Mke wangu habebeki...

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,969
1,392
Niko nasoma nje ya Tanzania huku nifanya kazi katika company fulani nikilipwa mshahara dollar 1,800 kwa mwezi,najigharamia mwenyewe masomo yangu kwa 50% nyingine ni sholarship na gharama nyingine za maisha.

Nimeacha mke na mtoto mmoja nyumbani.mke wangu najitahidi kumtumia dollar 1,000 kila mwezi.yeye anafanya kazi katika shirika fulani Tanzania na anapokea mshahara kiasi fulani mara zote analalamika pesa ninayomtumia haitoshi imagine juzi nimetuma kwa exchange rate ya Tanzania alipokea kama Tsh,1,800,000 bado ananipigia cim na kunigombeza pesa haitoshi kwenye matumizi yake ya maisha na mtoto sasa jamani huyu ni mke au mzigo?

Nimemweleza hari halisi ya maisha ya huku haelewi naishi kwa kujibana ili kile kinachopatikana tukiserve lakini wapi nahisi kama nilikosea kwenye uchaguzi au anafanyia nini hiyo pesa ya kila mwezi au anaamua kunifanyia ushenzi tu nimemwambia kuna watu wanalia mchana na usiku wanakosa bahati kama hiyo lakini haelewi.

Ila ninafikiria kumchukua mtoto wangu akalelewe na mama yangu mzazi au nimchukue nihishi naye ..nahisi huyu mwanamke nimzigo tena haubebeki..nasiyo kwamba kuna assets za ndani ananunua nyumba hiko full hadi usafiri nilimpatia wa kutumia.

Jamani mke wa namna hii nimfanyeje?

1627195481933.png

 
Duh! Ndugu yangu, hilo ni gunia la misumari, halibebeki. Kadiri unavyoligeuza ndivyo unavyolipa nafasi kukuumiza zaidi.
Ukitahamaki, amemaliza kujenga kwao halafu anakwambia samahani nilipotea njia.

Rejea TZ haraka, chukua mtoto wako, mpeleke kwa mama na yeye mpe mapumziko. Aelewe TZ wapo wanaoishi kwa chini ya Ts. 300,000 kwa mwezi, sasa ikiwa yeye 1.8 million pamoja na mshahara wake tuseme ni 200,000 tu, tayari anazo 2millions. Amka baba!
 
Unaibiwa ndugu yangu. Mtoto mmoja tu unatoa zote hizo. wengine hutoa wakirudi . Hah hah Joke
 
Mkuu fanya uchunguzi wako taratibu tena kwa watu ambao unawaamini kuwa ni nini kipo nyuma ya pazia
Maana unaweza kuta anajenga kwao au anahonga wanaume na mtoto wako anaishi kwa shida
Kwa sababu kwa hali halisi yeye na mtoto tuu kutumia 1.8m ni issue sana kaka
Kuwa makini kabla ya kuchukua maamuzi yako kaka
 
Mnachokisema ni kweli ila wazazi wangu wanamtetea sana..hata sijui hawewapa nini?
 
Jamani pole sana, nitarudi baadaye kwa ushauri . Sisi wanawake sometimes......
 
Labda kama anatumia na hao wazazi. Otherwise huyo mkeo ni mfujaji na kama ndiyo life style yake hiyo looh! Alitakiwa aolewe na wazee wa EPA siyo wewe unaetegemea monthly salary! Pole ndugu. Kwani background ya wazazi wake ikoje financially?
mnachokisema ni kweli ila wazazi wangu wanamtetea sana..hata sijui hawewapa nini?
 
Du pole sana mkuu, au labda anawapa hizo pesa wazazi wako pia ndio maana wanamtetea.
 
Duh! Usd 1000 per month haimtoshi?! Na bado ana ajira!
Wake up mkuu hapo unaibiwa.
 
Muache uniowe mimi, ukirudi unakuta gorofa na magari kama manne! unaibiwa jamaa yangu!
 
mnachokisema ni kweli ila wazazi wangu wanamtetea sana..hata sijui hawewapa nini?
Mara nyigine wazazi umri ukiwaenda sana wanakuwa kama watoto-wanashindwa kusoma michezo mingine-au yeye anawahandle vyema kwa kuwa anajua ndo wapo karibu naye ili kukupa support yao pindi atakapokuwa anaihitaji
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom