Mke wangu kisirani, anakataa unyumba. Msaada tafadhali

Jun 19, 2012
21
9
Wakuu,

Nilimuoa April 2011. Kabla ya hapo tulikuwa na uhusiano kama mwaka m, alikuwa ni virgin na hakutaka kushiriki tendo la ndoa hadi tulipooana, ni mzanzibar ana maadili ya dini kiasi. Kwao kawaida, baba ni mstaafu wa jeshi na mama ni mama wa nymbani, anjishughulisha na biashara ndogondogo za vitafunwa!

Tatizo lake kubwa ni kuwa hapendi kukosolewa anapokosea, na neno sorry kwake ni kama amejidhalilisha.

Kuna kipindi aliacha kazi alikoajiriwa akidai wakorofi, nilimfungulia biashara ya internet cafe, ilinicost zaid ya 13million! Yeye ndo alikuwa msimamizi lakini haikupita mwezi akawa hasimamii na wakati mwngine hafiki kabisa net nilipomuuliza ndo ikawa mwisho kujihusisha nayo akisema nataka kumnyanyasa kwa ako kanet tu, alisusa na kuniambia hatajihusisha na mali yangu yoyote hata baada ya kumbembeleza!

Kuna pesa pia nilimkopesha kaka yake kipindi cha maandalizi ya ndoa yetu, alipopewa anirudishie alizitumia bila kuniarifu. Nilipomuuliza akasema najifanya kidume nataka kumcontrol kila kitu, yy hatakubali. Nilitamani kusimamisha ndoa! Hata hivyo nilijipa moyo huenda atajirekebisha.

Baada ya ndoa, aliendelea kuwa mama wa nyumbani na baada ya mwezi alishika ujauzito! Vituko vilizid na kama kawaida hakutaka kuambiwa kakosea, nilichukulia ni hali ya ujauzito, niliignore!

Bahat ofsini niliteuliwa kozi fupi ya miezi 6 nje ya nchi, alirud kwao Zenj. Niliporudi alikuwa na ujauzito mkubwa so niliamua kumuacha kwao had alipojifungua.

Baada ya miez miwili nilimfuata.

Lakini nilikuja kuanza kushangaa alipokuwa hataki kushiri nami tendo la ndoa kwa madai kachoka. Ikapita miezi miwili mingine hivohivo! Nilivumilia. Sasa ni zaid ya miez 6 hataki ingawa amekuwa akishauriwa sana na mamaake na ndugu zake wengine!

Nikizungumza nae hudai hana tatizo lolote kibaya zaid anakasirika ukiendelea kumdadisi na ananuna!
Kuna siku baada ya kumbana sana na kumtishia kumrudisha kwao alinambia niongee na dadaake kama nataka kujua kinachomsibu.

Dadaake alinambia kuwa alipokuwa Zenj aliwahi kumwambia kuwa anaponiona tu anahisi hasira na ananichukia tu bila sababu,pia et walienda kwa mganga wa kienyeji ikaonekana ana jini mahaba na hata yeye dada mtu analo ingawa ye mumewe hamnyimi anajitahid kupambana nalo na amekuwa akimshauri mdogo wake bila mafanikio.

Imefikia hatua napachukia nyumbani na hata mtoto sina raha naye coz wakat mungine akiniona nacheza nae huja kumchukua.

Najitahid kumletea vijizawad, lakini ni kawaida kukuta ulichomletea hapohapo hata cku mbili hajakigusa, neno asante kwake hakuna mpaka najistukia may b hapend vitu nnavomletea.

Zaid hapend kabisa kuzungumzia maswala yetu, nimemshauri sana aongee bila mafanikio.

Haonekani kujirekebisha na amewahi kudai talaka nilipomtishia kumpiga siku 1 akidai hajawahi hata kupigwa kibao kwao, kama nimemchoka nimwache!

Wakuu,
Nafikiria nimuache lakini namfikiria pia mtoto atapata taabu kwa kukosa malezi ya baba na mama. Mapenzi yangu kwake yamepungua kwa kweli coz hakuna ule ukaribu wa mume na mke!

NAOMBENI MSAADA WAKUU
 
Ukisikia kua uyaone ndio haya sasa sio magorofa na magari. Vumilia ipo siku yataisha. Tafuta mshenga mweleze il mshauriane muanzie wapi.
 
hilo ni wazi mno
mkeo 'hakupendi wala hajawahi kukuipenda'

wazanzibari nawajua
wanachukulia 'kuolewa' kama 'baraka' ambayo haikataliwi

so mtu anajilazimisha kuolewa hata kama hayuko 'in love' na mwenzie

so wa kwako 'kaolewa' na wewe kama 'sheria' tu
kiukweli hajawahi kukupenda kabisa

majini mahaba visingizio tu
 
dah! Pole sana kaka...ndo maana me bado niponipo kidogo..wake wa kuoa hawaeleweki kabisa...
 
Hiyo hali ya jini mahaba aktika vita vya kiroho huitwa spiritual husband kwa maana limemwoa na linakuona kama unaliingilia. Dalili zake ni mwanamke si kukosa tu hamu bali humchukia mumewe au mkewe bila sababu.

Dawa yake ni kufanyiwa deliverance kwa njia ya maombi na si kwenda kwa waganga. Ukiangalia Emanueli TV live, Jumapili, jumatu na Alhamisi saa 8 hadi 4 usiku utaelewa ninachokisema. Haya maroho yanawaingia watu wengi mno.
Hamna shortcut hapo ni kwenda kwa waombaji kama wachungaji au watumishi na kama huamini katika maombi basi utaendelea na mateso au la uamue kuachana naye.
 
Hapo hakuna upendo, alitaka tu sifa ya kuolewa.
Da wanawake jamani, yaani kila mahali ni kero tupu, sijui malezi ya wazazi kuanzia 1980 yalikuwa na tatizo gani, ndoa nyingi nazishuhudia za vijana wa 80's ziko kwenye misukosuko sana, na asilimia kubwa yanasababishwa na wanawake.
 
Mkuu pole sana kwa matatizo yanayokupata.Kiufupi siku hizi wanawake wakuoa ni wachache sana na asilimia kubwa wako kama huyo wakwako.Nachokushauri pima mwenyewe athari za kumwacha na za kuendelea kuwa naye halafu fanya maamuzi.Nisikudanganye mwenye maamuzi ni wewe maana ndiyo unaepata shida.Nakutakia kila la kheri shehee!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kwa kifupi huna mke, tafuta mke. Usipoteze muda kuishi na mke wa wenzako ndan (Ana bwana nje), kabla ya kumwacha nenda kapime DNA na huyo mtoto huenda sio wako ndo mana ukimgusa tu anakuja kumchukua. Pole sana.
 
Kwa kifupi huna mke, tafuta mke. Usipoteze muda kuishi na mke wa wenzako ndan (Ana bwana nje), kabla ya kumwacha nenda kapime DNA na huyo mtoto huenda sio wako ndo mana ukimgusa tu anakuja kumchukua. Pole sana.

Mkuu nayachukua uliyoniambia. Sijawahi kuhisi kama ana bwana nje kwa kuwa mazingira tunayoishi yako tight kidogo na mara nyingi yuko nyumbani na ndugu na jamaa licha ya kuwa nna uwezo wa kuaccess hata simu yake bila ya yeye kujua na sijakuta hata sms yake or call yenye shaka. Hapo ndipo nnapozidi kuchanganyikiwa mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom