Mke wangu kisirani, anakataa unyumba. Msaada tafadhali

duuuh i am speechless, nnaposoma makala kama hizi uwa nawaza mara mbilimbili kuhusu kuoa, sipendi kelele ndani ya nyumba, mwanamke kanuna hujui sababu wala hasemi, hakupi unyumba, ukichepuka pembeni ndo ivyo tena yani ni vululuvululu....itanichukua muda sana mpaka nikate shauri la kuoa
 
hao wapwani wanaolewa ili kutoa nuksi, mleta mada yuyo mwanamke atakusumbua na kwa tabia za kizenji mmmmh achana nae.....au la kama nilivyokwambia oa mke wa pili mpe kazi ya kusimamia miradi.....akili itamkaa sawa tu.....
 
ndo maana walisema ndoa ndio maisha yako yote yalipo, tusiwe tunaiona tabia ya m2 mapema then tuna assume itaja isha, tabia ya leo ndo hyo hyo jana na hata kesho...plz najua ulimpenda but u have to sacrify utafute mwingne
 
Ningepewa nafasi ya kurudi kwenye ujana wangu na kuchagua mwenza basi huyo angekuwa chaguo langu la kwanza!
 
Pagumu sana hapo;ukimuacha baada muda mfupi atarudi mbio na kusema ameshatibiwa na amepona!njaa sio mchezo au utashangaa ataolewa na mtu wa kawaida kabisa anayejua kuyapunga hayo majini mahaba yao!kazi unayo kaka pole sana!swali la kizushi hiyo virgin ulikuta kote ?maana nasikia huwa wanatunza sana upande mmoja na mwingine u wazi!sasa kama wewe si mtenda kazi zote inakuwashida kidogo!mtazamo tu!
 
Pagumu sana hapo;ukimuacha baada muda mfupi atarudi mbio na kusema ameshatibiwa na amepona!njaa sio mchezo au utashangaa ataolewa na mtu wa kawaida kabisa anayejua kuyapunga hayo majini mahaba yao!kazi unayo kaka pole sana!swali la kizushi hiyo virgin ulikuta kote ?maana nasikia huwa wanatunza sana upande mmoja na mwingine u wazi!sasa kama wewe si mtenda kazi zote inakuwashida kidogo!mtazamo tu!

Mkuu Skills4ever sina hakika na hiyo ya upande mwingine, sijawahi kuifanyia kazi, namuomba MUNGU isintokee tho mh...!!! Any way ts a home work mkuu ntaidadisi zaid...thanx kwa nyongeza ya pekee
 
Kama hakuna tendo la ndoa hapo hakuna ndoa, kuliko kuendelea kuumia mpe taraka yake aende kwao, tafuta mke mwingine ukizingatia wewe mwenyewe unasema mapenzi yamepungua kwake, muache aende zake Mungu atakupa mke mwingine. Pole
 
hilo ni wazi mno
mkeo 'hakupendi wala hajawahi kukuipenda'

wazanzibari nawajua
wanachukulia 'kuolewa' kama 'baraka' ambayo haikataliwi

so mtu anajilazimisha kuolewa hata kama hayuko 'in love' na mwenzie

so wa kwako 'kaolewa' na wewe kama 'sheria' tu
kiukweli hajawahi kukupenda kabisa

majini mahaba visingizio tu

Huku kwetu tunaita kusafisha nyota...ili mambo yaende The Boss.
 
pole bhana kuba! hapo wizi mtupu, hakuna Jini Mahaba wala Jina Chuki hapo!
huyo anashida zake tu, ukiona hivo malengo yake ya kuingia kwenye hiyo ndoa haijatimia na amegundua wewe si mtu wa kushikwa masikio!
chapa nje "LIWALO NA LIWE (Mizengo K. Pinda, 2012)"! wa hivo wengi sana, otherwise mruhusu akuweke kiganjani!
 
kwa mtindo huu ile formula ya hit and run itaonekana sana...SIO SIRI UMENTISHA NA KWA MTINDO HUU KUOA NI NDOTO AOTAYO MTU AKIWA ANATEMBEA TENA MCHANA!!!! ee mungu tusaidie!!!!
 
dah! Pole sana kaka...ndo maana me bado niponipo kidogo..wake wa kuoa hawaeleweki kabisa...

We tafuta mrembo oa mwenzio anasumbuliwa na tatizo la Muungano.Wazanzibar wote wamegoma hawataki muungano so hata binti nae anauvua muungano taratibu.
 
Wakuu
Nilimuoa April 2011. Kabla ya hapo tulikuwa na uhusiano kama mwaka m1.. alikuwa ni virgin na hakutaka kushiriki tendo la ndoa hadi tulipooana, ni mzanzibar ana maadili ya dini kiasi. Kwao kawaida, baba ni mstaafu wa jeshi na mama ni mama wa nymbani, anjishughulisha na biashara ndogondogo za vitafunwa!
Tatizo lake kubwa ni kuwa hapendi kukosolewa anapokosea, na neno sorry kwake ni kama amejidhalilisha.
Kuna kipindi aliacha kazi alikoajiriwa akidai wakorofi, nilimfungulia biashara ya internet cafe, ilinicost zaid ya 13million! Yeye ndo alikuwa msimamizi lakini haikupita mwezi akawa hasimamii na wakati mwngine hafiki kabisa net, nilipomuuliza ndo ikawa mwisho kujihusisha nayo akisema nataka kumnyanyasa kwa ako kanet tu, alisusa na kuniambia hatajihusisha na mali yangu yoyote hata baada ya kumbembeleza!
Kuna pesa pia nilimkopesha kaka yake kipindi cha maandalizi ya ndoa yetu, alipopewa anirudishie alizitumia bila kuniarifu. Nilipomuuliza akasema najifanya kidume nataka kumcontrol kila kitu, yy hatakubali. Nilitamani kusimamisha ndoa! Hata hivyo nilijipa moyo huenda atajirekebisha.
Baada ya ndoa, aliendelea kuwa mama wa nyumbani na baada ya mwezi alishika ujauzito! Vituko vilizid na kama kawaida hakutaka kuambiwa kakosea, nilichukulia ni hali ya ujauzito, niliignore!
Bahat ofsini niliteuliwa kozi fupi ya miezi 6 nje ya nchi, alirud kwao Zenj. Niliporudi alikuwa na ujauzito mkubwa so niliamua kumuacha kwao had alipojifungua.
Baada ya miez miwili nilimfuata.
Lakini nilikuja kuanza kushangaa alipokuwa hataki kushiri nami tendo la ndoa kwa madai kachoka. Ikapita miezi miwili mingine hivohivo! Nilivumilia. Sasa ni zaid ya miez 6 hataki ingawa amekuwa akishauriwa sana na mamaake na ndugu zake wengine!
Nikizungumza nae hudai hana tatizo lolote kibaya zaid anakasirika ukiendelea kumdadisi na ananuna!
Kuna siku baada ya kumbana sana na kumtishia kumrudisha kwao alinambia niongee na dadaake kama nataka kujua kinachomsibu.
Dadaake alinambia kuwa alipokuwa Zenj aliwahi kumwambia kuwa anaponiona tu anahisi hasira na ananichukia tu bila sababu,pia et walienda kwa mganga wa kienyeji ikaonekana ana jini mahaba na hata yeye dada mtu analo ingawa ye mumewe hamnyimi anajitahid kupambana nalo na amekuwa akimshauri mdogo wake bila mafanikio.
Imefikia hatua napachukia nyumbani na hata mtoto sina raha naye coz wakat mungine akiniona nacheza nae huja kumchukua.
Najitahid kumletea vijizawad, lakini ni kawaida kukuta ulichomletea hapohapo hata cku mbili hajakigusa, neno asante kwake hakuna mpaka najistukia may b hapend vitu nnavomletea.
Zaid hapend kabisa kuzungumzia maswala yetu, nimemshauri sana aongee bila mafanikio.
Haonekani kujirekebisha na amewahi kudai talaka nilipomtishia kumpiga siku 1 akidai hajawahi hata kupigwa kibao kwao, kama nimemchoka nimwache!

Wakuu,
nafikiria nimuache lakini namfikiria pia mtoto atapata taabu kwa kukosa malezi ya baba na mama.
Mapenzi yangu kwake yamepungua kwa kweli coz hakuna ule ukaribu wa mume na mke!
NAOMBENI MSAADA WAKUU

Kwa kweli na umahiri wangu wa kusimamia ndoa but hii ni ngumu kwa kuwa kukosana kwenyewe ni vitu childish sana. Ila tu hii ndoa itakuwa ngumu sana kwa huyu mleta mada. Hebu pia shirikisha viongozi wa dini ili aombewe maana kama ni mapepo yaondoke. Bila maombi hapa mtaishia kuwa na mahawara tu. Pole sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom