Mke wangu ni mgumu sana kujishusha

Mke wangu ni mgumu sana kujishusha

Wakuu nawasalimu kwa jina la muungano.

Niende moja kwa moja kwenye mada kuu, nimekua kwenye ndoa na huyu mke wangu yapata miaka nane sasa, tulioana wote tukiwa vijana na ni binti ambae tulisoma nae kuanzia primary tukaja kukutana chuo, kwahiyo namfahamu vizuri tu. Nikiri tu kwenye mambo mengine ya kifamilia yupo vizuri sana, ila tatizo linaanza ni kujishusha na kuomba msamaha pale tunapotibuana.

Hii hali inanikwaza sana sababu bila kujishusha mimi tunaeza kukaa hadi mwezi hatuongei eti ameninunia. Mara nyingi huwa inanilazimu mimi kujishusha baada ya kubanwa na upwiru sana. Kwa ninavofahamu kupishana kauli kwenye ndoa kupo na ni jukumu la wanandoa wote kuipambania ndoa kwa kujishusha na kuyaongea, ila mwanamke ndio anatakiwa awe mstari wa mbele kujishusha ili mambo yaende, ila kwa huyu mke wangu imekua tofauti.

Kwa sasa tuna watoto watatu ila hii hali inanifanya nihisi kama nalazimisha mapenzi hivi hadi nimeanza kupata mawazo ya kuivunja hii ndoa. Nakwazika sana.

Naombeni ushauri wenu wakuu.
Kwa kuwa umemjua vema,,,, ni rahisi kuishi nae, hakuna best zaidi yake huko outside, unajidanganya kuvunja ndoa eti kwasababu mke hajui kujishusha, kuna misingi uliikosea mwanzoni ndo imemjengea mazoea 😇
 
Kuna watu kuomba msamaha hawawezi ila watafanya jambo kuonyesha wamejutia kosa. Kama mkeo ni wa aina hiyo na sio malaya wala mchawi Relax tulia kwenye ndoa ila kama unaona huwezi achana nae wenye UTI na ghono wapo wengi tu mtaani, nenda wakuchune.

Ni kweli, kuna watu wa aina hiyo . Utaona anajirekebisha lakin kusema hilo neno hawez
 
1. Chukulia kwamba huo ni ugonjwa wake.

2. Kama hauna mazara sana na ni kiburi cha uanaume, we shula tu.

3. Mwenye akili ndo anaitunza ndoa, kwa hiyo itunze.

Angalizo:

Kama kweli kuna jambo la muhimu sana kakosea, halafu hataki kukubali, Nakushauri kaza mpaka mwisho, atashuka tu.

Kuna kitu kinaitwa break point, yakwako ipo karibu, iongeze tu izidi yake, ikishazidi atashuka tu, akikuwoma hiyo tabia atakutesa sana.

Kaka umechapia umesema Shula tu badala ya shuka tula. Unatuchanganya sie wapare Shula tu maana yake Jamba tu[emoji23][emoji23]
 
"Huezi kumuhukumu mtu bila kumsikia", tungemsikia na yeye tungejua tuseme nini juu za ndoa ako...
 
Kama sio mnyakyusa huyo ni mchaga.
Wanawake wa kinyakyusa ni watata sana
📌📌📌📌📌📌📌📌

Huwa hawataki ujinga ujinga. Yaani ni bandika bandua kampa kampa kama huna kifua utakimbia au utapata presha ni ego tu kwa kwenda mbele. Ku-deal nao sawasawa ni lazima kujitoa ufahamu na wewe uwe mtu usiyejali vinginevyo presha ya kupanda inakuhusu 😁😁😁
 
Wakati mpo katika mapenzi na uchumba alikuwa anajishusha kukiwa na mzozo? Au umemfikisha kwenye ndoa ndiyo ukinyonga wake ukamuisha? Au uliziona alama za tahadhari ukakaza fuvu kutokana na utamu wa mbususu uliyokuwa unapewa kwa kuibia ibia? 😁😁😁
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom