Mke wangu ananipa wakati mgumu

Jusikafiri

Member
Sep 6, 2022
12
67
Bila salamu,

Ndugu zangu mimi ni mwenyeji humu ila nimetumia ID hii ili nipate msaada kwa tukio lililotokea hivi siku za karibuni huenda kuna sehemu nafeli kama mwanaume au haya mambo ya maumivu ndugu zangu mna uzoefu nayo.

Nina mke wangu ambaye tupo kwenye ndoa takriban miaka mitano sasa na tunae mtoto mmoja wa miaka mitatu tulikuwa tunaishi kwa furaha na amani hapo nyuma sasa siku za karibuni mambo yakaanza kuvurugika ugomvi ugomvi hauishi ubishani haukauki ndani, kuna muda naona ni mambo ya kawaida ndo ubinadamu wenyewe kukwaruzana ni mambo ya kawaida.

Niende kwenye mada, Miezi kama mitatu nyuma mke wangu alienda kwao mkoa mwingine kuna mambo alienda kufatilia huko ya kifamilia na kazi, sasa kipindi cha mwanzo hali ilikuwa shwari tunawasiliana vizuri badae mambo yakaanza kubadilika ugomvi kwenye simu unamwambia hili yeye anafanya lingine nilijikaza sana sasa juzi nikaona niongee nae vizuri mke wangu tujue shida nini tujenge palipobomoka.

Ila kiukweli huyu mwenzangu hakuwa na amani sana ongea yake ilikuwa kinyonge sana na kuna siku za karibuni nilikuwa nakasirika hadi natishia kumuacha ila likuwa anasema sawa tu niache.

Ilikuwa asubuhi siku hiyo naongea naye kiustaarabu kabisa kuwa ana shida gani mara gafla akaanza kulia kwenye simu ananambia kuna jambo anatamani kuniambia ila anahofia litaleta madhara basi nikaanza kumbembeleza pale bora aseme tu ni jambo gani tujue tunafanyaje, hapo roho ipo juu juu navuta picha mambo mbalimbali hayaji akilini baadae akaamua kusema kinachomsibu akanambia “baba D nina mimba"

Sikuwaza chochote kibaya nikamuuliza tu sasa kwanini hukunambia muda wote na hiyo mimba ina muda gani? Akanijibu kuwa inakaribia mwezi sio yako.

Alooo! Nyie watu kumbe kuna mambo yanauma hivi nilihisi kama nimetobolewa moyo na kitu cha baridi niliishiwa nguvu masikio yalikuwa kama yameziba, namsikia kwa mbali analia sana ananiomba nimsamehe na ana mpango wa kuitoa tu nikamuuliza mmekutana mara ngapi na huyo mtu akanambia mara 3

Nilikata simu kwakweli nikatulia kama nusu saa nafikiria jinsi alivyokuwa akigegedwa mke wangu yani nilikuwa nasikia hadi sauti za mahaba kichwani ndugu zangu haya mambo kumbe ndo yanauma hivi.

Nilipiga sana simu ilikuwa inatumika kama dakika 20 hivi alionesha yupo busy kuna mtu kama wanajadiliana, badae akapiga simu mwenyewe yani simple eti baba D nilikuwa nakutania tu nijue msimamo wako.

Sijawasilina nae mpaka leo hii namuonea huruma sana mwanangu sijui nafanyaje ila nina homa mwili hauna nguvu, yani kwa maelezo yale naona hakuna utani ni tukio lipo na huenda wamejadiliana na huyo malaya mwenzake watoe mimba.

Inauma aise mke wangu kachakatwa, hapo sidhani kama kuna utani

Nishaurini nifanye nini sijamtafuta hadi sasa hivi na leo naenda kunywa pombe kwa mara ya kwanza.

Ukweli mtupu hakuna utunzi.
 
Ungemtega ili upate uhakika kweli anayo alafu ndo uamue kadri moyo wako utakavyopenda mana si wote wanaweza samehe japo wapo ambao wanafanya kama hakuna kilichotokea na maisha yanasonga!
Nilijikaza nimefupisha tu maelezo ila mwanzo alikua serious hana tabia yakuigiza kulia aliyemshauri aniambie ni utani kanipa wakati mgumu yani hata akipiga sim mwili unaishiwa nguvu
 
Mjusi Kafiri pole sana, ukimaliza kunywa jaribu ku download series inaitwa House of Cards 1&2 ni ya Muda kidogo. utakachokutana nacho humo ndio ushauri wangu kwako ndugu yangu
Itabidi niiangalia iyo ninayo ila nimeangalia kidogo tu mwanzoni
 
Pole sana mkuu. Katika maisha hakuna mkamilifu kwa asilimia hata 80. Ushauri wangu kwako ni huu.

Jitafakari na jiangalie ndani ya moyo wako na matendo yako. Je umewahi kumsaliti mke wakoo? Mara ngapi? Na kwa yup na yupi? Je unampenda mke wakoo?

Jiulize hayo maswali mara nying kadri uwezavyo alafu tumia akili tulivu kufanya maamuzi ukijifikiria nawe je umewahi kuchepuka then utoe hukumu kwa upande huo.

Usinywe pombe mkuu maana haitakusaidia kitu zaid ya kukumalizia hela zako na kukuharibia cv yako.

relax bro huu mchezo wa ndoa hauhitaj hasira ila uaminifu na moyo wa kusameheana
 
Kama hujawah kunywa pombe, usithubutu hata kuionja wakati huu wa stress, pombe itachochea kuharibikiwa zaidi katika mipango yako, imekupasa kunywa kwa furaha.

Je, unauhakika ni mjamzito na baba wa ujauzito ni sela fulani la kitaa?

Je, mwenendo wa mkeo hapo home kwako ulikiuwaje?

Je, wakati wa kupiga shoo, ulikuwa unamsatify?

Je, hali ya uchumi wako ikoje?

Jibu kwanza haya, tupate mwelekeo

Nayeyuka kitahilatahila
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom