Mke wangu hampendi mtoto wangu niliyempata kabla ya ndoa

Mtoto wa mume wangu aliyezaa nje kabla ya kunioa na nikamfuata kwa bibi yake tukaishi naye na alikuwa sababu ya kuvunja ndoa na hata baada ya baba yake kufariki bado anasumbua

Next week naenda kwenye kesi.

It's better kujihami mapema. Kila mtoto akae na mama yake.
Duh pole sana mumy, huyo mtoto kaathiriwa na ndugu zake hasa mama yake mzazi kwakuanza kumjaza maneno mabaya na kufanya kukuchukia toka akiwa mdogo dah nihatar sana. Anapaswa akae na mwanasaikolojia kulingana na umri wake anaweza akashauriw na akawa vzr
 
Mtasema yote lakin mtoto pia ana haki ya kuishi Na baba yake,hamuwezi inabidi mtafute wanaume ambao hawana mtoto kabisa,lakin unaenda kuwa Na mtu unajua ana watoto!! mtoto anabana nini acheni uchoyo leeni watoto
Waoane wote wenye watoto ili kuepusha sintofahamu
 
Hata akiwa anazalisha huko kila kukicha analeta nyumbani wewe kazi yako nikulea tu! Au unamaanisha nini?
Hapana nikimkuta nao
Lakin kuja watu waume zao wanazaa kila kukicha hapo balaa
 
Makasiriko ya nini how can you force someone to love ur kids nyie nyie wanaume huwa hamtaki watoto wake wengine mnataka waende kwa Bibi au baba zao, tujifunze responsible kwa action zetu wewe uzae then muachane kwa tabia zenu halafu mu force mtoto kupendwa
Nani kakwambia kila anayekua na watoto nje ya mwanamke aliye naye currently ni kwa sababu ya kuzaa ovyo?

Wengine wamefiwa na wake zao wakiwa bado vijana wakaamua kuoa tena.

Inaonekana wazi ww una roho ya kishetani na ni rahisi sana hata kumchoma mtoto na pasi kisa kaiba Tsh 100/=.

Naamini mtoto hana hatia na action za baba au mama yake. Anahitaji upendo na kuwa treated kama mtoto.

Na ujue most of these kids ambao wananyanyaswa ndio wanaokujaga kuwabeba hao watoto uliokua unawalea kimayai wakawa mazuzu hadi kwenye maisha.

Mtoto ni mtoto asee
 
Duh pole sana mumy, huyo mtoto kaathiriwa na ndugu zake hasa mama yake mzazi kwakuanza kumjaza maneno mabaya na kufanya kukuchukia toka akiwa mdogo dah nihatar sana. Anapaswa akae na mwanasaikolojia kulingana na umri wake anaweza akashauriw na akawa vzr
Ana roho mbaya tu mamake alifariki hata kabla sijachukua.
 
Watu mliozaa kwanini huwa mnapenda ku force watoto wenu wapendwe na wengine kilazima hasa ukichukulia mitoto yenyewe huwa mikorofi imeathiriwa na ugomvi wenu wa mahusiano yali yovunjika na ni watoto wasio pendeka hata ufanyeje wataona huyu sio mama yetu.

Kuku tu mwenyewe huwa anakimbiza vifaranga visivo mhusu sembuse binadamu, na kama kweli ulikuwa na upendo why haukupatana na uliyezaa naye mkamlea mwanenu yeye aligoma then una force mtoto apendwe na mpenzi wako mpya.

Mpenzi wako kaja kwako ku enjoy mahusiano na sio kuhangaika na mtoto asiye mhusu

Mkuu tukuhukumu au tukuache na uhuru wa mawazo yako..
InFact muhimu ni mtoto alelewe malezi ambayo ataona hakuna upungufu wowote au manyanyaso,,, sio lazima ampende sana ila ampe treatment sawa na watoto wake inatosha,
 
Watu mliozaa kwanini huwa mnapenda ku force watoto wenu wapendwe na wengine kilazima hasa ukichukulia mitoto yenyewe huwa mikorofi imeathiriwa na ugomvi wenu wa mahusiano yali yovunjika na ni watoto wasio pendeka hata ufanyeje wataona huyu sio mama yetu.

Kuku tu mwenyewe huwa anakimbiza vifaranga visivo mhusu sembuse binadamu, na kama kweli ulikuwa na upendo why haukupatana na uliyezaa naye mkamlea mwanenu yeye aligoma then una force mtoto apendwe na mpenzi wako mpya.

