Mkurugenzi JamiiForums: CCM imewekeza fedha nyingi sana mitandao ya kijamii kuliko UKAWA

Msulibasi

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
5,836
7,492
Akihojiwa na Azam Two ameulizwa anaonaje matumizi ya mitandao ya kijamii katika kampeni-amejibu JamiiForums, Facebook, Instagram hata Twitter vimetumika sana.

Kisha akaulizwa: Unaonaje kati ya wagombea na vyama, kipi kimecover sana mitandao?

Akatoa jibu la moja kwa moja: Mwanzo CHADEMA walitawala sana lakini kwa sasa CCM wamewekeza fedha nyingi sana.


 
Last edited by a moderator:
Sidhani kama UKAWA walikuwa na haja ya kuwekeza sana kwenye mitandao ya kijamii maana huku mtaani kijana kwa mapenzi yake mwenyewe yupo radhi kununua bando kwa ajili ya kuitetea CDM tofauti na CCM bila pesa hakuna wa kupoteza muda.
 
Sidhani kama UKAWA walikuwa na haja ya kuwekeza sana kwenye mitandao ya kijamii maana huku mtaani kijana kwa mapenzi yake mwenyewe yupo radhi kununua bando kwa ajili ya kuitetea CDM tofauti na CCM bila pesa hakuna wa kupoteza muda.

Wataka mabadiliko tunapambana na wala mamilioni ya mafisiem..na tunawatoa kwa TKO..uzuri ni kwamba. Ccm hawajui hao jamaa walowanunua wanakomaa mitandaoni lkn kura ni ukawa!

utashangaa nikikwambia hata wale wasanii njaa wakata mauno majukwaani kula ccm kura ukawa hata makada maarufu wapo ccm kimwili tu kura ukawa!bila ya kuiba kura mwaka huu their up for total surprise!and that's for sure!
 
Ninachowapenda watu wa UKAWA humu kwenye mtandao.
1/Wanajitolea wenyewe(Hakuna anayewalipa chochote)
2/Hawafahamiani kiuhalisia(Wamekutana tu humu mtandaoni na kuunganisha Fikra)
3/Hawajulikani popote na viongozi wa UKAWA.
4/Wanaandika zaidi vitu vya ukweli na Upeo.
 
Back
Top Bottom