Mke wangu kaacha ndoa yake kisa kazi

Mke wangu kaacha ndoa yake kisa kazi

Mahitaji muhimu.

kaka mahitaji muhimu kwa mwanamke kwako unaweza ukaona ni UPUUZI ,ndiyo maana Bible ikasema tuishi nao kwa akili.

Mwanamke anaweza akawa na pair 50 za viatu ndani na baadhi amevaa mara moja na vizuri tu lakini siku ikaja sherehe akataka umnunulie vingine ukimuuliza mbona vipo ndani vipya jibu atalokupa kwamba tayari wenzake walishamuona navyo...kwahiyo hapo ni wewe kutumia akili ili aweze kukuelewa bila kuleta mtafaruku ndani ya familia.

Mwanamke akimuona rafiki yake kwenye facebook/instagram/tiktok kapelekwa Dubai na boyfriend/mme wake basi na yeye pia atafosi apelekwe yaani baadhi akili zao zipo MAKALIONI ,hawafocus kwenye maendeleo ya familia wao wanawaza na yeye afanye awarushe roho wenzake mitandaoni.

Waswahili wanasema mtoto akililia wembe mpe akijikata ndiyo akili inamrudia ,nimeshuhudia case nyingi sana za wanawake kurubuniwa kwa styles hizo ,wanakimbia familia zao na wanaenda kwa hao michepuko kisha wanatelekezwa ,wanashindwa kujua kwamba huyo mchepuko alikuwa anamtaka yeye kwasababu wake za watu hawana gharama wanahudumiwa na wanaume zao na akishaachwa gharama zinamrudia yeye ambacho hicho kitu hakuzoea hapo ndipo wanapokimbiwa na kuanza kulialia kutaka kurudi tena kwa mumewe OG.
 
Kama mke ameondoka na kukuachia mtoto wa miaka miwili, hakuna mke hapo.

Hakuna mke wala mama hapo, amini !!!

Hakuna mwanamke anayejielewa atakimbia ache mtoto wa miaka miwili.

Huyo ni hana akili, tafuta namna ulee mtoto wako.
 
The bottom line is, women are unpredictable; you are either in or out !! Otherwise you'll die prematurely !! We are living in a very different era !! Your thinking has to be different; always ahead, and readily prepared for whatever comes next !! Women today are not mothers of yesteryears !!
 
Demu malaya anapigwa miti kisa kazi na hata huyo jamaa jirani kishapiga hapo akamdanganya atamtafutia kazi
Demu malaya anapigwa miti kisa kazi na hata huyo jamaa jirani kishapiga hapo akamdanganya atamtafutia kazi
Yawezekana,,, maana hata tendo la ndoa,,, nilikuwa napewa kwa kulazimisha,,,,wakati mwingine anahama kitandani analala chini....ili nisimuombe tendo
 
Nilimuambia avumilie kidogo,,,nitamfungulia BIASHARA,,,,ila yeye ana tamaa ya haraka,,, afu kibaya Zaidi...anayemtafutia kazi Mme wa mtu,,,NYUMBA ya Jirani wakati MKE wake hajui chochote
Avumilie kidogo miaka mitano?
Wewe ni jamii ya wapi na una elimu gani.

Mbona sijaona dalili yoyote ya mkeo kufanya kosa, kaomba kutafutiwa kazi na jirani wala sio mtu wa mbali. Sijaona kwamba amefanya kitu kibaya wala kukusaliti kwenye kutafuta kazi. Kama hutaki aajiriwe mbona miaka mitano yote unamfanya beki tatu tu ndani wewe mwenyewe huna hela ndio maana unatafuta mtaji miaka mitano yote.

Inaonekana kabisa wewe peke yako huwezi kutosheleza mahitaji ya familia mpaka yeye afanye kuingiza kipato. Kwanini unaiga lifestyle ya wanaume wenzako wenye uwezo kiuchumi.

Babu yangu miaka ya 1970s mwanzoni alimpeleka bibi kwenye mafunzo maalum akapate kazi, tena muda huo akiwa mjamzito. Wewe 2026 unaachana na mke kisa anatafuta kazi na mtaji wa kumpa huna. Nenda kaoe kula kulala huyo mke ulikosea hapo ungeishi kwa wasiwasi naye.
 
Mama anaacha mwanae mwenye umri wa miaka 2 na miezi 8? Hii ndio dalili kubwa ya kujua kua huyo ni Mwanamke wa aina gani,

Je ulikua unamtimizia mahitaji yake yote ambayo ni muhimu? Aliwahi kukulalamikia kua kuna mahitaji fulani anataka na ukashindwa kumtimizia? Kilichomsukuma yeye kutafuta kazi ni kipi hasa?

Wasiliana na wazazi wake uwataarifu kisha piga kimya,akili yako iwe kwenye malezi ya mwanao,huyo atarudi mwenyewe,akirudi uamuzi ni wako kama utataka uishi nae au la,

Usionyeshe udhaifu wa kumpigia simu au kumtafuta,fanya kama vile hakijatokea kitu,

Stay strong Mkuu.
Simu kaiacha hajaondoka nayo... kwahiyo kumtafuta ni ngumu,,
 
Avumilie kidogo miaka mitano?
Wewe ni jamii ya wapi na una elimu gani.

Mbona sijaona dalili yoyote ya mkeo kufanya kosa, kaomba kutafutiwa kazi na jirani wala sio mtu wa mbali. Sijaona kwamba amefanya kitu kibaya wala kukusaliti kwenye kutafuta kazi. Kama hutaki aajiriwe mbona miaka mitano yote unamfanya beki tatu tu ndani wewe mwenyewe huna hela ndio maana unatafuta mtaji miaka mitano yote.