Mpenzi wako kaja kwako ku enjoy mahusiano na sio kuhangaika na mtoto asiye mhusu
Toto korofi sawa hapo sitii neno ila kama una machuki yako kama ya mama ya kambo huo ni ujinga mkubwa kumchukia mtoto ambae aliletwa duniani bila idhini yake.Kwani alipenda kuzaliwa then wazazi wake waachane.
WANAWAKE WA KIBONGO WENGI NI MAGAIDI UNAWEZA MKUTA MMAMA AMA MDADA NYUMBANI KWAKE ANAMNYANYASA MTOTO AU DADAWA KAMBO ALAFU JUMAPILI ANA NENA KWA LUGHA HADI MACHOZI YANAMTOKA AKILILIA HURUMA YA YESU.pumbafuuu
 
Hivi mwanamke kumkataa/kumchukia mtoto wako uliyezaa kabla ya kumuoa. Kuna mapenzi hapo? Yaani hampendi Mwanao je wewe atakuwa anakupenda kweli?
Hapa wanawake wengi pamewashinda.Mshukuru Mungu umegundua kwa sababu angeweza kukudanganya kwa kujifanya anampenda kumbe siyo.sasa ikifikaga hapa huwaga hakuna jawabu zaidi ya kumhamisha mwanao hapo nyumbani,yaani alelewe na ndugu yako wa karibu labda dada ako hivi.sababu ukichelewa atapewa sumu afe
 
Sio kujitambua ni heri kuanza kulea mtoto mchanga inakuwa ni rahisi kuliko huyo mkubwa ambaye ameathirika kisaikolojia haleleki tena maugomvi ya wazazi yamemharibu akili na watoto wa sikuhizi jinsi walivo sio rahisi kiukweli na sikuhizi watu kuzaa zaa hovyo ni fashion, mkaka kazaa na wanawake wa nne tofauti anakuja kuoa mtu hana mtoto amsaidie kulea watoto wa baba asiye na self control same applies na kwa single mom hyo ni kutesa watoto na kuja kulaumu wengine kuwa hapendi watoto wako.

Turudi kwenye maadili zamani ilikuwaga marufuku kuzaa bila ndoa na watoto walilelewa na wazazi hakukuwa na shida, ila sikuhizi umalaya na kuzaa hovyo ni sifa why uhurumiwe kwa kuleta mtoto bila kujipanga!?

Tuache kutesa watoto kwA umalaya wetu
Na nyie mmezidi kutubebea mimba bila ya sisi kutaka mtoto.Unalikuta li msichana kisa limekuona una gari na ka nyumba basi linaamua livae mabomu kwa kukubebea li mimba lisilo pangwa.Hapo limesahau kuwa umeliomba uchi na sio Mimba.
Ma sichana ya kibongo mavivu kujitafutia maisha yanawaza kuolewa kwa kumzalia mtu kisa ana maisha yaani mimba imekuwa kama mtego wa kutangaziwa ndoa.Tena usiombe ukutane na mi sichana yenye rangi nyeupe mivaa vimini na ile yenye mitako sampuli hizi mbili ndo zinaongoza kutengeneza misichana isio na akili za maisha.Mawazo yao kuuza mikoba kumbe inatafuta wanaume.@Dinazarde
 
Kinachopondwa na kuchukiwa Ni tabia za wanawake husika.

Sio mtoto,
Sijawai sikia au kuona mwanaume anamchukia mtoto wa single mother Hata sikU moja.

Wengi wanaoishi na single mother, wanalea effectively watoto wao.
Ndoo maana na sisi hatuwapendi ma single maza kwa sababu wao wana roho ngumu sana kwa watoto wetu wa nje
 
Nitajiskia kawaida kabisa moyoni, mtoto wangu why maneno ya wengine yaniumize I'm responsible with my actions na nina accept choices zangu maishani with my full chest, and I can do anything to Ensure mental health ya mwanangu haipati mushkeli wote na ikiwa lazima sitaki ku affect afya ya mwanangu na mahusiano yangu kabisa kabisa, and I can't blame anyone
Wao wanataka waharibu mambo Wao halafu wambebeshe lawama mwingine.
 
Wengine tunawapenda tu hatuna shida nao kabisa
Mi napenda watoto wewe wangu wasiwe wangu nalea tu
Inawezekana unasema hivi kwa sababu umelea/unalea watoto wa ndugu zako mfano wa kaka yako,dada zako,wa Shangazi,wa mjomba au hata wadogo zako..
Au watoto baki yatima wasiojiweza.


Subiri mumeo akuletee mtoto aliyezaa nje umlee uone kama ni rahisi.
 
Sisi mbona wakwenu huwa tunawalea kiroho Safi TU?

Wanawake Ni viumbe wabinafsi Sana.
Mnachukulia suala la kulea kirahisi rahisi sana nyie watu!! Mama ndio mlezi kwa kiasi kikubwa, yeye ndio anatumia muda mwingi na mtoto kuliko baba. Hivyo madhaifu yake ni rahisi kuwa noticed zaidi. Kulea mtoto asie wako inahitajika upate support kubwa sana kutoka kwa wazazi halisi wa huyo mtoto. Hivyo kama wanakuletea mauza uza basi ni ngumu mnoooo.

Kwa upande huu upendo hujengwa na wala haulazimishwi, kama ambavyo ninyi mlichukua muda kufahamiana na kupendana pia inahitajika muda kubond na mtoto/watoto. Sasa kama kuna mambo meusi hayaeleweki ni ngumu aisee, hisia zikishaumizwa ni ngumu sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom