Bila salamu,
Ndugu zangu mimi ni mwenyeji umu ila nimetumia ID hii ili nipate msaada kwa tukio lililotokea ivi siku za karibuni huenda kuna sehemu nafeli kama mwanaume au haya mambo ya maumivu ndugu zangu mnauzoefu nayo.
Nina mke wangu ambaye tupo kwenye ndoa takribani miaka mitano sasa na tunae mtoto mmoja wa miaka mitatu tulikua tunaishi kwa furaha na amani apo nyuma sasa siku za karibuni mambo yakaanza kuvurugika ugomvi ugomvi hauishi ubishani haukauki ndani, kuna muda naona ni mambo ya kawaida ndo ubinadamu wenyewe kukwaruzana ni mambo ya kawaida.
Niende kwenye mada, Miezi kama mitatu nyuma mke wangu alienda kwao mkoa mwingine kuna mambo alienda kufatilia uko yakifamilia na kazi, sasa kipindi cha mwanzo hali ilikua shwari tunawasiliana vizuri badae mambo yakaanza kubadilika ugomvi kwenye simu unamwambia ili yeye anafanya lingine nilijikazana sana sasa juzi nikaona niongee nae vizuri mke wangu tujue shida nini tujenge palipobomoka.
Ila kiukweli uyu mwenzangu hakuwa na amani sana ongea yake ilikua kinyonge sana na kuna siku za karibuni nilikua nakasirika hadi natishia kumuacha ila likua anasema sawa tu niache.
Ilikua asubuhi siku hiyo naongea naye kiustaarabu kabisa kuwa anashida gani mara gafla akaanza kulia kwenye simu ananambia kuna jambo anatamani kuniambia ila anahofia litaleta madhara basi nikaanza kumbembeleza pale bora Arsene tu ni jambo gani tujue tunafanyaje, hapo roho ipo juu juu navuta picha mambo mbali mbali hayaji akilini baadae akaamua kusema kinachomsibu akanambia “baba D nina mimba"
Sikuwaza chochote kibaya nikamuuliza tu sasa kwanini hukunambia muda wote na hiyo mimba ina muda gani? Akanijibu kuwa inakaribia mwezi sio yako.
Alooo! Nyie watu kumbe kuna mambo yanauma ivi nilihisi kama nimetobolewa moyo na kitu cha baridi niliishiwa nguvu masikio yalikua kama yameziba, namsikia kwa mbali analia sana ananiomba nimsamehe na anampango wakuitoa tu nikamuuliza mmekutana mara ngapi na uyo mtu akanambia mara 3
Nilikata simu kwakweli nikatulia kama nusu saa nafikiria jinsi alivyokuwa akigegedwa mke wangu yani nilikua nasikia hadi sauti za mahaba kichwani ndugu zangu haya mambo kumbe ndo yanauma hivi.
Nilipiga sana simu ilikua inatumika kama dakika 20 hivi alionesha yupo busy kuna mtu kama wanajadiliana, badae akapiga simu mwenyewe yani simple eti baba D nilikua nakutania tu nijue msimamo wako.
Sijawasilina nae mpaka leo hii namuonea huruma sana mwanangu sijui nafanyaje ila nina homa mwili hauna nguvu, yani kwa maelezo yale naona hakuna utani ni tukio lipo na huenda wamejadiliana na uyo malaya mwenzake watoe mimba.
Inauma aise mke wangu kachakatwa, hapo sidhani kama kuna utani nishaurini nifanye nn sijamtafuta hadi saizi na leo naenda kunywa pombe kwa mara ya kwanza.
Ukweli mtupu hakuna utunzi.