Mke wangu ananipa wakati mgumu

Jaribu kufikiri hivi.

1. Angeweza kutoa bila kukujulisha na kamwe usingejua. Je ni kwanini akuambie halafu anaenda kuitoa?
2. Kama alikuwa ana kujaribu alikuwa ana test nini hasa. yaani alitaka kujua nini?

Nionavyo mimi mke wako yuko njia panda. Ana mtu ambaye kwa akili yake anaona ni sahihi zaidi kuliko wewe. Inawezekana hata huko kuondoka kwake ilikuwa ni namna ya kutafuta nafasi ainjoy na huyo mtu. hakuhitaji tena, yaani anataka kutengeneza mazingira muachane ila akusingizie kwamba wewe ndo ulimiacha wakati yeye alikuwa anatania.

Chakufanya.

1. Kaa zako kimya usimtafute wala usimtumie fedha za matumizi. Akikutafuta mwambie aendelee na maisha yake kwani na wewe unakaribia kuoa.

2. Kama kweli anakuhitaji.atarudi nyumbani kumaliza msala. Mdani ya wiki tu. Ukiona anakupotezea ujua ndo imetoka hiyo.

3. Kuanza upya si ujinga...

Ila hujasema.swala la hela, je una hela?
 
Nilijikaza nimefupisha tu maelezo ila mwanzo alikua serious hana tabia yakuigiza kulia aliyemshauri aniambie ni utani kanipa wakati mgumu yani hata akipiga sim mwili unaishiwa nguvu
Mzazi mwezako hawezi kufanya utani wa jambo km hilo. Hiyo ni kweli 100% wanawake ni wazuri sana kwa kuigiza.
Pole sana ndugu.
 
Hamna haja ya kumrudisha nyumbani, huyo akampime hukohuko alipo, akisibitisha anamalizana nae hukohuko!
Sahii kabisa,
Lengo lilitakiwa amshtukize kumpima gafla
Ili asije kujipanga akampiga changa la macho

ukweni hiyo itakua ngumu maana hawawez kushea choo kimoja Kama vile akiwa kwake.

Akiwa ukweni ataomba mkojo,
Mwanamke ataingia chooni atazuga zuga afu atapeleka mkojo wa mdg wake. Ukipima kitu haimo

Anachopaswa ni waingie wote chooni akojoe mkojo anauona ampatie ili aupime pale pale.[emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakishazibomoa ndoa zao kwa kiburi cha mchepuko ukosa vyote mume na mchepuko, kesho uenda kukanyaga mafuta kwa mtume wao, yule jamaa ni haki yake kula pesa.
Hakuna mchepuko mpumbavu atakaekubali kuchukua goma lililochezea ndoa yake, maana anajua kama jamaa kafanyiwa hivi Mimi ni nani nisijefanyiwa vile usepa kimyakimya. Mke wa mtu akishaachika na michepuko hula kona na kurudi kwa mme hawezi alilikoroga anaishia kuwa super single mothers mkosa pote. Halafu unakuta wanawake waliochwa kwa kuchezea ndoa zao huwa ndio washauri wazuri wa ndoa, SAsa wewe mbona uliichezea.

Yaani natamani ujumbe huu niulaminate niwawekee wanawake wote kwenye vyioo vyao vya kujitazamia, huwa wanaelewa baada ya kuachika. " Nyie KINAMAMA ukiichezea ndoa YAKO kwa kiburi cha mchepuko ukiachwa na mchepuko ula kona, nani abebe mzigo.
 
Pumbavu unakuwa kama juma lokole take action.
 
Ushauri tu ungefunga safar ya kushtukiza mpaka uko kwao mkononi umeshika UPT(kipimo cha mimba) ukifika tu bila maelezo unamchukua unampeleka gest unamsimamia akojoe then unapima Mkojo ukikuta Imo ujue umepigiwa


Akili kubwa hii
Nasema uongo ndugu zangu?
 
Halafu mtu akiua, unasikia wapumbavu wakisema wanaume wana roho mbaya...
 
Dah!!!!!huyo dada kazingua Sana tatizo wanawake bwana tunaendeshwa Sana na hisia,Sasa huyo aliyemjaza ndio kamuona wa maaaaana kumzidi mume aliyempenda na kujitoa hata kumuoa kabisa,yaani hisia zipo on duty kasahau kila kitu,,,,alikwambia makusudi ili uumie useme humtaki Tena ili aendelee na huyo father pregnancy,Sasa bahati mbaya father pregnancy kamgomea na kumpa huo ushauri wa kijinga eti nakutania,my friend hapo hakuna utani!.....Aisee hapo Sasa utaamua mwenyewe kuzika ama kusafirisha
 
Baba D, kwani wewe kufika huko alipo mke wako ni Sh ngapi?
Kama una Kifua nenda Hata kesho kisha nunua just UPT tu mcheki mimba! Kama alikuwa nayo Hata kama kaitoa upt itasoma positive. Baada ya hapo maamuzi utajua wewe mwenyewe!
 
Kunywa sumu ujifie.Unaambiwa kila siku Tanzania ni nchi ya ujamaa.Maana yake kila jambo litumike kama jumuiya.Yaani kuchangia.Usikonde.
 
Ulishawahi kuona mtu anapata medali ya kuvumilia ndoa. Nitavumilia shida e.g hali ngumu ya kiuchumi na ugonjwa lakini sio haya matatizo ya kujitakia.
 
...ebu wangu nikomae naye tu kumbe yake ya kawaida tu, ahsante bro!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…