Mke wangu kisirani, anakataa unyumba. Msaada tafadhali

Mke wangu kisirani, anakataa unyumba. Msaada tafadhali

Yooote ni mbwembwe ndoa ni tendo landoa (yaani kijig jig) bila hivyo hakuna ambaye angeoa, hilo ndo namba moja, ukitaka watoto unaanza na hilo, raha, hilo ndo la kwanza, hakuna jibu zuri zaidi ya kutafta namna ya kumwambia byeee! i mean, kama ni mahakama kavunje ndoa upate wa kukupa tunda daily kama mke wangu afanyavyo! nikiwa kazini mara napokea sms Darlin leo ukiingia tu mlangoni jiandae ku... nayo..mara darling kesho mpaka tuchelwe kazini, yan raha tu hata kama haitakesha... lol
 
Pole sana kwa hali hiyo mkuu. Jambo la kufanya nakushauri mpeleke huyo mwanamke kwenye maombezi ataombewa na hali hiyo itaondoka lakini kama unataka hali hiyo isirudi tena inabidi yeye au nyote wawili mfanye maamuzi ya kuokoka km haitawezekana kuokoka hali hiyo itarudi tena.
Jambo la pili ni kuwa kama mmefunga ndoa ya kiislam kuna option ya talaka, mpe talaka ili uoe mwanamke mwingine au kaa na mkee wako mkubaliane kuwa unaongeza mke wa pili. Sasa utakaa kwenye hali hiyo hadi lini? eti unakaa na mwanamke ndani lakini hakuna tendo la ndoa...... duh, hata hivo umejitahidi sana yaani miezi sita mizima humgusi mkeo.
Pamoja na kuwa sijaoa lakini kwangu naona ni mtihani mkubwa sana.
Kila la heri
 
Pole sana kwa hali hiyo mkuu. Jambo la kufanya nakushauri mpeleke huyo mwanamke kwenye maombezi ataombewa na hali hiyo itaondoka lakini kama unataka hali hiyo isirudi tena inabidi yeye au nyote wawili mfanye maamuzi ya kuokoka km haitawezekana kuokoka hali hiyo itarudi tena.
Jambo la pili ni kuwa kama mmefunga ndoa ya kiislam kuna option ya talaka, mpe talaka ili uoe mwanamke mwingine au kaa na mkee wako mkubaliane kuwa unaongeza mke wa pili. Sasa utakaa kwenye hali hiyo hadi lini? eti unakaa na mwanamke ndani lakini hakuna tendo la ndoa...... duh, hata hivo umejitahidi sana yaani miezi sita mizima humgusi mkeo.
Pamoja na kuwa sijaoa lakini kwangu naona ni mtihani mkubwa sana.
Kila la heri
 
mkuu usimuache mkeo! Tafuta tiba za Kiroho. Naamini unampenda mkeo, itakuwa ndoa imara sana kama ukifanikiwa kumpatia tiba mken kuliko kumpa talaka. Hujui ukioa mke mwingine atakuja na vituko gani!
 
kama wewe ni muislamu basi oa mke mwingine. kabla hujafanya hivyo mwambie yeye, mshenga au dada yake.
hakuna mambo ya majini hapo ni tu kwama hakupendi na hataki kusema ukweli. usiamini mambo ya majini go to realitry
 
the truth about love is; kitu chochote apendacho mtu hatapenda kukiacha na vilevile hatakibughudhi. ukitaka kujua mtu anakupenda utapima hicho je anapenda kuwa na wewe? je hataki kukuudhi, je yuko tayari hata kutoa alichonacho kwa ajili yako? simply kabisa kama hayo hayapo jibu ni kuwa upendo hakuna. upendo humea wenye upendo. kama muislamu oa kama mkristo fuata ushauri wa dini ubebe msalaba wako
 
It is very possible ana hayo majini tena kwa hao wazanzbar ts normal thing ss hapo uamuzi ni wako bt hilo tatzo linasovika
1. Tafuta viongozi wa dini i know ww ni muislam bt nakushaur utafte wa kikristo
2. Mueleze tatizo kwanza uanze kuombewa ww alafu uamini
3. Ww pamoja na viongoz mumuombee mkeo cz nna uhakika ukikurupuka kumpeleka kenywe maombi hatokubali ng'o
4. Maombi plus imani yako towards God will deliver her from those evil spirit wherever she is

Nshaona kesi kama hizo nyingi tu na wanasaidiwa yanaisha for your information hata hajijui kama anakufanyia lolote baya na akishafunguliwa utashangaa atakavyoregret the way she is treating you bt kama ukikaa usubiri ajirekebishe tegemea vituko vikali na vipya zaid ya ulivyoviona ss.......Dont let devil mek your life miserable while God is there to defend you my dear
 
deliverence ya jini mahaba dume anayeleta faraka haiangalii DINI wala dhehebu ,njoo Buguruni Kwa Mzee Salu uombewe upone na uonevu wa shetani.
 
pole bhana kuba! hapo wizi mtupu, hakuna Jini Mahaba wala Jina Chuki hapo!
huyo anashida zake tu, ukiona hivo malengo yake ya kuingia kwenye hiyo ndoa haijatimia na amegundua wewe si mtu wa kushikwa masikio!
chapa nje "LIWALO NA LIWE (Mizengo K. Pinda, 2012)"! wa hivo wengi sana, otherwise mruhusu akuweke kiganjani!

Hili nalikubali mkuu, thanx to all GTs
 
Huyu sasa naona ni wa kumpa talaka tu mtoto atalelewa hata na shangazi zake
 
Wakuu
Nilimuoa April 2011. Kabla ya hapo tulikuwa na uhusiano kama mwaka m1.. alikuwa ni virgin na hakutaka kushiriki tendo la ndoa hadi tulipooana, ni mzanzibar ana maadili ya dini kiasi. Kwao kawaida, baba ni mstaafu wa jeshi na mama ni mama wa nymbani, anjishughulisha na biashara ndogondogo za vitafunwa!
Tatizo lake kubwa ni kuwa hapendi kukosolewa anapokosea, na neno sorry kwake ni kama amejidhalilisha.
Kuna kipindi aliacha kazi alikoajiriwa akidai wakorofi, nilimfungulia biashara ya internet cafe, ilinicost zaid ya 13million! Yeye ndo alikuwa msimamizi lakini haikupita mwezi akawa hasimamii na wakati mwngine hafiki kabisa net, nilipomuuliza ndo ikawa mwisho kujihusisha nayo akisema nataka kumnyanyasa kwa ako kanet tu, alisusa na kuniambia hatajihusisha na mali yangu yoyote hata baada ya kumbembeleza!
Kuna pesa pia nilimkopesha kaka yake kipindi cha maandalizi ya ndoa yetu, alipopewa anirudishie alizitumia bila kuniarifu. Nilipomuuliza akasema najifanya kidume nataka kumcontrol kila kitu, yy hatakubali. Nilitamani kusimamisha ndoa! Hata hivyo nilijipa moyo huenda atajirekebisha.
Baada ya ndoa, aliendelea kuwa mama wa nyumbani na baada ya mwezi alishika ujauzito! Vituko vilizid na kama kawaida hakutaka kuambiwa kakosea, nilichukulia ni hali ya ujauzito, niliignore!
Bahat ofsini niliteuliwa kozi fupi ya miezi 6 nje ya nchi, alirud kwao Zenj. Niliporudi alikuwa na ujauzito mkubwa so niliamua kumuacha kwao had alipojifungua.
Baada ya miez miwili nilimfuata.
Lakini nilikuja kuanza kushangaa alipokuwa hataki kushiri nami tendo la ndoa kwa madai kachoka. Ikapita miezi miwili mingine hivohivo! Nilivumilia. Sasa ni zaid ya miez 6 hataki ingawa amekuwa akishauriwa sana na mamaake na ndugu zake wengine!
Nikizungumza nae hudai hana tatizo lolote kibaya zaid anakasirika ukiendelea kumdadisi na ananuna!
Kuna siku baada ya kumbana sana na kumtishia kumrudisha kwao alinambia niongee na dadaake kama nataka kujua kinachomsibu.
Dadaake alinambia kuwa alipokuwa Zenj aliwahi kumwambia kuwa anaponiona tu anahisi hasira na ananichukia tu bila sababu,pia et walienda kwa mganga wa kienyeji ikaonekana ana jini mahaba na hata yeye dada mtu analo ingawa ye mumewe hamnyimi anajitahid kupambana nalo na amekuwa akimshauri mdogo wake bila mafanikio.
Imefikia hatua napachukia nyumbani na hata mtoto sina raha naye coz wakat mungine akiniona nacheza nae huja kumchukua.
Najitahid kumletea vijizawad, lakini ni kawaida kukuta ulichomletea hapohapo hata cku mbili hajakigusa, neno asante kwake hakuna mpaka najistukia may b hapend vitu nnavomletea.
Zaid hapend kabisa kuzungumzia maswala yetu, nimemshauri sana aongee bila mafanikio.
Haonekani kujirekebisha na amewahi kudai talaka nilipomtishia kumpiga siku 1 akidai hajawahi hata kupigwa kibao kwao, kama nimemchoka nimwache!

Wakuu,
nafikiria nimuache lakini namfikiria pia mtoto atapata taabu kwa kukosa malezi ya baba na mama.
Mapenzi yangu kwake yamepungua kwa kweli coz hakuna ule ukaribu wa mume na mke!
NAOMBENI MSAADA WAKUU
Nimesoma nakurudia mara mbili zaidi kuangalia "maadili ya mkeo" sijapaona zaidi ya wewe kusema hivyo. Internet cafe 13m bora ungemuwekea nssf ili akizeeka wakati umekufa kwa stress zimsaidie yeye na mtoto.
 
Hiyo hali ya jini mahaba aktika vita vya kiroho huitwa spiritual husband kwa maana limemwoa na linakuona kama unaliingilia. Dalili zake ni mwanamke si kukosa tu hamu bali humchukia mumewe au mkewe bila sababu.

Dawa yake ni kufanyiwa deliverance kwa njia ya maombi na si kwenda kwa waganga. Ukiangalia Emanueli TV live, Jumapili, jumatu na Alhamisi saa 8 hadi 4 usiku utaelewa ninachokisema. Haya maroho yanawaingia watu wengi mno.
Hamna shortcut hapo ni kwenda kwa waombaji kama wachungaji au watumishi na kama huamini katika maombi basi utaendelea na mateso au la uamue kuachana naye.
Niliacha kutegemea maombi ya mtu mwingine baada ya kugundua Mungu yupo kwaajili ya wote na si kwahawa wajasiriamali pekee. Kuhusu talaka, akimuacha tu ajiandae kugawa mali pasu.
 
Back
Top Bottom