawi na Zambia.

Changamoto katika Bandari ya Mtwara
Ukosefu wa miundombinu ya usafirishaji wa ardhini kama Reli ambayo ingekuwa ni kiunganisha kutoka maeneo ya uzalishaji kama migodini (Mbamba bay, Mchuchuma na Liganga).

Ukosefu wa meli za mwambao za uhakika ambazo zingesadia kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka Mtwara kwenda Tanga na Dar es Salaam na nchi jirani ya Comoro.
 
View attachment 2902902

Hii umedadavua vema sana. Kiukweli kuna hatua kubwa imepigwa. Sasa ni muda wa kuongeza ushawishi ili wafanyabiashara waitumie hata kushushia magari yaendayo Zambia, Malawi na hata Congo
 
Back
Top Bottom