Mkenya 'Kihiyo' aongoza shule ya kimataifa Dar es Salaam

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,415
2,000
Raia wa Kenya asiyekuwa na sifa za ualimu ameajiriwa kuwa Mkuu wa Shule za Kimataifa za St. Columba's jijini Dar es salaam Jamhuri limebaini

Shule hizo zinazomilikiwa na Kanisa la Presbyterian Church of East Africa, lenye Makao Makuu nchini kenya, ziko Upanga na Makongo jijini humu

Serikali ya awamu ya tano pamoja na mambo mengine, imevalia njuga uboreshaji wa Elimu, ikiwa pamoja na kufanya uhakiki wa walimu, jambo ambalo, ama halijatelekezwa, au linafunikwa katika shule za St. Columba's

Uchunguzi uliofanywa na Jamhuri umebaini Mkuu wa Shule hizo zinazotoa elimu ya msingi kwa lugha ya Kingereza, David Wathiga, hana elimu wala sifa za kushika wadhifa huo

Ni kwasababu hiyo, imebainika kuwa alishawahi kufukuzwa asifanye kazi hiyo, lakini akarudi kinyemela kwa msaada wa maafisa wa Idara ya Uhamiaji na wenzao wa Idara ya Kazi wanaohusika na ajira nchini.

"Huyu alikuwa Mwalimu wa kawaida katika Kampasi ya Makongo mwaka 2011, kabla ya kufukuzwa kutokana na uwezo mdogo wa kufundisha masomo ya Sayansi na Hisabati, kila mmoja anashangaa ni vigezo gani vilitumika kumrudisha na kumpa wadhifa wa juu kabisa" kimesema chanzo cha habari

Wakati anatimuliwa, Meneja wa Shule katika Kampasi ya Makongo alikuwa Steven Kabumba, na Katibu wa Bodi ya Shule akiwa ni Vida Mwasalla

Kabla ya kuachishwa, uongozi wa shule ulimtaarifu kwa maandishi kuwa usingeweza kumtafutia kibali kingine cha kuendelea kufanya kazi nchini baada ya kubaini hana uwezo wa kufundisha

Mbali na kuwa na kiwango cha chini katika utendaji, imebainika kuwa Wathiga alisoma katika Chuo cha City & Guilds nchini Kenya ambacho mitihani yake haitambuliwi na Baraza la Mitihani nchini humo (KNEC) chuo hicho kimekuwa hakitambuliwi kitaaluma mahala popote.

Kwa mujibu wa vyeti ambavyo navyo vinavyodaiwa kuwa ni vya kughushi, Wathiga ana Diploma ya Elimu ya Kiroho (Theological Education by Extension)

Chanzo: Gazeti Jamhuri
 
From Sir With Love

JF-Expert Member
Sep 13, 2010
1,934
2,000
Mleta mada, unaonekana una hasira sana baada ya kufukuzwa kazi hapo shuleni kwa sababu ya kula ada bila kupeleka ofisini.

St. Columba's ilikuwa ni shule bora za English medium, japo kwa sasa imedoda kwa sababu ya watu kama nyie.

Shule ni ya kanisa, lakini mlikuwa mnachukua rushwa kusajili watoto.

Mlikuwa mnachukua ada kutoka kwa wazazi kama cash na kuzila badala ya kumwambia mzazi apeleke bank. Mbaya zaidi mlikuwa mnatoa risiti fake.

Juzi tu wala rushwa wote wamefukuzwa kazi hapo shuleni, sasa mnalialia kwenye mtandao.

Maisha ni sehemu yoyote ile sio lazima hapo shuleni.

Binadamu bwana.
 
Unachanganya mada... hakuna mambo ya ada katika hii thread

inadaiwa hana sifa anabebwa na wakuu wake huyo 'Kihiyo'
 
Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
46,339

LABDA KUONGEZEA AMENUNUA MAGARI SABA DOUBLE COASTER HAYA MAGARI YANAFANYA KAZI ZA SHULE JIONI YANA BEBA ABIRIA BILA KIBALI PALE MAWASILIANO NA YANAPOSIMAMISHWA HUTOA KIDOGODOGO NA KUENDELEA NA SAFARI

HILOO DOGO MAGARII HAYA HUSIMAMA PALE MWANZO WA DARAJA KUANZIA SAA TATU USIKU YAKIWA NANEMBO YA HILO KANISA KABISA PESB... NA HULIPISHA WANANCHI 1000 KUFIKA TEGETA NAOMBA NIWAWEKE WAZI SIHIOO TU WAPO JAMAA WANAJIITA KILIMANI SEC SCHOOL
SERIKALI IMESEMA MIHULA MITATU WAO WAMEWEKA MINNE WANALIPISHA LAKWANZA MILION MOJA NA LAKI TISA IHANITHI MTUPU NA HAWA NIWAKENYA

MABASIYAO JIONI YANAENDA NJIA YA YA UNUNIIOOO.. NAMENGINE USIKU HIKAA PALE MWENGE SHIDAMOJA KUBWA WANAKULA SERKLI ZA MITAA NA HATA UKIENDA POLISI KULLAMIKA KAMA WANAJUA HILO TATIZO NSHIDAKUBWA.....

RELX N ENJOY
 
From Sir With Love

JF-Expert Member
Sep 13, 2010
1,934
2,000
Unachanganya mada... hakuna mambo ya ada katika hii thread

inadaiwa hana sifa anabebwa na wakuu wake huyo 'Kihiyo'
Mkuu mada imefichwa na neno kihiyo.

Najua kinachoendelea pale.

Siku za nyuma waalimu ambao walikuwa wanakula rushwa ili mtoto akubaliwe, ndiyo hao hao walikuwa wanaweka kambi immigration ili waalimu wenzao ambao wanakemea hayo wanayofanya wakamatwe ili waendelee kula rushwa.

Hao hao viongozi waalimu ambao ni wazalendo walikuwa hawampi binti kazi ya ualimu mpaka walale nae. Na hata ukiajiriwa watakuambia utoe mapenzi kabla hawajakufukuzisha.

Shule ni ya kanisa lakini imejaa visasi badala ya kufundisha watoto.

Mwalimu David, amekomaa mpaka magendo yote yameisha pale, na wabaya wote wameondolewa ndiyo maana hao waalimu wanakomaa naye.
 
Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
8,232
2,000
Mleta mada, unaonekana una hasira sana baada ya kufukuzwa kazi hapo shuleni kwa sababu ya kula ada bila kupeleka ofisini.

St. Columba's ilikuwa ni shule bora za English medium, japo kwa sasa imedoda kwa sababu ya watu kama nyie.

Shule ni ya kanisa, lakini mlikuwa mnachukua rushwa kusajili watoto.

Mlikuwa mnachukua ada kutoka kwa wazazi kama cash na kuzila badala ya kumwambia mzazi apeleke bank. Mbaya zaidi mlikuwa mnatoa risiti fake.

Juzi tu wala rushwa wote wamefukuzwa kazi hapo shuleni, sasa mnalialia kwenye mtandao.

Maisha ni sehemu yoyote ile sio lazima hapo shuleni.

Binadamu bwana.
Hata mimi niliona taarifa imekaa kimajungu zaidi, Watanzania tunapenda sana vitu vya mteremko hata kama uwezo hatuna tunakimbilia kufitini Wakenya sijui kwa nini? Jalini kazi zenu kwanza halafu na hii tabia za kuwaibia waajili wenu bila huruma nayo inachangia kutoaminiwa.
 
From Sir With Love

JF-Expert Member
Sep 13, 2010
1,934
2,000
Mnataka kusema mleta mada ni Singaile aliyekuwa mtaaluma pale na amefukuzwa??
Tena huyo sasa hivi anakesha immigration ili David aliyejitoa mhanga kumuumbua asirudi tena shuleni.

Wewe darasa linatakiwa wanafunzi 25 mpaka 30, mtu anapokea rushwa anaingiza wanafunzi 50 tena watoto wadogo, baby. Waalimu wenyewe darasani ni wawili. Huo si wazima

Kabla ya kuja st. Columba's ulikuwa unafanya kazi wapi mpaka uone maisha yako ni hapo tu?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom