Habari zenu wakuu
Maisha ni kusameheana
Uchumi wangu ni mzuri tu ni wa kati, nikisema uchumi wa kati wengi mnanielewa, nyumba nzuri, biashara nyingi, kazi nzuri, tunakula tunachotaka, mke wangu alikuwa anavaa mavazi ya gharama anayoyahitaji ,ndani fenicha nzuri za kutosha, tv touch screen inch 100, maisha mazuri kiujumla
Kuhusu show, namchapa show ya kutosha mpaka analiaga, yoooh yoooh nzuri endelea, oooh basi pumzika acha, toa kwanza, naomba nipumzike dk 5 kwanza.. wengi mnaelewa mipinduko ya kutosha
Kabla hajaondoka kwa muarabu nilizaa naye watoto mapacha wawili wa kike, now wana miaka 3
Katika mabiashara akakutana na huyo muarabu na nikashtukia katika uhusiano wetu wa kindoa, nikaona huyu kuna kitu ananificha
Siunajua ukiwa upo vizuri kiuchumi unakuwa na watu wa karibu wa kukupa maneno ya hapa na palee, wakanipa full story kuhusu mahusiano yake na muarabu
Usiku mmoja aliniaga anaenda kwenye shughuli na nikamruhusu na nikampa na gari ndogo aende nayo ila niliweka gps-location kwenye gari nijue anaenda ukumbi gani
Na alinambia atarudi saa 9 usiku, si unajua shughuli za usiku maukumbini huko, kumbe hakuwa anaenda ukumbini na location ikanionyesha walipoenda kula bata na huyo ponjoro wa kiarabu, ni mtu mzima na bonge pia
Nikachukua watu wangu wa karibu kama wawili hivi na kuanza kuifatilia hiyo gps-location , tukawakuta wapo hotel ya nyota 5 huko mjini ***** napastili
Kufika hapo nikaanza kutumia pesa kidogo ili waweze kunipa chanse ya kwenda kuwafumania na nilianza kuwatisha kama mtu mwenye cheo fulani kwa mkwara mzito na kutishia kuifungia hiyo hotel kwa figisu figisu za mjini
Wa kanipa full detail na nikafanikiwa kuingia mpaka chumbani nikawakuta na huyo jamaa, kibaya zaidi alikuwa mwanamke wangu wa ndoa
Ilikuwa ni fedhea kwa kweli, ameacha watoto nyumbani na wadogo kipindi hicho walikuwa bado wananyonya, yaani kwa kupagawa na waarabu na kwangu kila anachotaka nampatia, alinifedhehesha sana
Baada ya kumuhoji alinambia yupo tayari tuachane na kweli nilifata utaratibu nikampa taraka kwa muongozo wa mahakama
Mwarabu alimbadili dini akamuoa baada ya mda mfupi alimuacha kwa dharau na matusi mengi..
Nafikiri anaweza kuwa alifata michezo ya wasichana wa mjini kwa mwarabu, nikisema michezo ya wasichana wa mjini mnaelewa na mimi hivyo vitu situmii so nahisi tu ila sina uhakika..
Aisee siwezi kuwalaumu wanawake wote, ila huyo kitendo alichofanya ni kibaya sana, na waenga wanakwambia kuku wako manati ya nini?
Alirudi kwa vilio na magoti na misamaha mingi sana na hakukuwa na budi tu ilibidi nimsamehe na tuendelee na maisha kwani tumeshazaa na tuna watoto si vyema kuacha watoto walelewe na mzazi mmoja
Tukabidi tufate utaratibu na kufunga ndoa tena na sasa ana ujauzito tunatarajia kupata mtoto
Ndoa ni jambo la kheri sana na ukilipata unatakiwa ulilinde kwa nguvu zote misuko suko na mabonde kwenye ndoa yapo tu , kusameheana ni nguzo kubwa kwenye ndoa
Nikimfumania tena safari hii simsamei, nitatafuta mwanamke mwengine nitamuoa
Nampenda sana mke wangu ❤️