Inaonekana kabisa wewe peke yako huwezi kutosheleza mahitaji ya familia mpaka yeye afanye kuingiza kipato. Kwanini unaiga lifestyle ya wanaume wenzako wenye uwezo kiuchumi.

Babu yangu miaka ya 1970s mwanzoni alimpeleka bibi kwenye mafunzo maalum akapate kazi, tena muda huo akiwa mjamzito. Wewe 2026 unaachana na mke kisa anatafuta kazi na mtaji wa kumpa huna. Nenda kaoe kula kulala huyo mke ulikosea hapo ungeishi kwa wasiwasi naye.
Mimi tatizo sio kuamua yeye kujitafutia kazi.....tatizo ni kwanini hanishirikishi,ananificha nisijue kuwa anafuta kazi?. .anakuwa mipango binafsi bila mimi kuwa na taarifa yoyote kama mume wake?,,, Inamaana yumo kwenye ndoa kama kutegeshea ishu zake binafsi
 
Sijasoma mpaka mwisho ila tatizo ni uchumi hapo.
Haupo stable financial,pole sana
"Vita ya uchumi ni mbaya" JPM
Tatizo lake wala sio uchumi. Tatizo la mleta mada ni la kiakili zaidi, mentality.

Huyu superHB it seems ni mtafutaji shida ni vipaumbele ndio hana. Ukiwa na rafiki kama huyu utamjua tu kuwa akili zake zimekaa kimaskini kulingana na misimamo yao mibovu. Analeta ubaunsa kwenye njaa.

Kuna jamaa yangu alifeli shule alikuwa bodaboda akatumia hata hela kumtafutia mke wake kazi. Hata mwaka haukuisha yule jamaa akafariki kwa ajali pale Mbagala, mkewe kwa siku za mwanzoni ndio alipeleka watoto shule na kununua mahitaji kabla ya vikao vya ukoo kutafuta solution.
Kumbe ndugu zetu maskini ukiwa huna kitu kabisa kabisa wanakuepuka utakuwa mzigo completely. Wewe hela ya maji huna, nauli ya mjini huna, ya kula huna, ya dawa ya malaria huna. Wewe kila kitu huna.

Kuna mfanyabiashara Segerea pale alimuachisha mke wake kazi TRA wakati anaenda kumuoa ila wazazi wa mke walikataa, yeye mwenyewe akasaini form kwamba atamlipa 5M kila mwezi kama hela ya matumizi isiyo na maswali imetumikaje (factoring in kupanda daraja kazini + marupurupu). Sasa utamuiga vipi huyu wakati anajiweza, na alimfungulia biashara.

Mwanamke kama kuwa msaliti mbona anakusaliti tu akiwa mpiga umbea na mtazama Sinema Zetu.
 
Kaka mrudishe mke wako, huko ndani pamoto na huku nje pamoto vilevile! Hakuna aliyekamilika, kila mtu ana mapungufu yake ata wewe una mapungufu yako! Hiyo siyo sababu ya nyie kuachana or else kuna kitu unaficha!

Humu watu watakuchanganya sana sijui muache huyo kashakuwa hivi angali wao bado wanavumilia wake zao! Mrudishe msaidizane kutafuta hiyo kazi, wanawake wanapenda security, kama alikwambia mambo ya kazi ukawa unambania obviously lazima angetafuta alternative na huyo mme wa mtu ndio kampa attention na lazima asingeipuuzia! Mrudishe mke wako baadhi ya mambo ambayo haya affect ndoa yenu jitahidi kumsupport hata kama hutaki! Asipojishusha hapo mmoja ndio itaishia hapo! Kama umetambua shida nini so far hebu jaribu kusolve, we ndio mwanaume so far! Tumia akili na uwe calm and collected, ndoa sio mchezo ukiendekeza hisia bishara inaishia hapo!
 
Kuna muda huwa nachukulia ni Stori za kutunga kufrahisha kijiwe tuu.

Ila kama ni kweli ki ukweli basi mnaowa ilhali bado hujawa mwanaume unae weza simama kwenye nafasi yako vizuri.

Nakereka sana watu wanapotumia neno MKE WANGU kwenye Mahali ambako unaonekana husimami kama mwanaume wa huyo mwanamke.

Mwanamke amefikia hatua hizo unamwitaje MKE WANGU?,

Alafu stori kama hizi zimapelekea tuonekane tulo owa tuna shida sanaa.
 
Mimi tatizo sio kuamua yeye kujitafutia kazi.....tatizo ni kwanini hanishirikishi,ananificha nisijue kuwa anafuta kazi?. .anakuwa mipango binafsi bila mimi kuwa na taarifa yoyote kama mume wake?,,, Inamaana yumo kwenye ndoa kama kutegeshea ishu zake binafsi
Hapa tunasikiliza upande mmoja na utajitetea.

Ila huwezi nishawishi kwamba miaka mitano yote mmeishi pamoja na hajawahi kukuomba umtafutie kazi, mpaka kaenda kukuomba mume wa rafiki yake. It doesn't make any sense at all.
Kwani nyinyi huwa hamzungumzii changamoto zenu, future yenu, matarajio yenu? Huwa mnafanya mapenzi tu na kusimuliana umbea.

I can bet 100% alikwambia umtafutie kazi, ukakataa ukasema utampa mtaji. Fast forward miaka mitano imepita kazi huna na mtaji huna. Yeye sio mbumbumbu kwamba hana uwezo wa kujipambania kwa njia halali, akafanya hivyo. Unakasirika kwa yeye kukusaidia swala dogo lililokushinda for 5 years.
 
Mwanamke ni vizuri akajitambua na kujua wajibu wake.
Kazi ni bora awe nayo ili ikitokea haupo familia isihangaike.
Muhimu awe anajitambua
 
Back
Top Bottom