Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 877
- 4,105
Naambiwa mkurugezi wa mwendo kasi akijumuisha salary, posho, safari na usafiri kwa mwezi mmoja anatumia zaidi ya milioni kumi za wananchi.
Lakini pamoja na kulipwa fedha zote hizo bado hakuna siku amewahi kuonekana katika eneo la Mradi ambalo ni pungufu ya urefu wa kilomita 40. Yupo ofisini anasoma mafaili na kuidhinisha matumizi ya fedha.
Kwa ubosi alionao hata waziri anasubiri. Sambamba na kulipwa fedha zote hizo hataki anaamini Mradi wa Mwendokasi kubinafsishwa kwa mzawa hawataweza kuuendesha labda aletwe mchina au mzungu. Unajiuliza anafanya nini ofisini? Temekosa watu wakuwapa hii kazi?
Leo watanzania wanafanya biashara ya usafiri wa mabasi na hakuna kelele, watashindwa kusimamia Mwendokasi ambayo abiria wanasubiri masaa 2 hadi matatu kwa trip?
Mwendokasi ni jambo la kumuumiza kiongozi wa nchi kichwa? Mwoneni mama huruma ; acheni kumhujumu Mhe. Rais . Tokeni ofisini mkafanyr kazi aliyowatuma.