Nafikiri useme mpinzani wa Kilimanjaro kwa maendeleo vijijini ni Kagera.
BTW mnacholaumu hata sisi tuna lawama zetu, kama sio Nyerere na TANU yake kupandikiza mamluki na kuibia KNCU maendeleo uchagani yangekuwa kama ulaya.
Hizo barabara, shule, hospital, umeme vyote ilikuwa kazi ya KNCU. Umeme ulikuwa unazalishiwa nyumba ya Mungu ulitosha kabisa kwa Mkoa mzima wa Kilimanjaro, Financer alikuw KNCU. Miundombinu ya Maji ilitengenezwa na KNCU na maji yalikuwa bure hayalipiwi hata sumni (kuna baadhi ya maeneo yalihadaika na janja ya CCM wakakubali kuboreshewa ile miundombinu mwishowe wanaambiwa walipie, Mimi kijijini kwetu walipinga na mpaka leo kijiji chetu na sehemu kubwa ya Machame maji ni bure)
Kwenye elimu KNCU achilia kujenga shule na kugharamia ada na chakula ilijitolea kusomesha best students mpaka level ya masters kwenye vyuo vikuu vya nje. Mmoja wa beneficiaries ni Edwin Mtei, Basil Mramba, Nsilo Swai (Treasurer TANU na Waziri wa Biashara na Uchumi), Eliufoo (huyo alikuwa waziri wa kwanza wa Elimu Tanganyika) na wengine wengi ambao baadae walitumia na serikali kama wataalam na wakufunzi..
Kwenye Afya pia walijenga hospital zenye hadhi kwenye wilaya zote ambapo hospitali hizohizo leo hii ndizo hospital za rufaa za wilaya.
Kwenye miundombinu walijenga barabara na madaraja sehemu mbalimbali za vijijini na mjini. Na mengi ya madaraja hayo mpaka leo yapo na utayaona tu ni madaraja ya zamani.
Kwa kufanya hayo yote TANU ikaona KNCU ni threat kwake sababu hakuna mwananchi Uchaggani alikuwa anaililia serikali kwa chochote, na wimbi la wasomi wengi ambao wanasomeshwa elimu za juu kabisa mpaka Ulaya ikawaletea shida na hofu. Hapo ndio wazo la kuiua KNCU likajongea, na kweli walifanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Kuanzia hapo wachaga hawakukata tamaa, wakarudi kwenye nyumba za Ibada kuendeleza jumuiya zao. Leo hii mnakokuita kuhesabiwa ndiko kunatatua mambo madogo madogo ya kule vijijini kama kurekebisha barabara, kujenga au kuongeza vifaa zahanati za vijijini, kurekebisha shule, kusaidia miradi mbalimbali ya vijana na mengine mengi mengi..
Ila kama sio kuiua KNCU kule tungekuwa tunafanana na Ulaya kabisa..
Sent using
Jamii Forums mobile app