Mke wangu ameniacha njiapanda

EL ELYON

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
1,563
1,886
Wakuu mmebarikiwa sana na Mwenyezi Mungu.

Jana usiku ulitokea msala mmoja mimi na mke wangu.

Smartphone ya mke wangu ilivujia wino kwa bahati mbaya bado hajaipeleka kwa fundi sasa J5 aliniomba simu yangu aweke application ya business WhatsApp ili achart na marafiki zake nikamwambia sawa.

Sasa jana usiku nilitoka kidogo wakati nipo njiani ikaingia sms kwenye WhatsApp upande wa namba yake ikiwa inasema MAMBO....mi nikajibu NANI....ikajibiwa IMA....nikamjibu UNAJUA UNACHART NA NANI....akajibu JINA LA MKE WANGU.....nikamwambia OK....tukasalimiana nikijdai kama mimi ndo mhusika yaani mke wangu.

At last jamaa akaomba picha nikamkatalia kwa kumwambia siwezi na nikauliza yanini picha. Jamaa akadai amemiss kuniona yaani kumuona mke wangu.

Nikamuuliza umemisi nini akajibu MAMBO YAKO BADO SJASAHAU....nikauliza mambo gani akajibu ya KITANDANI.

Nilipofika nyumbani nikamsalimia mke wangu nikamwambia anipe simu ndogo aliyokuwa nayo kucheck upande wa dialed call nikakuta ni muda si mrefu alikuwa anaongea na jamaa aliyekuwa amemtumia sms WhatsApp jamaa alikuwa kampigia wameongea kama dk 3.

Nikamuuliza huyu uliyekuwa unaongea naye ni nani wakati huo sjamwambia chochote kuhusu charting za hiyo namba kwenye WhatsApp yake.

Akajibu huyo ni shemeji yake kule alikoolewa mdogo wake.

Nikamuuliza mara 3 huyu ni nani maana pia namba hakuwa ameisave akashituka akauliza kwani kuna nini.

Nikamwambia kwahiyo wewe ulikuwa unafanya mapenzi na shemeji yako au siyo. Akashituka hapana nikamuonyesha WhatsApp vile jamaa amesema mke wangu akakataa kabisa eti jamaa akajiandikia tu ila hakuna lolote kama vipi tumpigie nikamwambia ok ngoja tumpigie wakati najiandaa kupiga akakataa ooooh subiri kwanza nikwambie nikakataa maana tumeshakubaliana tupige simu na yeye hilo wazo ndo kalisema.

Nikapiga jamaa akapokea mke wangu akagoma kbs kuongea nikakata simu.
Nikaenda zangu sitting room nikamuacha room.

Sasa tokea wakati huo sijaongea naye chochote namuangalia tu nimetoka job hapa namcheck tu maana sina kawaida ya kupiga mwanamke na sijawahi kumpiga hata kofi.

SASA WAKUU MNANISHAURI NICHUKUE HATUA GANI, PILI KWANINI MKE WANGU ALINIDANGANYA, TATU JE HUYU MKE NA HUYU JAMAA YAKE WAKIKUTANA MNADHANI HAWATAPASHA KIPORO HAWA RAIA HAWA, NNE KWA HISIA ZA HARAKA WALIPOKUWA WANAONGEA KWENYE SIMU WAKATI SIPO WALIKUWA WANAKUBALIANA NINI......🤔
 
Usipige mwanamke labda itokee una defend yourself. Huyo mwanamke siyo wako ni wajamii, maana yake una share na wenzako. Of cause sharing is caring, ila inabidi ujiridhishe matukio yao yalifanyika kabla au baada ya ndoa. Baada ya hapo fanya maamuzi magumu, ila si yale ya kuua na kujiua wewe kama yule mchizi wa mwanza.
 
Msikilize hicho anachotaka kukuambia, kisha mpe likizo akapumzike kwa Ima
🤔 Staki kumpa nafasi kumsikiliza tena kwenye hilo maana nilishampa nafasi nilipofika tu ye akadanganya ni shemeji yake kama nisingekuwa na ushahidi wa WhatsApp basi alikuwa ashanipiga chenga. Nikimpa nafasi tena atadanganya tu hapa nafikiria maamuzi tu ya kuchukua bs.
 
Usipige mwanamke labda itokee una defend yourself. Huyo mwanamke siyo wako ni wajamii, maana yake una share na wenzako. Of cause sharing is caring, ila inabidi ujiridhishe matukio yao yalifanyika kabla au baada ya ndoa. Baada ya hapo fanya maamuzi magumu, ila si yale ya kuua na kujiua wewe kama yule mchizi wa mwanza.
Mkuu hata kama walifanya kabla ya kuishi na mimi sasa wanaendelea kuwasiliana ili iweje mbaya zaidi tena kwa siri nikiwa sipo wanapigiana simu kuna amani kweli hapo mjomba...?🤔
 
Moja kati ya sifa za uanaume ni uwezo wa kuficha hisia zao za kweli kwa muda fulani hata kama inauma, sasa hapo umeshaanda mazingira ya wao kukubaliana na utaingizwa kingi ukija kutaka maelezo baadae.

Pale ulitakiwa uandae kila ushaidi ikiwa ni pamoja na kuendelea kuchati na huyo jamaa kiasi kwamba wakati unamuuliza hata hilo swala la yeye kusema "jamaa kaamua kujiandikia isingewezekana", na wakati unalianzisha ulitakiwa ulifikishe mwisho bila kumpa wakati wa yeye kukaa na kutunga namna ya kuja kukudanganya.

Kwasasa usije kusikiliza chochote atakachokwambia na hata huyo jamaa usimtafte atakuwa kampanga tayari,Mpe likizo huyo mwanamke.
 
Safi kabisa. Kabla hujafanya hivyo msikilize alichokuwa anataka kusema halafu mwambie aende zake ila tu kama nawe hujawahi mendea demu tangu umuoe vingine samehe muongee muyalize.
Mkuu kwenye uaminifu najitahidi sana sn huko nilishahama kbs. Bt hata kama nachepuka si ticket ya mke wangu naye kujaribu kufanya hivyo
 
Mkuu hata kama walifanya kabla ya kuishi na mimi sasa wanaendelea kuwasiliana ili iweje mbaya zaidi tena kwa siri nikiwa sipo wanapigiana simu kuna amani kweli hapo mjomba...?🤔
Unless kama ulimuoa akiwa na bikra zake mbili, ila hawa wanawake waliokula mileage kuna namna ya kukaa nao. Kama haja cheat wakati mkiwa kwenye ndoa tullia tu. Pengine huyo boya anasukumwa na nyege zake kutongoza mke wako na penzi hajapewa baada ya ndoa. Usifanye maamuzi ukiwa na hasira, endelea ku uncover information mpaka mwisho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom